JK na mtoto Frank Charles Valia(9) ikulu mjini Dodoma leo asubuhi ambapo mtoto Frank alikwenda kumshukuru Rais kwa kugharamia matibabu yake nchini India baada ya kupata ulemavu kufuatia ajali aliyopata kwa kuanguka kutoka juu ya mti.
JK na mkewe Mama Salma Kikwete(kushoto) wakiwa na mtoto Frank Charles Valia (9) ikulu ya mjini Dodoma leo asubuhi.Mtoto huyo Frank(watatu kushoto) na baba yake mlezi Khamis Said(wapili kushoto) walikwenda ikulu ya Dodoma kumshukuru Rais Jakaya Kikwete aliyegharamia matibabu ya Fank huko India ambapo anatarajiwa kurudi baada ya miezi sita.Mtoto Frank alipata ulemavu wa kupinda mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti.

JK. MTU WA WATU, MPENDA WATU. UONGOZI WAKO UMETUKUKA. ISINGEKUWA USALAMA WAKO, UNGEUNGANA NA WALALA HOI MITAANI KUCHEZA KIDUKU. HUYU NDIYE JK AMBAYE VISION YAKE KIUNGOZI NI KUBWA. NAAMINI AKIPEWA MUDA WATU TUTASAHAU MACHUNGU. ILA CHONDE CHONDE MZEE, MAMBO YA KUPEANA VYEO KIRAFIKI YATAKUANGUSHA MIAKA MITANO IJAYO, NAJUA UTASHINDA URAIS, WATU WAPENDE WASIPENDE MAANA BINAFSI UNAKUBALIKA NA UNA MVUTO MKUBWA. PUNGUZA IDADI YA WIZARA, CHAGUA WATU MAKINI KAYIKA VIZARA HUSIKA, TAFUTA WASOMI LUKUKI ULIONAO NDANI NANJE YA NCHI WAKUSAIDIE.
ReplyDeleteGod bless the boy. Thank you Jakaya Kikwete
ReplyDeleteBless his soul how unfortunate.
ReplyDeleteHii imenitachi kusema kweli.Katika njia zote za kupatia kura hii naikubali mana ina manufaa kwa jamii.Mungi ibariki Tanzania
ReplyDeleteGOOD STUFF MR KIKWETE, THAT IS WHAT WE WANT, TAKE CARE AND KEEP EYES ON YOUR PEOPLE, YOUR DOING RAELLY GREAT SIR. GOD BLESS TANZANIA, GODBLESS OUR PEOPLE IN TANZANIA AND GOD BLESS LITTLE BOY.
ReplyDeleteMDAU WA UK.
Kutoa ni Moyo sio Utajiri. Mungu akuzidishie maisha marefu yenye Amani na uzidishe upendo kwa watu wako. We love you JK. May Allah Bless
ReplyDeleteKutoa ni moyo hasa kipindi hiki cha Uchaguzi.Lazima mtu utumie akili yako vizuri kupitia hizi media.
ReplyDeleteJK, Mungu Akubariki kwa wema na huruma yako, Rais wetu mpendwa!
ReplyDeleteHizi si kampeni, huu ni utu wake, wema wake na huruma zake ambazo amezionyesha muda wote kusaidia Wananchi wake wote na hasa wale wenye matatizo makubwa kama haya!
Tunaomba na kusali uzidi kubarikiwa na upate uwezo zaidi
kutuongoza na kusaidia wote!
Na si yeye tu na Mama Salma nae ameonyesha mara nyingi tu kuwa mstari wa mbele kusaidia wenzetu maskini kama hawa!
Sisi tunafarijika sana kuwa na Kiongozi asiependa makuu, mwenye huruma na yuko mstari wa mbele kuwajali maskini wa Mungu.
Mungu awabariki nyote, Amina.
Storming
www.uksokainbongo.blogspot.com
www.sokainbongo.com
Unajitahidi baba,wote na mkeo mmpewa moyo wa huruma kwa wenye shida hilo tunalijua.Ila timu ya wachezaji wako wanakuangusha. Achana rafiki zako hao wamejaa ubinafsi toka mioyoni hadi kwenye nyayo zao,hebu angalia hata mikoani wapo watu waadilifu na wenye uchungu wa nchi wasionunulika watasaidia taifa letu. Jipange sawasawa naamini Mungu atakusaidia safari hii. Chondechonde tuulimarishie miundo mbinu hasa Umeme ( huu utaleta wawekezaji) na barabara kuunganisha mikoa yenye resources za kuinua uchumi wa nchi.
ReplyDeleteFungua blog ambayo utapata mawazo toka kwa watu wa kada mbalimbali kwa uhuru kwa manufaa ya inchi yetu.