Msanii Kidum wa Burundi. Chini ni wimbo husika

Kufuatia post katika globu dada ya Globu ya Jamii ya www.bongocelebrity.com ya jana (BOFYA HAPA) kuhusu kutoelewana kulikoibuka kuhusiana na wimbo 'Nitafanya' wa wanamuziki Kidum na Lady Jaydee na Producers wa wimbo huo Hermy B (original version) na RKay Kamanzi(second version),tumepokea maelezo kutoka kwa Kidum.Bila kuyahariri tunayaweka hapa chini;

Mimi ni Kidum .Nataka kutoa maelezo kikamilifu kuhusiyana na iyi muzozo wa uyu wimbo wangu na Lady Jaydee .Hakuna shida yeyote yipo kati yangu na Hermy B ambayo ni producer wa round ya kwanza ya recording ya uyu wimbo .

Kama vile munajuwa mimi naishi Nairobi na hapa ndipo nafanya shuhuli za muziki wangu kwa muda mrefu .Sasa kama kwa mfano nime rekodi Dar es salaam alafu nisikiye kuna hitirafu kidogo kwa wimbo ni ngumu niwe nachukuwa ndege kila mara nikikuja Dar es salaam ingawa napapenda sana wakati hapa Nairobi piya kuna studios .

Kwa mfano version ya kwanza Key ile tuliimbiya mimi na jaydee ni yenye ambao ilikuwa chini sana kuweza kuwa rahisi kwa mwana dada lakini tulipo rudiya sasa mwana Dada sauti yake ikatoka kama ya malaika .Hapakuwa ubaya wakurudiya ku rekodi tena uyu wimbo sababu mimi mwenyewe niko msanii na kuna kile kitu mimi natafuta kwa hali ya ubora zaidi kama sikipati bila shaka ata ku rekodi mara ya tatu siwezi kusita kufanya . Wimbo ni wangu mimi na lady jaydee sisi wenyewe tukielewana na tu amuwe kuwurudiya sioni kama kuna ubaya .

Hata Hermy B mwenyewe na amini munamusemeya uwongo ya kwamba anamatatizo kuhusiyana uyu wimbo sababu mimi mwenyewe naelewa vema kwenye radio stations nyingi wanacheza version yake ya Audio . bado ni uyo wimbo tu iwe video ama audio .Na pia bado ni Kidum na Lady Jaydee iwe ni video ama ni Audio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 17, 2010

    this guy know what is doing !! keep it up men ! am ur big fun !love ur voice !! wasanii wabongo wainge mfano wako. wasanii wa bongo huwa awajuhi kuwas serious na kazi zao wanaa endekeza njaa tu mbele awatazami mbele!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2010

    NIMESILIZA ZOTE MBILI KWA UPANDE WANGU NIMEIPENDA YA VIDEO NAONA SAUTI ZAO ZIMETULIA ZAIDI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2010

    Nashindwa kuelewa nani mwenye licence ya huo wimbo, producer au mwimbaji??

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 17, 2010

    huyo producer lazima asisikie vibaya kwani kazi aliyo hifanya alivurunda !!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 17, 2010

    kama producer kalibwa analia lia nini tena the dude can do whatever he wants with the track !! ma producer wa tz wamezoea kuwalipulia wa sanii wa bongo kazi zao kwa sababu wasanii wa bongo awana pesa ya kurecord producer anajifanya ana mu offer kurecord free kumbe anakula hapo hapo!1

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 17, 2010

    Nimesikiliza huu mziki duuh huyu Kidum ni mara ya kwanza kumsikia na ana sauti kali sana. Jamaa is very talented.

    ReplyDelete
  7. Duh! hivi wabongo mtaona mbali lini?mimi nashangaa kwahii ishu ya huu wimbo kabisaa!!Kidumu mwenyewe ndo mwenye wimbo kama alivyosema hata akirudia tena kurekodi mala ya 3 au ya 4,5 hakuna shida yeyote,,kwani zooote hizo ataendelea kusikika yeye na kamanda Wambula Jidee,,Wabongo mumeshazoeea mambo yakubebana polisi,,huyu ni kidumu uraia wake nasikia ni mrundi/mkenya amekomaa kisanii ni balaa.Hata akienda burundi wale wauwaji wanatafuta kumuua nasikia duh!! big up Kidumu na Judhit wambula.

    ReplyDelete
  8. Kilichonifurahisha ni kiswahili chake tu.Oooh My God.Ha ha ha ha ha.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 17, 2010

    mi nimependa hilo singi tu alilolitoa Jide!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 17, 2010

    Huyu bwana kweli hata mimi namuamini sana kwa jinsi anavyojiamini kwenye kazi yake ya usanii,,kwasababu hapa bongo wasanii wengi hawajali kazi zao wao wanaweka mbele umaalufu tuu,,lakini jamaa anaangalia mbele sana kikazi hata mapato,,alivyoongea hawezi kusafili eti mpaka bongo kutokana na itlafu iliyomo kwenye mziki duh!!!hapo ni kweli kabisa.Tena hata mziki wake umetulia na unafurahisha,,na wewe mbigili unaongea eti kiswahili chake hujui kwamba kila lugha ni ngumu kama hujazaliwa ndani yake?Au hata wewe yawezekana una ukanumba flani!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 17, 2010

    big u brother ngoma tamu!zaidi ya malaika hiyo sauti.ule mto ulivyorusha jide keputeniii kazi anayo ahahah, nimesikiliza zaidi ya mara 20 lkn bado nataka kuendelea kusikilia hiyo combination ni noma sijaona bado

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 17, 2010

    kwa hili song sikosi mzalendo kamua jide tuko pamoja

    ReplyDelete
  13. Nyimbo nimeipenda sana haswa pale anauma kidole 'I SWEAR' ni miaka mingi sijaona mtu anafanya hivyo.

    ReplyDelete
  14. Nimemuelewa kidumu na ninakubaliana nacho kama producer wa kwanza alichemsha sehemu na hana uwezo wa kurekebisha kwani skills zake na vifaa vimeishia hapo ni lazima atafute sehemu nyingine watakayorekebisha, 2. Maproducer wa bongo tulieni mnapofanya kazi za wasanii lasivyo mtazidi kudharilishwa daily. Maan tutatengeneza na nyie na kuwapa watu wengine warekebishe makosa yenu, hapo itakuwa noma

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 18, 2010

    UMAKINI vs UBABAISHAJI. Hii si kitu ngeni kwa wajuzi wa mambo. Kilichotokea hapa ni Ubabaishaji wa Kibongo unagongana na Umakini wa Msanii anayejua anachofanya, na anyefahamu haki zake. So, hii ni mwendelezo tu wa utamaduni wetu wa kibongo wa kufanya mambo kibabaishaji,halafu kutaka kijulinda, badala ya kujifunza na kubadilika. Tuna matatizo makubwa ya utamaduni wa ubabaishaji. KEEP UP KIDUM!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...