Alma Eno kabla ya kuanza mchezo
Alma na play writer Greg Freeman

Alma na wenzie
Alma na Cast nzima ya BEAK STREET

ENGLAND BEAK STREET
by GREG FREEMAN
(it's dog - eat - dog in a cat world)
TIME OUT's
No1 Critics' Choice**** Show

Msanii wa maigizo na filamu mwenye asili ya kitanzania Alma Eno, ameng'ara na kutikisa ulimwengu wa Theatre mjini London kwenye onyesho la mchezo uitwao BEAK STREET ulioandikwa na mwandishi maarufu Greg Freeman, na kuongozwa na Ken McClymont.

BEAK STREET ni mchezo wa kijangili ulio kwenye ulimwengu wa Mapaka. Mchezo huo umekuwa ukionyeshwa kwenye kitongoji cha West End mjini London, ambacho ni maarufu kwa majumba ya maigizo,sinema na starehe.

Beak Street imeonyeshwa kwa wiki 24 sasa katika majumba ya Tabard Theatre na Theatre Delicatessen (Sekunde 30 kutoka Selfridges) Alma Eno anacheza silka mbili kwenye igizo hili; kwanza anacheza paka teja ambaye anaweza kuuza mtu yeyote kwa maziwa ya unga.

Vilevile anacheza silka ya Chorus ambayo anakuwa nafsi ya jangili Beak. Onyesho lake limesifiwa sana na wahakiki na sasa amefanikiwa kuingia mkataba wa kuigiza kwenye mchezo mpya wa Zip Postcode Wars ambao unaendeshwa na gwiji Ray Shell.

Alma ambaye ni mwigizaji wa kulipwa, alipata shahada yake ya sanaa na maigizo kutoka chuo maarufu cha Mountview Academy of Theatre and Art. Chuo hiki kinasifkia kwa kutoa waigizaji maarufu wa kimataifa kama Amanda Holden,Nick Moran, Ayub Khan Din mwandishi wa mchezo na sinema ya East is East and director Edward Hall.

Da'Eno pia ameshawahi kucheza kwenye kipindi cha televisheni ITV hapa Uingereza kiitwacho Collision. Vilevile yuko kwenye filamu ya British Art iitwayo Boggie Woogie. Maneno ya Critics chini Freeman and Ken have once again dipped into the absurd with their new production Beak Street - a dark comedy of noir shadows, mean streets and gangster cats, where only one thing is really certain:cats , they aint known for their loyalty A testament to freeman's faith in his imagination and ours' ( Time Out Critcs' Choice ****) This is a fine and powerful play that pulls no punches' (Chiswick Times) Iron-rod narrative and polished script.. imaginative staging.. alll makes Beak Street excellent value for money' Extraextra.com Baraka URBAN PULSE





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    go Alma go! hivi huyu ndo mama yake anaitwa Farida Mtengeti?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2010

    Naona Alma umekamata fegi na cider! Njoo Bongo uwape darasa kina Kanumba.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2010

    Hongera sista,kp on representing,mdau mwanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...