Hallo ankal,
Naomba unisaidie kupost hii
Natafuta nyumba ya kupanga,nahitaji chumba(kiwe na choo cha ndani) na sebule,ningependa viwe maeneo ya tabata au ilala.naomba pia mwenye nyumba akubali kupokea kodi ya miezi sita.
Natanguliza shukrani zangu za dhati
mawasiliano:
0756 313365

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2010

    Kwakeli kifo cha Prof. Mwaikusa binafsi kimenistua sana sikutegemea kwa nchi kama hii inayosifika duniani kwakuwa na amani na utulivu yakatokea mambo kama haya ya mauaji ya kinyama unaua familia nzima kuuwa baba na mtoto nikuangamiza familia kabisa. Ingekuwa ni nchi zenye vita za wenyewe kwa wenyewe nisingestuka sana maana nikawaida ya hao jirani zetu kuuna kila siku kwa tamaa za kijinga.Na hata mazingira ya kifo chake ni magumu kuyazungumzia nilazima Watanzania waamke sasa kwanini wale wanao tetea maslahi ya umma wa Watanzania wanakufa kiajabuajabu? Alianza Sokoine,Akafuata kolimba,Wakaenda kwa kombe,Wengine ni wakina Mbatia (Mb),Chacha wangwe (Mb),Amina Chifupa (MB),Balali,Prof.Chachage na wengine wengi tu ambao sijawataja kwa kweli vifo vyao vmeleta utata sana na watuhumiwa huwa hawakamatwi kabisa na hata wakikamatwa wanaachiliwa huru kama yule dereva aliye kuwa anamuendesha wangwe eeh yupo huru mtaani nini hiki Baba wataifa uko wapi Tanzania ya leo sio ile uliyo itoa mikononi mwa wakoloni ni mijibazazi tu ndio inayotunyonya na kutukandamiza maskini........Mungu Ibariki Tanzania na Mungu Ilaze roho ya marehemu mahala pema peponi na uwape faraja wafiwa...

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2010

    1 BEDROOMS, 1 MASTER (SELF CONTAINED), SITTING ROOM, FENCE, AT KINYEREZI NSSF. 200,000 PER MONTH, 6 MONTH ACCEPTABLE. IF INTERESTED RESPOND TO THIS BLOG WE WILL CONTACT YOU ON YOUR PHONE

    ReplyDelete
  3. michuzi usiiibanie comment zangu maana huwa sizioni sio fresh kabisa maana nina huzuni sana na nchi yetu Tanzania

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 14, 2010

    Tafuta madalali kaka na uonyeshwe hizo nyumba. Bongo bado hatujaendelea kihivyo! usikwepe madalali 4,000 kuona kwa saa 1, halafu kodi ya mwezi mmoja yao ukishapata chumba.

    Nenda tabata shule pale pembeni kuna madalali maskani kuna bendera ya simba na yanga panauzwa matunda au Bima opposite na magorofa ya masoko kwa pembeni.

    Nguru Mbichi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 14, 2010

    Samahani mdau wa Wed July14, 01:08:00PM!

    Ukisema Bongo hatujaendelea kihivyo sio kweli!!

    Bongo maana yake Tz nzima, sema Dar (na iwe baadhi ya maeneo ndio hao madalali wa vijiweni wanatumika)
    Na siku hizi hata mikoa mingine (mfn Arusha)wanapatikana Agency/madalali waliosajiliwa sio kama ilivyozoeleka madalali wa vijiweni.
    Pia ujumbe aliotoa muhusika hapo unafika mojakwamoja kwa wenye nyumba na madalali, na sio lzm atafute dalali tu, ambao hata awajasajiliwa na kodi awalipi.

    Hiki ni kikwazo kimojawapo waTz awatafaidika kuwepo kwenye EAC.

    Madalali amkeni, mtabaki nyuma mpk lini, fanyeni biashara zenu kitaalamu acheni mambo ya vijiweni,mtapigwa jua mpk lini wateja hao hata awajui mnapatikana wapi

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2010

    Acheni kuwavurugia watu mpango yao. Madalali watakupeleka usikotaka kwa kutaka pata mlo. Utaratibu aliotumia huyu ni wa kawaida kwa waungwana waliostaarabika, na kwa njia hiyo wenye nyumba zenye hadhi anayotaka atapata bila mikwara ya madalali.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2010

    Wewe unataka nyumba na choo ndani badala ya kusema nataka nyumba yenye maji? Choo ndani utakiweza bila maji? Ulizia kwanza kama nyumba ina maji ndo uanze kuweka masharti ya vyoo vya ndani.-Mdau, NYC, USa

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2010

    Tarehe Wed Jul 14, 05:05:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous ahhahhahah umeongea point lala kweli kabisa bila maji hicho choo cha ndani utakitumiaje??

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2010

    jamani uko bongo kama chumba ni 200,000 kwa mwezi kima cha chini cha mshahara ni Tsh ngapi ???

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 15, 2010

    kima cha chini cha mshahara muulize kong'ota na mbayuwayu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 15, 2010

    wnasema zaidi ya nusu ya watanzania wanaishi chini ya dolla moha ya kimarekani kwa siku sasa .200,000 tsh za rent wanazipataje kama si kuchochea ufisadi!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 15, 2010

    jamani mimi nataka kurudi bongo sasa naombeni ushauri kwa mshahara gani wa chini na weza kuishi bongo ??mi ni graduate .sitaki maswahi juu ya mwaswahi naomba jibu !!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 15, 2010

    Kweli msemo huu ni ws ukweli msafara wa mamba na kenge wapo mijusi.akianzisha mmoja kitu wote mnafatisha kama nyumbu.maoni ni kuhusu kifo cha profresa sasa nyie mnatuletea hadithi za nyumba vp? M mungu ailaze roho yake pema peponi m mungu ataeaone
    sha wote walio shiriki

    Yabinty

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...