Rais Msaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisikiliza maelezo ya matumizi ya trekta ya kusukuma kwa mkono alipotembelea banda la Kampuni ya The Land China Com linalojishughulisha na uuzaji wa Matrekta wakati alipotembelea Maonyesho ya 34 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, jana. Kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Issa Mohamed.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2010

    hivi serikali inafikiria nini kuhusu kumpa mzee ruksa heshima kwa kuvipa baadhi ya vitu jina lake,maana barabara tu ndo zina jina la mzee ruksa,au ndo ile ile design mpaka mtu afariki dunia ndo aanze kuitwa kama kwa nyerere,sidhani kama inasaidia maana mwenyewe hayuko tena,ni bora muvipe majina mtu akiwa hai,naye ajivunie nchi aloitumikia.

    ReplyDelete
  2. Afande Shekigenda(Mstaafu), Ruvu JKTJuly 07, 2010

    Huu "mustach" wa Mzee Ruksa unanimaliza sana. Nafurahia anavyoutunza kwa kuuchana kwa kutumia kitana kidooogo na kumpa haiba nzuri anapotabasamu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 07, 2010

    Mdau wa pili, ni kweli kuwa mzee Mwinyi anaonekana fresh kwa mtu wa miaka 85. Nakubaliana kuwa tumuenzi mzee huyu kwa kuwa (1) watanzania wengi wazawa wamejenga nyumba za kisasa wakati wake (2) ametutoa ushamba kwa kuruhusu watanzania tuwe na vitu vya "anasa" kama vile TV na friji
    (3) katika awamu yake magazeti, TV stations na redio binafsi zimeruhusiwa kwa mara ya kwanza tangu tupate uhuru (baadhi yao yakawa yanamkashifu lakini hakuyafungia) (4) wakati wake passport zikawa ni haki ya raia wote, tofauti na awamu ya kwanza ambapo mtu alikuwa lazima awe anakwenda safari ya kikazi, masomo au tiba ndipo apewe passport (5)alifuta sheria ya watu kutiwa kizuizini (preventive detention)bila mashtaka (6)katika miaka 10 ya utawala wake Tz ilijitosheleza kwa chakula miaka tisa! (ukiondoa 1993 ambapo ukame ulizikumba nchi zote za Afrika mashariki na kusini) (7)ailporuhusu watu kufanya biashara na kuivunja Shirika la Ugawaji wa-tz waliokuwa wakivaa magunia au kutembea uchi 1984-85, Kibondo, Kasulu, Dodoma vijijini, Mtwara vijijini, n.k. wakaanza tena kuvaa nguo (japo mitumba) (8)hata wale maadui zake waliokuwa wanamzulia uongo -baada ya kuendesha uchunguzi mkali 1995-96 - wamekiri kuwa mzee huyu na familia yake hawajachuma na wanaishi maisha simple; na ndiyo maana (9) kila aendako TZ watu wanampokea kwa furaha na kukumbuka miaka ya neema. May God almighty continue to bless Mzee Mwinyi. Amen. Paul Mollel.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...