Ibrahim Hassan Gobbos
Nawajua Mnanijua, Tulichokikosa
Na Tunacho Kihitajia Nakijua.
WAHAPA HAPA…

Baada ya kutafakari kwa kina, kuombwa na walio wengi na kuzungumza na wana-Kivukoni vijana na wazee. Nachukua fursa hii adhimu kuomba kuwa kiunganishi chao kama mgombea nafasi ya Udiwani kata ya Kivukoni kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM.
Nachukuwa fursa hii nikiwa na ari na kiu ya kuleta maendeleo na ubora katika upatikanaji wa huduma na ukuzaji uwezo wa vijana katika kuchangia maendeleo na kudumisha hali ya mwanakivukoni kiuchumi na kijamii.

Kwa kauli hii naomba idhini yenu na kila kura ya mwanakivukoni mwenye kiu na ari ya maendeleo ya kivukoni. Mapenzi yangu ni kuwa kiunganishi na mwakilishi wa kivukoni kuleta yale yanayo kubalika na wote.
Kimsingi Ibrahim Gobos ni Wahapa Hapa, Mwenzenu, Kijana wenu na mwenye kiu ya kuunganisha wote kivitendo kuiletea kivukoni hadhi na maendeleo inayostahili kuwa nayo na kuigwa kama mfano bora.

Ili kuwa mwakilisha na kuwatumikia lazima niwajue na kuwafamu na kutoa mchango wenye kina, kwa hili napenda kusema nina nia ya kweli nawatambua, nawafahamu na nina uwezo wa kuwa kiunganishi na muwakilishi wa kuleta ari mpya na kasi ya maendeleo inayohitajika na wanakivukoni.
Uwezo wangu utakuwa wenye manufaa pale penye ushirikiano na wote ili kuweza kuweka fikra zote ziwe zenye mlengo wa maendeleo kwa kushirikiana nao katika kusukuma mbele guruadumu la maendeleo ya kata yetu ya kivukoni.
SABABU ZA KUGOMBEA
1. Kuwajibika kama raia na mwana CCM kijana ili kutoa mchango wangu wa jumla na kuongeza safu ya vijana katika kuleta maendeleo.

2. Kuleta fursa sawa, bunifu na mpya za maendeleo kupitia uwakilishi wa vijana katika ngazi ya Udiwani katika Kata ya Kivukoni.

3. Kuwa kiungo na kiunganishi muhimu cha maendeleo ya wakazi kivukoni katika sekta zote muhimu.

Kwa kuona Changamoto na fursa zilizopo ndani ya Kata ya Kivukoni hazitumiki au hazitambuliki kwa miaka mingi, kwa hayo imekuwa ni sababu kubwa na msukumo wa dhati kwangu na kwa ridhaa yangu kuomba kuwa diwani wa kata hii ili kutumia kipaji, uwezo na elimu kuishirikisha jamii na wadau mbalimbali kuainisha fursa hizo ili kuondoa kero na kuleta maendeleo na chachu ya kuamsha uwezo na vipaji vya vijana walio wengi na kuwapatia fursa ya kuleta maendeleo na mabadiliko yenye maridhiano na hali halisi ya kivukoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    Way to go Ibrahim!! Lutengano!!Mzee Minga Product!! Wakilisha kata , baadaye tarafa, mjunbe wa NEC , Member of Parliament. Then who knows!! They say no one knows how far can one go until one reaches there!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2010

    who is hassan gobbos??

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2010

    WEWE UNAYEULIZA HASSAN GOBBOS UMEZALIWA JUZI, ALIKUWA MCHEZA MPIRA MASHUHURI SANA WA YANGA MIAKA YA 1960's HADI MWANZO 198's0 AU MWISHO WA 1970's KAMA SIKOSEI ALIKUWA AKICHEZEA YANGA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2010

    HASSAN GOBOS HE WAS A FOOTBALLER PLAYING FOR YANGA AND THE COUNTRY, HE WAS A FORMIDABLE PLAYER EVER PLAYED FOR OUR COUNTRY. PANGA PANGUWA AKOSEKANI KATIKA KIKOSI CHA YANGA NA TAIFA, ALIKUWA MZURI SANA ENZI HIZO ZA EAST AFRICA CHALLENGE, NAHISI ALICHEZA PIA MWISHO WA EAST AFRICA GOSSAGE ALIKUWA AMONG FIRST ELEVEN YA TAIFA KWA MFULULIZO ZAIDI YA MIAKA KUMI NA AKINA MOHAMED CHUMA TOKA BANDARI MTWARA, CHUMA ALIKUWA MKIMYA MTARATIBU NA MTU WA MUNGU SWALA TANO LAKINI ALIKUWA MAKINI KWA MPIRA NAMBA TATU YA TAIFA FOR 13 YEARS, AKINA MAULID DILUNGA AMBAYE ALISHAWAHI KUWA KAMA SIKOSEI KATIKA FIRST ELEVEN YA AFRICA

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2010

    HUMJUWI HASSAN GOBBOS? BASI NI MTOTO WA JUZI AU ULIKULIA KIJIJINI HATA RADIO HAIKUWEPO WAKATI ANASUKUMA NGOZI YA NG'OMBE ENZI HIZO, MIMI NILIKULIA PORINI LAKINI NILIKUWA NAMJUWA KUPITIA RADIO MBAO 177 ENZI HIZO ZA KLABU BINGWA TANZANIA NA TAIFA CUP UWANJA WA KARUME, WAKATI HUO UKIITWA UWANJA WA ILALA KABLA KARUME AJAFARIKI NI SIKU NYINGI YAPA 40 YEARS AGO LAKINI TOKA AACHE MPIRA PENGINE NI MIAKA 20 NA USHEE HIVI ILIYOPITA SINCE 60s HADI 70s HADI 80s MWANZONI KABISA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2010

    Hassan Gobbos ni mwanasoka (yaani mcheza mpira maarufu) aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Tanzania yaani Taifa Stars na klabu ya Young Africans almaaruf kwa jina la Yanga katika enzi za miaka ya sabini.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2010

    Eh, Ibra una kazi...

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2010

    Wahapa hapa ...maana yake nini? Huu ni ubaguzi mbaya sana unaotakiwa kukemewa na kila mtu.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2010

    Nenda Ibra, . Yes, you can! 'unless you spread your wings, you will never know how high you can fly'

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 18, 2010

    Hey nyie wazee wa humu msimkalie shingoni kijana wa watu. Hata mimi nilikua najiuliza huyo Hassani ni nani ...mjue kuna wanawake humu na kuna vijana pia sasa kueleweshana kwa upendo sio jambo baya..Mimi nikikwambia leo Justin beaver na wewe si utashangaa lakini sitakuona looser nitakuelewesha tu kuwa ni nani....


    Back to the topic. Mimi nilizania udiwani watu wanapewa tu kama vile ukuu wa wilaya na mikoa. Nikiwa mdogo diwani wa Arusha yule baba alikua pale forever...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...