UCHELEWAJI WA PICHA NA SAUTI
KWENYE KING’AMUZI CHA STAR TIMES

Ankal, pole sana na libeneke la kuelimisha jamii kupitia blog yako safi na inayopendwa na wadau wote wapenda habari.

Naomba tafadhari unisaidie kuweka kwenye blog yako ili wadau wa kutazama TBC 1 na pengine wataalamu wenyewe wa TBC1 wakishirikiana na watalaamu wa STAR TIMES waweze kunisaidia tatizo hii ambalo nimeliona mimi kuhusiana na picha pamoja na sauti zinazorushwa kupitia kwenye king’amuzi cha STAR TIMES kuna tatizo la utofauti mkubwa sana wa uchelewaji wa picha pamoja na sauti ukilinganisha na zile zinazopokelewa moja kwa moja kupiti kwenye antenna za kawaida bila king’amuzi, je tatizo lake ni nini hasa?
na kama wana re-transimit kwa nini pawepo na uchelewaje wa zaidi ya dakika kama 1.5 kwa ufahamu wangu hawa waheshimiwa watakuwa wana pokea picha toka kwenye tramsmitter za TBC 1, Channel 10 na kuzi changanya (Mix) na kisha kuzirusha kwa kutumia technolojia ya kisasa yaani dijitali (digital tramsmission) na king’amuzi kina (de-Mux). '
Naomba wataalamu wahusika wanifahamishe kwa nini pawe na utofauti mkubwa kiasi hiki???
Mdau wa teknolojia
Mihay

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2010

    IN ADDITION TO ZAT..! MBONA CHANNELL 10 INFUNGUKA NA SAUTI YA KISS FM.YAAN PICHA CHANNEL 10 NA SAUTI NI KISS FM.
    PLEASE ASSIST !!

    NA MBONA BBC HAIFUNGIKI?? INONYESHA ALAMA YA $ TU,AS IF HAJALIPIWA..SISI VINGAMUZI SI TULIAPLIA ADA KILA MWEZI?? AU HAITOSHI KWA BBC??

    STARTIME TUPENI SOMO HAPA!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2010

    Mimi nakubaliana na mtoa wazo kwani performance ya Star Times hairidhishi kabisa kwani sauti na picha haviendani au wako kwenye majaribio? Inakuwaje picha zinakatikakatika? Tunaomba kwanza watupatie contact zao tuweze kuwasiliana nao moja kwa moja.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2010

    That is the value of your money! Ingawa ukweli huu unauma. Njoo huku DSTV uone mambo! Always anything cheap is very expensive!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2010

    mdau ili kupata sauti ya chanel 10 bonyeza "track" kwenye rimoti yako

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2010

    mdau ili kupata sauti ya chanel 10 bonyeza "track" kwenye remote yako

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2010

    1.5 Mins delay ni kubwa sana, na sio kawaida. Lakini ni kawaida kwa mfumo wa digital transmission kuchelewa kidogo compared na analogue transmission, ndio maana inaonekana kama star times wanachelewa kidogo.

    Hii ni sawa na trasmission ya radio na ya tv analogue pia zinatofautiana, kwa mfano ukiwa unasikiliza mpira live kwenye radio, at the same time unaangalia kwenye tv (Analogue/Digital Transmission) utagundua radion inakuwa mbele kidogo kwa kama sekunde 15 hadi 20.

    Kwahiyo napenda kushare kuchelewa kwa star times ni kawaida, kutokana na jinsi waves za digital zinavyosafiri, lakini haitakiwi kuchelewa kwa zaidi ya dakika moja. That is unusual.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2010

    ............... msishangae jamani!....NI YA KICHINA. TEH TEH TEH, TBC BWANA.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2010

    Nimekubali kweli "bure ghali".
    Hoja iliyoletwa na mdau ni ya kweli.

    Pia unapobadilisha channel picha ya channel iliyokuwa inaonekana awali inaendelea kuganda kwa sekunde kadhaa kisha ndiyo unaona picha ya channel uliyo-tune.

    kingine ni kwamba wakati TBC na Star Times walipokuwa wanazipigia debe decorder zao walikuwa wakiahidi wateja kwamba kutakuwa na channel zinazoonyesha picha za ki-nigeria masaa 24 kama ilivyo kwenye DSTV (e.g. Africa Magic & Africa Magic Plus)lakini hadi hii leo hakuna kitu sana sana utapata picha kiduchu za ki-nigeria channel ya CITIZEN . Kama si TBC na mbia wao kutapeli watu ni nini?

    Mwisho najiuliza iweje kuwadhulumu wateja haki yao ya kuangalia fainali za kombe la dunia kwa zaidi ya dakika 20 kwa kuweka mambo ya CCM? Ikumbukwe kwamba wateja wengi walihamasika kununua decorder hizo kwa ajili ya kuangalia fainali hizo.Kuna dalili za utapeli. Kama sivyo TBC na mbia wenu trekebisha mambo (kasoro hizo) na ktekeleza ahadi ya kutuwekea channel za picha za ki-nigeria. Vinginevyo wateja watakubali hasara ya kukaa na makopo yenu waliyonunua (decorders) bila kulipia malipo ya kila mwezi na wengine kurudi DSTV.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2010

    Pia Hawa Jamaa walituuzia VING'AMUZI vyao sisi watu wa mkoani kama hapa Tanga, tena nikiwauliza mara mbili mbili huku vinakamata ? Wakajibu ndiyo lakini mpaka sasa wapi ...hakuna kitu.
    Ila inavyoonekana hawa jamaa wana asili ya mambo kama ya kichina hivi....!!! Hovyoo kabisa.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 14, 2010

    Tatizo la kuchelewa kwa sauti lipo hata kwenye satellite pia. Kwa wale wanaotumia dish la FTA (Free to Air) watakubalian na mimi kuwa channel nyingine kama ITV, EATV, STAR TV, CH 10, TVM, MBC2, MBC3, TV ZIMBO, RTS na nyinginezo, sauti iko 'in-sync' na picha isipokuwa TBC1, probably tatizo linaanzia ndani ya TBC wenyewe wala siyo kwenye teknolojia

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 14, 2010

    Star Times Mlituahidi picha za ki-Nigeria ziko wapi???? wizi mtupu

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 14, 2010

    He! yaani ni kama umefungulia redio mbili kwa mpigo zote una-'tune' station moja, ila redio moja inapokea mawimbi ya FM na nyingine shortwave, utaona redio moja inawahi kutoa sauti ya matangazo kabla ya nyingine.
    Du, makubwa haya.
    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 14, 2010

    Basi tuwape nafasi TBC na StarTimes wajibu hoja badala ya kuwaponda kupita kiasi, kwa kweli wameanza vizuri. Baadhi ya watu wasio na uwezo wa kumudu gharama za Decoder na Madish wamefaidika. Hauwezi kupata kila kitu kwa gharama ile. Ni mwanzo mzuri, tutegemee mazuri mengi toka kwao.

    Mdau Dar.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 14, 2010

    ......aiseeeh! yaaani leo nilikua naenda kulipia, ahsante mdau kunishtua........wakirekebisha tujulishane!

    Mume mwenza.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 14, 2010

    Star times wanazingua sana mi mwenyewe mwanzoni king'amuzi kilikuwa kinaonesha channel chache kama 23 hivi nilipowapa taarifa fundi alikuja akarekebisha nikaanza kupata zote ila zinasumbua sana JANA walisema muda wa usiku watafanya marekebisho asubuhi ya leo OH MY GOD channel zimejichanganya ukiweka BBC inakuonesha BET ukiweka TBC 2 unaona PHOENIX hata kama mwanzo ni mgumu wajitahidi kuboresha bei yao ni cheap likini sio sababu ya kuvuranda wakiharibu mwanzoni watazidiwa na kampuni kama DSTV MI MPAKA NAWAKUMBUKA GTV KWANI WALIKUWA POA SANA CHANNEL nzuuri mfano G-AFRICA MOVIE ZA KINAIJERIA NZURI KULIKO HATA ZA AFRICA MAGIC,vitu kama HEROES na vingine vingi STAR MEDIA NAJUA MNAONA MAONI YETU HEBU BORESHENI

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 14, 2010

    aisee hiyo ya dk 1.5 kiboko haiwezekani kuwe na delay ya namna hiyo.kuchelewa ni kwa sekunde kidogo hiyo ni kutokana na conversion toka digital to analogue kwa kuwa TV yako ni analogue.kuhusu picha za kinaigeria kuanzia kesho 15/07/2009 zitaonekana hii amesema MR.Mwanda toka TBC

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 14, 2010

    THANKS WADAU.
    NIPO HOME HAPA NA-TRACK KINGAMUZI NAONA NAPATA PICHA NA SAUTI YA CHANNEL 10 FRESSSH!! DU NA BBC INAPATIKANA SASA..WERA WERAAAA !

    KWA SALIO LETU (LA SAWA NA VOCHA ZA JELO JELO) HII INATOSHA!!
    JAMANI TUSILAUMU SANA SALIO LETU HALITOSHI KUWA SAWA NA DSTV.

    THANKS WADAU, THANKS STARTIMES

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 14, 2010

    Bongo tambarare
    jana mlituonyesha picha za mji wa Dar mkasema "Dar panapendeza na kunaendelea" Kumbe kupendeza na kuendelea ni kwa wachache tu na kihivyo hivyo...Natumaini ile sehemu tulioonyeshwa jana haina hayo matatizo....

    ReplyDelete
  19. Duuk kweli Startimes wameniudhi sana kutuwekea politiki badala ya match. tena politiki yenyewe ilikua imesheheni POROJO tele.
    pia naungana na wadau kusema "synchronization" ya picha na sauti ni poor na delay ni kubwa sana. Ankal tafadhali hebu waanzishie libeneke tupate majibu

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 15, 2010

    Ni kweli kuna matatizo katika hivi ving'amuzi,labda tuwape muda wajipange sawasawa.Ila pia katika ofisi zao kuwe na mafundi wao ambao watakuwa wanazungukia wateja kusolve some problems na sio hadi mjteja abebe king'amuzi kupeleka ofisi zao kwa msaada, pale atakutestia itaonekana fresh lakini ukirudi home mambo yaleyale.Na kwa wale ambao channel10 inaingiliana Radio ya Magic/Kiss FM Wafanye yafuatayo:-
    Weka chanel 10,kisha bonyeza kitufe kilichoandikwa Truck katika remote yako ya Star Dstv utaona sauti ya radio itatoka na utaweza kuona na kusikia vizuri chanel 10.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 15, 2010

    Hawa jamaa wazushi sana..! Et Sinza haishiki vizuri mpaka uweke antenna ndefu, mbona wakati mnajitangaza hamkusema? Haya sasa ndio shida ya vya bure. Decoder lenu nalitupa.... no nalichoma moto.. Bora niwape pesa wasauzi wanaonipa channels za ukweli na uhakika! LONGOLONGO KIBAO BONGO HAKUNA TUWEZALO NI MANENO NA KUVAA KANGA SHWAIN

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 15, 2010

    Mkuu kunaking'amuzi cha Easy Television 10,000 kwa mwezi, kama unatafuta bei rahisi hicho kitakufaa nilipokuwa bongo nilitumia installation ni kama 100,000 u will never regret kuna chanel kama 48, though kama kumi lugha yake ilikuwa inanitatiza sio kingereza wala kiswahili lakini the rest was fine,DSTV SOMTIMES HAIKIDHI HAJA ZA MTANZANIA

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 15, 2010

    Du wadau nashukuru kwa kutufahmisha utumbo wao, maana tulikuwa tunataka kwenda kulipia, mwanangu bora tu kwenda DSTV kweli vya bure vinagharama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...