ankal akiwa Mandela Square kitongoji cha Sandton katika vekesheni
yake ambapo leo anajiunga na wadau duniani kote kusherehekea siku ya Mandela day
usiku wa kuamkia leo ankal anapata lanchi ya
usiku na wadau katika mgahawa wa MOYO
kama bongo vile. kabla ya nguna unanawishwa... ankal na wadau mgahawa wa MOYO na msanii anayetumbuiza mgahawani MOYO. hapo anakung'uta mpini huku akiimba na sauti inasikika kila mahali. angalia video hapo chini
moyo oye!







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    Hiyo hotel dress code ni hayo makoti? naona kila mmoja analo au yaligawanywa bure.....Huwezi jua ukarimu wa wenzetu mtu asije akafa na baridi shukua coat mwa mwa!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    Ankal najua hii hutoibania sababu itakupendeza ,ebu tuambie nasikia wewe ni mmoja wa watakaoingia kwenye jumba la Big Brother mwaka huu ? maana yake nimeshtukia hivyo vijackets mlivyovaa. pia Michu acha ukiritimba wa kubania comments ikiwa wewe kama mmoja wa wana habari na wana habari siku zote kauli mbiu yenu freedom speech (uhuru wa kujieleza)ebu wacha wana blog ya jamii kama unavyoiita wawe wakitoa mawazo yao. kama utaibania na hii basi ushindwe na uregee uwe kama bamia .
    mdau UK

    ReplyDelete
  3. YANGA BOMBAJuly 17, 2010

    we muhidin ina maana kesho uchaguzi wa yanga pale PTA hall sabasaba ground hutashiriki?siku hiyo yanga yako unaifanyiaga wapi wewe kijana?rubi upige kura kuwachagua viongozi wako wewe ebo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2010

    sijaona kafulana mara hii mana ata kule ukerewe ulikwenda nacho??? sembuse huko

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2010

    kaka najua bado upo vikesheni !! hila wadau tunaomba kama unaweza ku post humu lyrics ya nyimbo
    Kidumu & Jay Dee - Nitafanya


    thanks

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2010

    Mbona kila veksheni upo peke yako? maiwaifu wako yuko wapi? au hataki na yeye ale bata kama wewe? au hao wanakualika wanakupa ofa wewe bila kujali maiwaifi wako?

    Hii message tafahali itoe hata kama nimekuudhi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2010

    Hongera kaka michuzi.Mimi niko Ireland.
    Aisee umenishtua kumwona jamaa yangu tuliopotena nae miaka kibao nimemtafuta bila mafanikio.
    Ni huyo uliopiga naye picha mkiwa wawili, picha ya pili kabisa hapo juu tafadhali. Nakuomba uniunganishe naye kwa njia yoyote ile kwani nimemtafuta sana naona kama ndoto kumwona hapa. Mpatie email yangu tafadhali:
    joo2@hotmail.co.uk
    Please nitashukuru mara milioni kwa msaada wako.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 17, 2010

    mdau unayetaka wimbo wa kidum na jaydee ingia kwenye bongecelebrity kwa chini wameweka zote

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2010

    we Michuzi wewe ?? !!!!!!
    ni baridi kiasi hicho cha kuvaa gulovuz ????
    mwe, jamani mimi sikubali kama kuna baridi mpaka uvae hivyo lol
    uje huku tuliko ndiyo uone baridi, wacha mchezo bwana !!!!!!!!!!!


    Asante kaka

    mdau
    Toronto, Canada

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2010

    NaOna Ankali leo ZeFulana haikuweza kumudu kiWinta cha hapo Sauzi , ikabidi Zefulana itulize ball Hotelini ......ahahhaaaa picha safi sana!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2010

    VEKESHENI! SI UTAAMBIE TU UMETUMWA NA DAILY NEWS UKAPIGE PICHA ZA MANDELA DAY MZEE!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2010

    Ankal,
    Mbona huwa huendi na shemeji yetu? Ni mara chache sana kama ulishawahi hata siku moja kwenda naye vakesheni. Je ndiyo mfumo dume? Kwamba hakuna kutembea na maiwaifu wako?
    Au unaenda kwenye jumba la big brother huko South ndiyo maana unaonekana ki-big brother vile!!

    ReplyDelete
  13. Katika Msafara wa Mamba, kenge pia huwemo msafarani. Tarehe 18 Julai ni siku ya kuzaliwa Mandela, lakini pia ni siku ya kuzaliwa kwa Blackmannen. Mambo hayo.

    Iliyobaki ni kuwashukuru wote watakaotupongeza katika siku yetu ya kuzaliwa.

    Umri wetu unatofautiana kama ilivyo ukubwa wa Mamba na Kenge. Lakini safari yetu ni ile ile poeni. Sisi tofauti hiyo haitupi shida.

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  14. na mimi nakuja kuoshwa mikono duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu,mume wa mtu asieoshwa mikono na mke wake siata ibiwa na wazulu?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 18, 2010

    Asalaam alaykhum wajina kula bata ndio matunda ya kazi yako. Mola akulinde na akupe maisha marefu yenye good time na baraka tele chapa kazi kama kawaida ndio siri ya mafanikio yako.

    wasalaam chef Issa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 18, 2010

    mdau wa Sat Jul 17, 06:59:00 PM, sawa tushajuwa kama uko canada! ushafurahi?

    Yaani wewe umeshafika s afika katika miezi ya june mpaka august? au ndio katika wale ambao hawakuwahi kufika popote zaidi ya walipo sasa? hata hivyo hujasoma somo la jiografia? au hata basi hutizami katika internet ukajua misimu ya s africa kabla ya kuja hapa na criticism ya utumbo mtupu?

    Kwa taarifa yako s afrika kwa sasa ni baridi sana hasa wakati wa usiku, pia kuna baadhi ya sehemu hata snow inaanguka.

    Hukuangalia world cup? kwa nini unadhani watu walikuwa na makoti? juha kalulu wewe!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 18, 2010

    tunajua south africa ni baridi lakini huyo mdau hajamaanisha kama hakuna baridi ila anamaanisha ni baridi mtoto nadhani na wewe ujafika canada ukajua ni baridi ya aina gani iliyoko huko elewe ni north pole huko its freezing cold sio hiyo baridi ya south africa ni mtoto

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 18, 2010

    wewe mkulima.. wa Sun Jul 18, 02:33:00 PM

    kwani huyo mdau hapa juu alivyo sema kuna ubaya gani?
    hata mimi niliwaza hivyo hivyo, wote tunajua S.Africa huwa kuna baridi lakini sidhani kama ni ya kuvaa glovuzi....
    watu wengine bwana jazba nyingiii
    muwe mnaelewa utani jamani.!!!!!

    huna lolote nenda mbele huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...