KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Tanzanite ya Tanzanite One ya Mererani wilayani Simanjiro imejitosa kudhamini mashindano ya urembo ya Kanda ya Kaskazini yatakayofanyika Julia 16 katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya Naura mjini i Arusha.

Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Lusekelo Mwakalukwa alisema jana mjini Arusha kuwa kampuni hiyo imedhamini mashindano hayo kutokana na kutambua umuhimu wa fani ya urembo nchini.

“Warembo watakaoshiriki mashindano ya kanda ya kaskazini wanatoka mikoa ambayo kampuni hiyo inafanya shughuli zake hivyo ni nafasi nzuri ya kushiriki shughuli za kijamii kwa kudhamini mashindano hayo”alisema.

Alisema kampuni hiyo imtoa udhamini huo kama sehemu ya mchango wake wa kushiriki kwa karibu katika shughuli za kijamii na pia kutangaza madini ya Tanzanite kwa watu wa kada mbalimbali nchini na duniani kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Crown Entertainment inayoaandaa mashindano hayo Erasto Jones alisema mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Naura Springs ambayo nayo ni moja wa wadhamni.

“Kwanza tunaishukuru TanzaniteOne kwa udhamini wao ambao utasadia sana kuboresha mashindano ya mwaka huu ambayo yatakuwa ya kiwango cha juu sana kutokana na maandalizi tuliyoyafanya”alisema.

Jones alisema mashindano hayo yatashirikisha warembo watatu kutoka mikoa minne ya Arusha,Kilimanjaro,Tanga na Manyara ambao wanatarajiwa kuweka kambi mjini Arusha kuanzia Juni 19 mwaka huu.

Aliwataja wadhamini wengine kuwa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom,Kampuni ya Bia kupitia kinywaji cha Redds,Naura Springs Hotel,,City Link Hotel,Redio Clouds, PSI na Artfull Photo Graphic
.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...