JK na mtoto Frank Charles Valia(9) ikulu mjini Dodoma leo asubuhi ambapo mtoto Frank alikwenda kumshukuru Rais kwa kugharamia matibabu yake nchini India baada ya kupata ulemavu kufuatia ajali aliyopata kwa kuanguka kutoka juu ya mti.

JK na mkewe Mama Salma Kikwete(kushoto) wakiwa na mtoto Frank Charles Valia (9) ikulu ya mjini Dodoma leo asubuhi.Mtoto huyo Frank(watatu kushoto) na baba yake mlezi Khamis Said(wapili kushoto) walikwenda ikulu ya Dodoma kumshukuru Rais Jakaya Kikwete aliyegharamia matibabu ya Fank huko India ambapo anatarajiwa kurudi baada ya miezi sita.Mtoto Frank alipata ulemavu wa kupinda mgongo baada ya kuanguka kutoka juu ya mti.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    JK. MTU WA WATU, MPENDA WATU. UONGOZI WAKO UMETUKUKA. ISINGEKUWA USALAMA WAKO, UNGEUNGANA NA WALALA HOI MITAANI KUCHEZA KIDUKU. HUYU NDIYE JK AMBAYE VISION YAKE KIUNGOZI NI KUBWA. NAAMINI AKIPEWA MUDA WATU TUTASAHAU MACHUNGU. ILA CHONDE CHONDE MZEE, MAMBO YA KUPEANA VYEO KIRAFIKI YATAKUANGUSHA MIAKA MITANO IJAYO, NAJUA UTASHINDA URAIS, WATU WAPENDE WASIPENDE MAANA BINAFSI UNAKUBALIKA NA UNA MVUTO MKUBWA. PUNGUZA IDADI YA WIZARA, CHAGUA WATU MAKINI KAYIKA VIZARA HUSIKA, TAFUTA WASOMI LUKUKI ULIONAO NDANI NANJE YA NCHI WAKUSAIDIE.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2010

    God bless the boy. Thank you Jakaya Kikwete

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2010

    Bless his soul how unfortunate.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2010

    Hii imenitachi kusema kweli.Katika njia zote za kupatia kura hii naikubali mana ina manufaa kwa jamii.Mungi ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2010

    GOOD STUFF MR KIKWETE, THAT IS WHAT WE WANT, TAKE CARE AND KEEP EYES ON YOUR PEOPLE, YOUR DOING RAELLY GREAT SIR. GOD BLESS TANZANIA, GODBLESS OUR PEOPLE IN TANZANIA AND GOD BLESS LITTLE BOY.

    MDAU WA UK.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2010

    Kutoa ni Moyo sio Utajiri. Mungu akuzidishie maisha marefu yenye Amani na uzidishe upendo kwa watu wako. We love you JK. May Allah Bless

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2010

    Kutoa ni moyo hasa kipindi hiki cha Uchaguzi.Lazima mtu utumie akili yako vizuri kupitia hizi media.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2010

    JK, Mungu Akubariki kwa wema na huruma yako, Rais wetu mpendwa!
    Hizi si kampeni, huu ni utu wake, wema wake na huruma zake ambazo amezionyesha muda wote kusaidia Wananchi wake wote na hasa wale wenye matatizo makubwa kama haya!
    Tunaomba na kusali uzidi kubarikiwa na upate uwezo zaidi
    kutuongoza na kusaidia wote!
    Na si yeye tu na Mama Salma nae ameonyesha mara nyingi tu kuwa mstari wa mbele kusaidia wenzetu maskini kama hawa!
    Sisi tunafarijika sana kuwa na Kiongozi asiependa makuu, mwenye huruma na yuko mstari wa mbele kuwajali maskini wa Mungu.
    Mungu awabariki nyote, Amina.
    Storming
    www.uksokainbongo.blogspot.com
    www.sokainbongo.com

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2010

    Unajitahidi baba,wote na mkeo mmpewa moyo wa huruma kwa wenye shida hilo tunalijua.Ila timu ya wachezaji wako wanakuangusha. Achana rafiki zako hao wamejaa ubinafsi toka mioyoni hadi kwenye nyayo zao,hebu angalia hata mikoani wapo watu waadilifu na wenye uchungu wa nchi wasionunulika watasaidia taifa letu. Jipange sawasawa naamini Mungu atakusaidia safari hii. Chondechonde tuulimarishie miundo mbinu hasa Umeme ( huu utaleta wawekezaji) na barabara kuunganisha mikoa yenye resources za kuinua uchumi wa nchi.

    Fungua blog ambayo utapata mawazo toka kwa watu wa kada mbalimbali kwa uhuru kwa manufaa ya inchi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...