Kiongozi wa shughuli za uchaguzi na msemaji wa NCCR-Mageuzi, Faustin Sungura (kulia) akimkabidhi fomu ya kinyang'anyiro cha kiti cha Uraisi Tanzania, bw. Hashim Rungwe. Aliyesimama kati ni bw.George Kahangwa, mkuu wa idara ya mafunzo na sera wa NCCR-Mageuzi.
Hashim Rungwe (61) ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha siasa cha National Convention and Construction Reform (NCCR-Mageuzi) jana Jummane, alijitokeza kuchukua fomu za kuwania kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho.
Rungwe aliyekuwa akijinadi kwa kauli mbiu ya ‘Mwanzo wenye nguvu’ amekuwa kada wa kwanza wa chama hicho kuchukua fomu hizo licha ya mchakato wa utoaji fomu kuanza tangu Juni 16 mwaka huu. Rungwe huyo ambaye ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho alichukua fomu hizo jana katika ofisi za makao makuu ya NCCR jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku tatu kabla ya kumalizika kwa mchakato wa uchukuaji wa fomu hizo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada kuchukua, Rungwe alisema anagombea Urais ili kulipatia Taifa siasa na uongozi safi kwa kuwa mambo hayo mawili ndio yanayokosekana katika Serikali iliyopo madarakani.
“Nikifanikiwa kupata ridhaa ya Chama na Watanzania, kwanza nitahakikisha tunaongeza mchakato wa kulipatia Taifa katiba mpya itakayotokana na Watanzania wenyewe, kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayojumuisha Watanzania walioko katika vyama vya mbalimbali vya siasa” alisema Rungwe
Alisisitiza kuwa atalijenga Taifa lenye uadilifu ili kutokomeza ufisadi, uzembe na ukosefu wa uzalendo, kusimamia maslahi ya wafanyakazi hasa kima cha chini cha mshahara kuwa 315,000, kuheshimu uhuru wa wananchi kuabudu kulingana na imani zao pamoja na kusimamia maamuzi ya mambo ya msingi ila yasifanywe kuwa jambo la mzaha.
“Pamoja na mambo mengine ninaamini kwamba nchi ikiwa na raia wengi makini, wenye elimu na ujuzi wa mambo mbalimbali wataifanya Serikali iwe makini sana katika utekelezaji wa kazi zake za kila siku jambo ambalo litaliletea taifa maendeleo ya hali ya juu chini ya mpango uitwao mwanzo wenye nguvu” alisema Rungwe
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha hicho unatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu ambao utampitisha mgombea Urais wa chama hicho ambacho kilipata asilimia 28 ya kura zote za urais katika uchaguzi Mkuu mwaka 1995. NCCR-Mageuzi hivi karibuni ilikimbiwa na Mwenyekiti wake kwa kwanza, Mabere Marando ambaye alijiunga CHADEMA.

Kila la kheri Mh. Rungwe.....Tupo pamoja katika kuleta mabadiliko nchini kwetu.
ReplyDelete"Mwanzo wenye nguvu" oyeeeee!!!!
haya basi tuseme ni democracy lakini mimi sioni sababu ya kila mtu kutaka kugombea urais hata kama chance yake ni zero. jamani watu waache kutupa pesa zao ovyo.
ReplyDeleteHuyu Mheshimiwa Rungwe ndio yule mwenye car dealership?
ReplyDelete(US Blogger)
mambo ya ruzuku hayo. Simamisha hata Friji ili mradi tu tupate ruzuku letu :)
ReplyDeleteKuna watu nazani wana ndoto za mchana !! sioni rasi hapo !! teh teh teh hahhaa bongo kweli kazi hipo!1
ReplyDeleteAnony wa 04:33am hahahah ahahaha!!
ReplyDeleteUS Blogger, Yes, huyu ndio yule mzee aliyefungua pazia la wazalendo kuuza magari nchini Tanzania. Ndio mtanzania pekee aliyekuwa na showroom ya kufa mtu miaka ya 90 wakati huo wahindi tu ndio wanauza magari. Pamoja na hayo yote, lazima tukubali kuwa hamna mpinzani yeyeto mwenye nafasi ya kushinda urais, kama bado sheria za uchaguzi zivyo zilivyo. Hata kama wapinzani wataungana bado kuna kazi ya kumtoa CCM...Maana jamaa ni wezi kinoma.
ReplyDeleteHIvi vyama vya upinzani viungane visimamishe mgombea mmoja, lkn kila mtu akijinadi kwa chama chake hawatafikia malengo milele na milele. CUF,CHADEMA,NCCR N.K unganeni bwana, la sivyo mtaishia kugawana kura.
ReplyDeleteila huu mfumo wenu wa sasa hauna tija
he is never sereous about anything related to promises....sasa itakuwaje uraisi!
ReplyDeleteHivi huyu si wakili mwenzetu? Au nimemfananisha?
ReplyDeleteNkyabo - Bongo
Huyu mzee ana pesa kama serikali ya mwinyi
ReplyDelete