MHESHIMIWA KAIMU BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA, BWANA CHABAKA F. KILUMANGA AKIPOKEA NEMBO MAALUM KUTOKA KWA BWANA JEAN-PAUL DE LA FUENTE, KAMA TUNZO MAALUM KWA NCHI YA TANZANIA KWA KUTINGA FAINALI KUTOKA KWA SHIRIKA HILO LA NEW 7 WONDERS.


MLIMA KILIMANJARO UMETINGA RASMI KWENYE FAINALI ZA KUTAFUTA NEW 7 WORLD WONDERS OF THE WORLD YAANI MAAJABU 7 YA DUNIANI. TUNASHUKURU BWANA ANKAL KAMA ULIVYORIPOTI HAPO SIKU ZA NYUMA TUUPIGIE KURA MLIMA WETU, KWENYE MTANDAO HUU WA JAMII.
WAKATI WA TAARIFA HIZO, MLIMA KILIMANJARO ULIKUWA NDANI YA ORODHA YA MAAJABU 406 YA DUNIA KATIKA KINYANG'ANYIRO HIKO. HIVI SASA KWENYE ORODHA HIYO YAMEBAKIA MAAJABU 28, NA MLIMA WETU WA KILIMANJARO UNASHIKA NAFASI YA 8. KURA ZA MAONI BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA SEHEMU MBALI MBALI DUNIANI KWA KUWASHIRIKISHA WADAU WA MATAIFA YOTE.
MATAIFA YENYE MAAJABU YAO YA ASILI YA KUJIVUNIA YAMEANZA KUPIGA KURA KWA KASI. HAKIKA NI VYEMA NA NI WAJIBU WETU WATANZANIA WOTE TUENDELEE KUUPIGIA KURA MLIMA WETU, ILI UWEZE KUPANDA CHATI NA KUWA MSHINDI KATIKA FAINALI HIZO.

TAARIFA HIZI ZA MLIMA KILIMANJARO KUTINGA FAINALI, ZIMETHIBITISHWA RASMI JANA NA MKURUGENZI WA NEW 7 WONDERS, BWANA JEAN-PAUL DE LA FUENTE,ALIPOTEMBELEA NA KUFIKISHA RASMI HABARI HII KATIKA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA. BWANA JEAN-PAUL ALIKARIBISHWA UBALOZINI NA MHESHIMIWA KAIMU BALOZI, BWANA CHABAKA F. KILUMANGA.

TAARIFA RASMI ITAFUATIA BAADE KUHUSIANA NA JAMBO HILI MUHIMU, AMBALO LITAPANDISHA CHATI NCHI YETU DUANIANI KATIKA SEKTA YA UTALII NA UWEKEZAJI, NA KUONGEZEKA KWA AJIRA NCHINI, KAMA ILIVYOKUWA KWA WASHINDI 7 WA MARA YA MWISHO KATIKA KINYANG'ANYIRO HIKO,AMBAO WALIPATIKANA MWAKA 2007, TAKWIMU ZINAONYESHA SEKTA YA UTALII KWA NCHI ZAO IMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 2.
WASHINDI WA MARA YA MWISHO, WATAALAM WANASEMA WALIKUWA KUTOKANA NA MAN MADE 7 WONDERS (MAAJABU 7 YALIYOTENGENEZWA NA BINADAMU), NA SASA HIVI NI NATURE NEW 7 WONDERS YAANI (MAAJABU 7 YA ASILIA). HAKIKA MLIMA WETU KILIMANJARO UNASTAHILI KUWEKO KWENYE ORODHA HII, NA NI JUKUMU LETU WATANZANIA KUPIGA KURA KUHAKIKISHA MLIMA WETU UNASHINDA.


KWA HABARI ZAIDI NA KUPIGA KURA, TEMBELEA: http://www.new7wonders.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    JAMANI TUPIGIE KURA MLIMA KILIMANJARO, RAHA JIPE MWENE, JUST SO SIMPLE, MCHEZA KWAO HUTUZWA. IT TAKES JUST FIVE MINUTES TO FINSH GUYS.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2010

    TUNAFURAHI SANA KWASABABU WANAUPENDA MLIMA WETU, "TUWE MAKINI PALE WANAPOUTUMIA KWA MANUFAA YAO" TUSIKUBALI MALIZETU ZA ASILI KUTUMIWA/TUMIKA. HAWA HAWA NDIO BAADAE WATASEMA MLIMA WETU UMESHUNGA NGAZI YA KUMI."TUUNDE CHOMBO MADHUBUTI KITAKACHOTANGAZA MALI ASILI ZETU TUZIENZI SISI WENYEWE KIMATAIFA"

    ReplyDelete
  3. watani wetu wa jadi akina Kamau wako wapi? hapo ndo wangetusaidia after all huu mlima uko kwao(wink wink)

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2010

    Watalii wakija kuuona Mlima ndo katusaidia hapo wewe mdau unayeuliza akina Kamau wako wapi? Siyo siri kwamba wageni ndio wanaothamini mlima sana kuliko wenyeji. Wenye kulala wazidi kulala... Ama umesahau kwenye miti hamna wajenzi? Si ajabu Misri wanatumia maji za ziwa victoria wakati mataifa kama Kenya, Tanzania na Uganda bado tatizo la maji lipo. Mambo ndo yale yale au mnasemaje wadau... Tunalalamika kwamba akina Kamau wanadai mlima uko kwao lakini wengi wetu hata kuukwea hatujawai nazungumzia ujumla. Sasa jee kama hatutaki akina Kamau waje basi nasisi tuende kule basi... hilo pia tunaona kazi. Kuukwea hatutaki. Wakija akina kamau Kuukwea tunasema ooh wandai mlima ni wao. Haya kazi kwenu wadau wenzangu mambo ya EAC na sisi tuendeni Kenya na kutangaza vivutio vya huko. Kwani kakatazwa mtu kutalii Kenya?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...