Na Aron Msigwa – MAELEZO.
Jeshi la Polisi nchini limesema kifo cha askari Polisi WP.7338 PC Suzana kilichotokea katika kituo cha Polisi Tarime tarehe 4/7/2010 kilitokana na tukio la askari huyo kujipiga risasi kifuani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini ASP Advera Senso amesema askari huyo WP .7338 PC Suzana siku ya tukio hilo aliingia kazini asubuhi na baadaye kutakiwa kuelekea kwenye lindo kwa muda kuzuia magari yasiingilie msafara wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa na ziara wilayani Tarime siku hiyo.
Amesema siku hiyo msafara wa rais ulipofika alipokuwa PC Suzana uligawanyika gari la RPC Mara liliacha njia ya msafara na kuingia barabara ya Bomani kwenda ofisi ya DC likifuatiwa na magari mengine matatu likiwemo la Rais.
ASP Senso amefafanua kuwa eneo ulipogawanyikia msafara kuna kilima na kona kali iliyosababisha RPC Mara kupotezana na magari yaliyokuwa mbele yake na hivyo kushindwa uelekeo wa msafara.
Jeshi la Polisi nchini limesema kifo cha askari Polisi WP.7338 PC Suzana kilichotokea katika kituo cha Polisi Tarime tarehe 4/7/2010 kilitokana na tukio la askari huyo kujipiga risasi kifuani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini ASP Advera Senso amesema askari huyo WP .7338 PC Suzana siku ya tukio hilo aliingia kazini asubuhi na baadaye kutakiwa kuelekea kwenye lindo kwa muda kuzuia magari yasiingilie msafara wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa na ziara wilayani Tarime siku hiyo.
Amesema siku hiyo msafara wa rais ulipofika alipokuwa PC Suzana uligawanyika gari la RPC Mara liliacha njia ya msafara na kuingia barabara ya Bomani kwenda ofisi ya DC likifuatiwa na magari mengine matatu likiwemo la Rais.
ASP Senso amefafanua kuwa eneo ulipogawanyikia msafara kuna kilima na kona kali iliyosababisha RPC Mara kupotezana na magari yaliyokuwa mbele yake na hivyo kushindwa uelekeo wa msafara.
“Mara baada ya kuona amepotea RPC wa Mara alisimama alipokuwa PC Suzana na kutaka kujua kwa DC ni wapi, akawaonyesha njia ya mkato ambayo haikuwa rasmi iliyopangiwa msafara” amesema.
Amefafanua kuwa ilionekana PC Suzana alielewa kuwa RPC Mara alitaka kwenda Ofisi ya DC wakati yeye alitaka kuelewa njia ulipopita msafara. Baadaye RPC Tarime Rorya alimwagiza mkuu wa kituo Tarime apeleke askari mwingine eneo hilo na PC Suzana arudi kituoni umbali wa takribani mita 100 toka alipokuwa amepangiwa kazi.
Amesema PC Suzana alipofika chumba cha mashitaka aliendelea na kazi, baadaye kwa kushirikiana na askari mwenzake PC Dora waliaadaa makabidhiano ya zamu na wakati wakiendelea kuandaa ghafla PC Suzana alichukua silaha moja kati ya mbili zilizokuwa kwenye sanduku na kuingia kwenye ofisi ya mkuu wa kituo na kufunga mlango.
Amefafanua kuwa askari wengine waliokuwa kwenye chumba cha mashtaka walipoona hivyo walikwenda kwenye mlango alipoingilia PC Suzana na kujaribu kuuvunja ndipo akapiga risasi mlangoni na risasi hiyo kutoboa mlango kitendo kilichowafanya kurudi nyuma na baada ya muda walivunja mlango na kumkuta PC Suzana akiwa amejipiga risasi kifuani.
ASP Advera amesema Jeshi la Polisi limechukua hatua za kiutawala na kuboresha mwongozo wa namna ya kusimamia misafara kwenye mikoa ya kipolisi yenye makamanda zaidi ya mmoja chini ya mkuu wa mkoa mmoja, mafunzo kazini na vyuoni kuhusu namna ya kukabilianma na msongo (stress Management).
Hata hivyo amebainisha kuwa kifo cha WP Suzana ni suala linalohitaji uamuzi wa kisheria na jalada la tukio hilo limekamilishwa na kupelekwa ofisi ya wakili wa serikali kanda ya Ziwa kwa maamuzi ya kisheria.
Changa la macho hilo
ReplyDeleteTaarifa hii imeacha maswali mengi na imezidi kuchanganya. Inawezekanaje mtu kuambiwa kurudi ofisini na ukaamua kujiua hivi hivi? taarifa haisemi kama kulikuwa na kutishwa, kufokewa, kudhalilishwa n.k! nadhani taarifa imejaribu kuwalinda watu fulani au inawezekana taarifa ilieleza mambo yote ila mwandishi ameandika kwa ufupi na kuacha masuala ya msingi?
ReplyDeleteSounds 90% cooked!
ReplyDeleteBana michuzi kama kawaida yako. This is cooked and case dismissed.
Hongera jeshi la poliiiisi!
Maelezo ya jeshi la polisi kuhusu kifo cha PC Susana si ya kweli kwasababu mtu hawezi kujipiga risasi bila sababu. Tayari wameonyesha kwamba kulikuwa na confusion baina ya RPC Mara na PC Susana kutokana na maelekezo ya msafara. Hivyo basi she must have been threatened with disciplinary action something she must have thought was unreasonable. Actually, the threat must have been too grave for her to bear. Considering that the President was in the area, ili RPC aonekane wa maana sana, akatumia nguvu za ziada kuliko akili kama ilivyo kawaida yao. What we need is an independent inquiry not some cover-up as I expected.
ReplyDeleteYaleyale ya Zombe na wenzake, kufundishana cha kuongea. Hii taarifa inaonesha ni jinsi gani jeshi letu lilivyo butu na kutokuwa na uwezo wa kutumia logic katika kutengeneza report za kudanyia umma.
ReplyDeleteReport hii imezidi kuzua maswali mengi zaidi kuliko kama wangekaa kimya tu kwani watanzania ni wepesi wa kusahau na suala hili walikuwa wameisha lisahau.
Haiingii akilini, mtu kuitwa kituoni na kuendelea na kazi nyingine bila kufanyiwa unyanyasaji, harrasment na utawala na baadae aishie kujitwanga risasi zaidi ya moja kwa kutumia SMG kifuani. Maswali waliyotakiwa kuyajibu ni:-
1. Baada ya kuitwa kituoni ofisi ya mashitaka nini kilifuata kati yake na uongozi wa polisi mkoani?
2. alipokimbilia ofisi ya mkuu wa kituo na kujifungia walisikia risasi ngapi?,
3. "Unaposema askari wengine walipotaka kuvunja mlango alipiga risasi mlangoni na kutoboa wakarudi nyuma na baadae kuvunja na kukuta amejipiga risasi kifuani"
Swali hapa ni je kipi kilianza kati ya kujipiga risasi kifuani au kupiga mlangoni, maana taarifa haioneshi baada ya kupiga risasi mlangoni walisikia risasi ingine ndani na huenda ndiyo iliyomuua, maana yake ni kwamba PC Suzana alikuwa na uwezo wa kupiga risasi mlangoni baada ya kujipiga kifuani risasi nne. HAPA KUNA MASWALI ZAIDI YA 150 YANATAKA UFAFANUZI.
3. Hawakusema wakati PC Suzan anaingia ofisi ya mkuu wa kituo wakati wa kukabidhiana yeye mkuu wa kituo alikuwa wapi?, na kama hakuwepo iweje ofisi yake iwe wazi?, na kama alikuwepo ndani alijificha wapi?
4. Mwisho wamemalizia na suala la "Stress Management", stress hiyo ilitokana na nini hasa?,
KWA TAARIFA HII YA KISANII ISIYOKUWA NA TAALUMA YA KIINTELIJENSIA NA COMMON SENSE, INAONESHA WAZI KUWA JESHI LA POLISI HALIKUSEMA UKWELI KWENYE HILI SUALA NA WALICHOJARIBU NI KU "COVER" WHAT REAL HAPPENED - KWA ULE USEMI WA MTU AMEISHAKUFA HATA UKWELI UKIJULIKANA HAITASAIDIA KITU, KWELI PC SUZAN AMEKUFA KIBUDU KWENYE HILI SUALA. SIJASHAWISHIKA NA KUAMINI KUWA ALIJIUA, KIFO CHAKE KIKO MIKONONI MWA MTU NA MTU HUYO ANALINDWA. ILA MUNGU NDIYO MTOA HAKI:
NDIYO MAANA WAMEMPATIA LOW PROFILE KUJA KUTOA UPUPU HAPA KWA KUHOFIA KINA MWEMA WATAJEOPARDIZE CREDIBILITY YAO KWA KUTOA TAARIFA YA KICHEKECHEA KWA FORM SIX
Hapa kuna kitu hapa.
ReplyDeleteYawezekana hayo ndio kweli yaliyojiri, na inawezekana si kweli, yaani huo ufafanuzi ni 'cover up story', iliyopikwa ili kuuridhisha umma.
Marehemu ameshakufa, hivyo hatuwezi kusikiliza upande wake wa habari.
Samahani, sisi wengine tumeharibiwa kiasi na 'movies' na shuhuda mbalimbali za matukio ya kihalisia yanayohusu vifo mbalimbali.
Unajua sio kitu kigumu mtu kukumaliza kwa silaha (huku akiwa kaishikilia hiyo silaha na kitambaa au gloves ili aiache alama zake za vidole kwenye silaha), kisha baada ya kukumaliza anakushikisha (marehemu) hiyo silaha ili alama zako za vidole (finger prints) wewe marehemu zibakie kwenye silaha?
Lakini kwa sasa mpaka uchunguzi wa huyo wakili utakapo malizika, ngoja tukae kimya kwanza, maana ina wezekana kuwa ni kweli alijimaliza mwenyewe akiogopa kuwa labda pengine kuna kitu angefanywa na 'wakubwa' kwa kutoa maelekezo ambayo siyo, kama ilivyoelezwa na mtoa taarifa. Nimesikitika sana, maaana binadamu yeyote hukosea, na kama mtu akikosea anaelekezwa tu, labda kama akiwa na shingo ngumu (mkaidi) ndio unamchukulia hatua.
Marehemu na apumzike kwa amani.
hakuna lolote na haoleti maana, bado hamjanishawaishi
ReplyDeletemi sijaelewa, yaani RPC pamoja na dereva wake hawajui ofisi ya DC ilipo?
ReplyDeleteHII RIPOTI NI KICHEKESHO KAMA MCHEZO WA KUIGIZA WALA HAINGII AKILINI MWA WAKUBWA. KWANZA HAELEWEKI IKO KAMA YA MTOTO WA VIDUDU AKIULIZWA NA BABA YAKE KWA NINI UMEMPIGA MWENZIO. LAZIMA KUNA VITISHO VYA HUYO RPC KWA DADA YETU MPENDWA VILIKUWEPO NA HADI AKAFIKIA MAAMUZI YA KUJIUA NA SI VITSHO VYA NDANI YA KISHERIA KAMA VILIKUWA NDANI YA SHERIA SIDHANI KAMA ANGEAMUA KUJIUA KWANI HATAKAMA ANGEFIKISHWA MBELE YA VYOMBO VYA DOLA SANA SANA ANGEFUKUZWA KAZI NA KUFUKUZWA KAZI SI MWISHO WA MAISHA MU HAWEZI KUJIUUA ETI KWA VILE ATAFUKUZWA KAZI. NI LAZIMA KULIKUWA NA MANENO YA VITISHO NA KASHFA ZA KIJINSIA KWA HUYU DADA, MANENO YA VITISHO BEYOND HUMANITY, MANENO YA KUDHALILISHAJI. AFTER ALL YEYE NI RPC WA MKOA ATAULIZAJI NJIA YA KWA MKUU WA WILAYA WAKATI ANAFANYIA KAZI MKOA HUO HUO, HII INAONYESHA JINSI GANI HAJUWI KAZI YAKE KIASI KWAMBA HAJUWI OFISI ZA WAKUBWA WENZANKE NDANI YA MKOA WAKE WA KIPOOLISI,THAT IS A JOKE! JAMANI HATA KAMA UMEUPOTEZA MSAFARA WA RAIS IS THAT A BIG DEAL IN TANZANIA! KWANZA ATAUPOTEZAJE MSAFARA WA RAIS KATIKA WILAYA NDOGO KAMA HIYO! HUYURPC ATAKIWA ASIMAMISHWE KAZI HADI UCHUNGUZI UTAKAPO KWISHA NA HII NI KAZI YA SAID MWEMA AKISHIRIKIANA NA WAZIRI HUSIKA HAYO NI MAISHA YA MTU SI MASIHARA. NA RAIS PIA ATAKIWA KULIJUWA SWALA HILI KIFO CHA MTU MMOJA SI KIDOGO NI SAWA TU NA VIFO VYA WATU MILINI KWANI VIFI HAINA UWINGI NA VYOTE VINA DHAMANI SAWA KIWE CHA RAIS AU MASIKINI WA BARABARANI VYOTE VINA UZITO SAWA NA WABUNGE WANATAKIWA KULIVALIA NJUGA JAMBO HILI HASA MBUNGE WA ENEO HUSIKA AMBAYE SASA HIVI KAMA SIKOSEI ANAHANGAIKA KUTAFUTE RE-ELECTION, WANANCHI HUYU MBUNGE ATWANGWE SDWALI LA HUYU DADA ALIYEULIWA MIMI NITWA AMEULIWA KWA VILE AMEKUFA KUTOKA NA MANYANYASO YA RPC. KWANZA RPC UTAPOTEAJE NJIA KATIKA MKOA WAKO WA KIPOLISI NAYE PIA NI MZEMBE ANATAKIWA AVULIWE HUO U-RPC PIA WANANCHI WA KAWAIDA WA ENEO HUSIKA MKISHIRIKIA NA NA NDUGU WA SUANA FUATILIENI HILO SWALA NA MULIFIKISHE SEHEMU ZA SHERIA NA BUNGENI, NA WANASHERIA PIA MSIKASE KIMYA, WAANDISHI WA HABARI PIA HII NI KAZI YENU, TUNATAKA NCHI YA UTAWALA BORA WA HAKI NA SHERIA USIO NA UPENDELEO WA UWAJIBIKAJI. MWISHO RAIS HII PIA NI KAZI YAKO USIKAE KIMYA TU. TUTAKU-JUDGE UTENDAJI WAKO PAMOJA NA HILI, LINAUMA SANA.
ReplyDeletehakuna lolote hii taarifa haijatulia hata kidogo,ninachojua mimi jeshi la polisi limeficha hii report na badala yake wameshindwa kuweka ule ukweli kamili,mana iweje mtu pasipokuwa na tatizo aweze kujipiga risasi,hapa ni kuwa kuna mkubwa amefichwa ili asiweze kutambuliwa,lakini sawa ndyo TZ yetu hii ya ari mpya na kasi mpya........pole sana wafiwa.
ReplyDeleteAAH MBONA HAPA HUYU MKUU RPC ALIKOSEA NJIA TUU YEYE MWENYEWE NA HII YOTE AMECHORA TUU KWA KUOGOPA KUWAJIBISHWA NA MKWERE. RPC KUPOTEA NJIA KWENYE MSAFARA WA RAISI NI SAWA NA MKUU WA USALAMA KULALA WAKATI RAISI ANATAKA KUPINDULIWA. HAPO PANATAKIWA EXTERNAL DITECTIVES UTAONA WATU WATAKAVYOTOA MACHO.
ReplyDeleteASP ADVERA ULIYOYAONGEA HAPA YANAHUSU KIFO CHA MTU HIVYO USIFIKIRI MAMBO NI RAHISI KIASI HICHO...
ReplyDeleteNI VIGUMU KUKUBALI AU KUKATAA TAARIFA HII LAKINI HATA IKOSOMWA KWA MGONJWA WA AKILI NI WAZI ATAJUA HII NI DANGANYA TOTO TUU...
HAPO MMEELEZA MATUKIO YA MUDA MFUPI KABLA YA MAUTI KUMFIKA INGAWA MMESAHAU KUSEMA KABLA YA KUJA KITUONI ALIKUNYWA CHAI AU UJI WA ULEZI''''''
SWALI LA MUHIMU HAPA.........
KAMA AFANDE SUZANI HAKUUWA, NI KWANINI AFANDE SUZANA ALIJIUA ????
AU KWA NINI AFANDE SUZANA ALIINGIA OFISINI AKIWA HAI NA BAADAYE IKAKUTWA MAITI YAKE???
KWA SABABU KUNA MAWILI HAPA??
ALIJIUA BAADA YA KUPATA VITISHO TOKA KWA WATU AMBAO WAMEFUNIKWA KATIKA TAARIFA HII AU ALIUAWA NA MTU ALIYEKUWAPO NDANI BAADA YA MLANGO KUFUNGWA...HUWEZI JUA!!!!
MUNGU YUPO NA NDIE ATAKAYELIPA KISASI NA KUHUKUMU...
ONI: TUNAOMBA OFISI MUHIMU KAMA HIZO ZIWEKEWE CAMERA ZA CCTV ILI WAKATI WA UCHUNGUZI ZISAIDIE
ULALE MAHALI PEMA PEPONI AFANDE SUZANA
nadani SMG ni ndefu kiasi cha kujilipua kifuani. ingekuwa kidevuni au hata mdomoni ni rahisi kuamini.
ReplyDeletekuna jambo hapa
nilikuwa sifuatilii hii stori leo ndio nimeisoma na kwa jinsi ninavyolijua jeshi letu la polisi na mazingira ya kifo, ukweli umefichwa na sidhani kama alijiua na hao maafande wenzake wana siri kubwa
ReplyDeleteKaka Michuzi huo ni uongo mtupu. Wanajaribu kutudanganya kama watoto wadogo Mungu yupo na atatoa ukweli tu.
ReplyDeleteHuyu askari inaonekana hakupewa kazi ya msafara.
ReplyDeletemsafara unaingizwa hapa ili kumfanya mzembe na mkosefu. Lazima alitiwa kashkash za kushtakiwa,taburu, kufutwakazi na kufungwa juu KWA KUHARIBU MSAFARA WA AMIRI JESHI MKUU.
PIA SIMLAUMU MAREHEMU KWA CHEO CHAKE KIDOGO, NA HUENDA KISOMO CHAKE KAMA TUNAVYOJUWA POLISI NI VIHIYO #1 DUNIANI.
WA KULAUMIWA NI VIONGO WANAOAJIRI NA KULIPA MISHARA KIDUCHU.
WE MSAFARA WA RAISI RPC HAJUI NJIA?
AFADHALI WENZANGU MMEONA HAYOO...MAMBO YA STRESS HAPA YANAASHIRIA KABISA KUNA UENEVU......
ReplyDeleteHapa niongee kama mnoko niliyeona nimepotea njia nikautosa Upolisi. Ninavyokifahamu hicho chombo kwa manyanyaso kinaongoza. Ukianza na mkuu wa kituo, mkuu wa polisi wa wilaya, wa mkoa na hadi huko makao makuu, ni balaa tupu. wanajifanya miungu watu. Ni matusi na vitisho kwa kwenda mbele. Shule zao zenyewe ndogo hivyo wanategemea vyeo kwa kujikomba.
ReplyDeleteSiyo ajabu huyo Pc alifokewa nakutishwa na kwa kuwa na roho ndogo akaamua kujiua. Kwanza siyo Mhehe kweli.
Mimi niliamua kuondoka kwani nilijua ningebaki humo nisingejiua bali ningeua ili iwe fundisho na kwa wengine
Yaani, uzembe utokee polisi, kifo kitokee polisi, polisi wajichunguze wenyewe, halafu wajisafishe..halafu sisi tusema Yes sir?
ReplyDeleteHaya tumekubali!
Jamani tusitumie JAZBA hebu twende hatua kwa hatua. Tuanze na wale tulioisikia habari hii zamani mioyo ikapoa, twende ngazi ya pili tuliotoneshwa vidonda na tatu kwa walioisikia leo kisha TUPIME yaliyojiri.
ReplyDelete1. Katika ile habariya kwanza tuliambiwa kuwa marehemu alikuwa amepangwa katika msafara kisha akaupoteza
2. Aliambiwa arudi kituoni na alipofika kaunta akachukua silaha ya moto akajilipua (TENA kuna mdu akahoji "Iweje mtu kama huyo aruhusiwe kuwa na silah kama amerudishwa kituoni?" Mwingine akahoji "Hiyo silaha aliipata wapi?" Kwani matrafiki wengihuwa hawatembei na silaha hata virungu tu huwa hawabebi. Sasa swali, yule aliyeeleza kuwa alijilipua akiwa kaunta alijuaje? Na hii ya ofisini imekujaje? Ipi ni ya kweli?
3.Aliingi ofisini akajifungia. SWALI? Walikuwa wanamfwatilia kila alipokuwa anaenda? kwasababu tukiumia mantiki, mf. mimi nafanya kazi labda benki, nikienda kwa meneja watu wanakuja kuvunja mlango? Hata kama nafanya kazi polisi, nimeingia ofisini kwa mkuu wa kituo watu watajuaje kama nimejifungia? Watu watajuaje kama naenda kujiua? KUNA WALAKINI?
4. Hivi kuna bastola za S.M.G? HAINGII AKILINI! Kama hakuna sasa inakuwaje mtu ukajipiga kifuani na S.M.G?
5. Wale waliovunja mlango eti walisikia risasi wakarudi nyuma alafu wakaena kuvunja mlango? Hata mtu ambaye ni retarded hataamini. Kweli mafunzo gani ya polisi ambayo unajua kunaadui nani mwenye silaha hujui kakaa angle gani kisha uvunje mlango? KWELI?
6. Kwanini akajiulie ofisi ya mkuu wa kituo? Kama privacy niyo aliyoitafuta kwanini asiene chooni? Kama kwa mkuu wa kituo kulikuwa na silaha, jee iliachwa iko full loaded? yaani imejazwa risasi?
7.Nilikuwa najiuliza kwanini nchi yetu imejaa majambazi bila kupata jibu LAKINI leo nimejua. Hivi kama RPC hujui ofisi ya DC ilipo kweli utajua kitongoji gani kina magaidi? Hivi sis watanzania tutaacha lini kuwa mambumbumbu? narudia MAMBUMBUMBU?
Ivi ukitaka kujiua unajifungia ofisini kwa mkuu wako ili. Si unaingia mitini tu. mbona tuliambiwa alikuwa arrested akawekwa chini ya ulinzi sasa yamekuwa haya. Hili ni tatizo lakuwa na jeshi la polisi form 4/6 leaver wanafikiri kila mtu anauwezo wao wakuelewa mambo. Jeshi limeoza hilo safisheni au jipu litawapasukia siku moja hakutakalika.Nimeona kamanda Tibaigana anagombea ubunge. lol kweli Bongo tambarare.
ReplyDeleteHaki ya nani! yani ni heri wangenyamaza tu..Inatia hasira
ReplyDeleteyaani nimefurahia comments zote hakika watanzania tuna akili sana. The way mnavyoanalyse mambo mnaonekana ni watu wenye uelewa sana na si watu wa kuburuzwaburuzwa. Napenda kuwaambia viongozi wetu kuwa zile zama za ujinga/ujima za kuburuzana zimeshaisha. Mkae mkijua mnaongoza watu wenye ufahamu wa juu. Nyakati kama hizi sitegemei mtu kama msemaji wa polisi kuita waandishi wa habari na kuanza kuongea kama mtu ambaye hajaenda shule. Viongozi wetu hakikisheni mkija mbele ya umma mnakuja na hoja za maana msiwafanye watu wajinga mambumbu hawaelewi kitu. Yaani watu wote waliocomment wanaonekana ni waelewa kupitia maelezo yao tu yaani wangekuwa mapolisi wazuri wanaoongoza mambo kisomi. Viongozi wetu acheni longolongo hizi zimeshapitwa na wakati mnajitia aibu jamaniiiiii eeeh!
ReplyDeleteAliye kufa kafa - hilo kweli changa la macho mtu mwenye akili zake hadanganyiki na maelezo yaliyoandikwa hapo; lazima kuna jambo aidha RPC au mkubwa fulani alimtakia marehemu ambalo halikuwa zuri hivyo kupelekea kifo chake, wenzetu polisi ile kuwa polisi tu wengi wao wanaona kuwa wanaweza kuwahadaa wanananchi kwa maelezo yao na wanasahau kuwa kuna watu hata bila ya kwenda shule wana vipawa vya kung'amua ukweli wa jambo.
ReplyDeleteUshauri wangu kwa polisi ajirini wasomi au someshini watu wenu, unakuta mtu anacheo kikubwa lakini elimu yake ni duni ndio maana kuna kuwa na mambo ya ajabu ajabu katika jeshi la polisi, mtu aliye na elimu yake kamili aliyo isomea hawezi kuwa na maamuzi na unyanyasaji usiokuwa na msingi. POLISI ELIMU IWE KIGEZO KIKUBWA ndipo amani itapatikana.
ReplyDeleteyani makes NO SENSE NO SENSE...yani unajiua kwa rasasi ya kufua?really haki duhhh mie m not buying hiyo story huwezi kujiua kwa kujipiga risasi ya kifua
ReplyDeleteAMA KWELI MAAJABU HAYATAISHA KATIKA DUNIA HII...LOGIC NI NDOGO TU HAPA....KWELI UTUMIE SMG HALAFU UJIPIGE RISASI KIFUANI?MTARIMBO ULE ULIVYO MZITO NA MREFU...KWANZA UNAILENGAJE HAPO KIFUANI NA UNAFYATUAJE?MAANA NIMESHAKUWA FAMILIAR NA SILAHA KAMA HIZO...SMG NI NDEFU HALAFU SEHEMU YA KUFYATULIA IKO KATRIBU NA MWISHONI SASA IMAGINE UMEIGEUZA ILI UPANDE WA MTUTU NDIO UWE KIFUANI FANYA TU MAHESABU YA HARAKAHARAKA KWA WALE WENYE UZOEFU NA SILAHA JAMANI...HEBU TUCHANGUE BONGO ZETU KATIKA SCENARIO YA NAMNA HII...PLEASEEE!!!AKILI SI TUNAZO JAMANI......
ReplyDelete....Mbaya zaidi wanajaribu kuhusianisha na kujiua kwa baba yake mzazi ili ionekane ni tabia ya kurithi kwao kujiua....
ReplyDeleteKWA JINSI NIJUAVYO JESHI LETU LA POLISI NA WELEDI WAKE HAPO LAZIMA SUZY ALITUKANWA SANA, ALITISHIWA SAANA NA KUDHALILISHWA SAANA NA UKIZINGATIA YY NI MWANAMKE NA AKONA MBELE HAKUONEKANI,NDO KUAMUA ALICHOKIFANYA
ReplyDeleteTeh, teh, teh! nawacheka nyie mnaojaribu kutudanganya! Hiireport hata mkiwasomea watoto ng'aaa, lazima na wao wata waumbua hata kwa kulia.
ReplyDeletemnatia aibu!! loo!
laiti mngejua mnaudhi watu msingeangaika kuandika uongo.
Nimesikitishwa na taarifa nzima na nadhani kuna haja ya kuandaa taarifa kitaalamu. Kuna mapungufu mengi ambayo yanaashiria au kuleta mashaka. Inatia shaka, RPC kutojua kwa DC au njia. Hivi RPC hakujua Rais anapita njia gani, mmh! na je gari lake lilikuwa mbali kiasi gani mpaka asiwaone waliotangulia hasa kwenye barabara zetu za vumbi(si angefuata vumbi tu, tehe, tehee!). Kama sijakosea huyu PC aliambiwa akazuie magari yasiingilie msafara na si kuongoza msafara. Je ni kweli ari ilitaka arudi kuendelea na kazi au ashughulikiwe?. Kwa vyovyote itakavyokuwa katika jibu la swali kwa nini askari mdogo aruhusiwe kukabidhi zamu, hakukua na mkuu wa zamu ambaye ndo nadhani anaruhusiwa kukabidhi yote haya na mwiso Ofisi ya mkuu wa Kituo ilikuwa wazi kiasi cha kila askari/mtu kuingia na ndiye eti akajifungia. kumbe ofisi ya muu unaweza kuifunga halafu hakufunga. Mkuu Mzembe. Na hayo mafunzo yangeandaa na RPC na OCS ya namna ya kuongoza misafara na umakini kazini.
ReplyDeleteWafiwa poleni na polisi hizi ni changamoto. Msitoke hadharani na ripoti kama hizi jamani.
Nafikiri kama angekuwa amefungiwa 'black box' kusingepaswa kuwa na 'press release' hii ya kupandikiza. Bongo kaazi kweeeli kweli.
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
nyie jeshi la polisi hukoo tarime semeni namna hii tulimpiga risasi nne za kifuani full stop, watu wote duniani ambao wanajimaliza kwa risasi wanatumia pisto kujichakaza tena moja tu ya bichwa au mdomoni na sio kifuani tena nne looo hili ni changa la mwili mzima, hata kwa pisto tuu kujielekezea kifuni bado itaenda usawa wa shingoni tu, haiingii kwa oblangata libinduki lilivyo lirefu alilishikaje kulielekeza kifuani kwake? kama ni hivyo ingetungua maeneo ya shingo chini ya kidevu, yaleyale majambazi yalikuwa yanarushiana risasi na polisi tukayashinda tukayaua, mkienda eneo la tukio hamna kitu, nyie polisi wa bongo mnapenda sana kuua wenzenu mnadhani mtaishi milele? hata nyie mtakufa tuu!
ReplyDeletehawa polisi sasa wamechoka kuonea raia wanaanza kuoneana wenyewe!
ReplyDeleteWatanzania kwa usanii na waaminia ila kwa hii ripoti,adanganyiki mtu hapa. Mapungufu na maswali ni mengi sana kwenye ripoti sijui hata kwanini imetolewa! Ila taambueni mwaweza daganya umma lakini hamuenzi danganya nafsi zenu. Hongereni kwa dhuluma zenu.
ReplyDelete