Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes usiku wa kuamkia leo imefungwa bao 1-0 na wenzao wa Ivory Coast kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny katika kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika Libya mwakani. Iwapo Ngorongoro itashinda kwenye mchezo wa marudiano itakutana na mshindi kati ya Gambia na Sierra Leone ambapo itaanzia tena ugenini mwezi Septemba na kumalizia nyumbani Oktoba mwaka huu. Pichani ndilo goli lenyewe....
Mdau Sammy-Kr

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2010

    Sio mbaya wadogo zangu mmejitahidi, ila tufanye juhudi nyumbani tushinde maana tumebakiza hatua chache tu...Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2010

    gud n bravo wana,najua tz hawatoki hao,mkirud mkaze makalio kwa tz mwanzo mwisho,home tunawanyuka hao,goli noja co ktu na inaonekana hawakutushika maskio hao,poa tz mbele tu mpaka mwisho!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2010

    Sio mbaya madogo...bravo. Huo ni ushindi mwembamba sana kwao ukizingatia walikuwa nyumbani. Kwetu sisi bao moja ugenini linaweza kutubeba endapo hatutabweteka na hayo matokeo. Muhimu tukaze buti kweli...waalimu naamini wameona wapi tulikosea na watarekebisha ili huku tuwapige 3-0. TFF fanyeni kila liwezekananlo maandalizi yawe mazuri...wakati ni huu, tuutumie ili tusije juta baada ya mechi. Najiona nikishangilia timu yetu ikiwa Libya hapo mwakani kwenye mashindano....Tanzania kuwa kama Spain INAWEZEKANA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2010

    hawa madogo they can take us very far ni wazuri kinoma kufungwa goli moja tu na ivorycoast sio lelemama hata kidogo.BIG UP ngorongoro haina noma kazeni msuli

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2010

    Na twiga star wamekongoliwa 6-0 south. Yaan soka la bongo raha kweli kweli!!!

    Anyway, kazeni buti madogo!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2010

    hivi timu ya twiga stars wameshinda ngapi naomba mnipe matokeo maana ile ndo timu tunayoitegemea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...