Mteja wa simu za mkononi wa Vodacom Tanzania Erick Kabelege(kulia)akiangalia salio lake aliloingiza mara baada ya kupewa laini ya simu iliyosajiliwa na vocha mpya ya shilingi 300“JITI TATU”ya kampuni hiyo na mfanyakazi wa kampuni hiyo Sharifa Maggid(kushoto)Vocha hiyo imezinduliwa leo na kugawiwa bure maeneo mbalimbali jijini Dares salaam,katikati Emmanuel Mwasaga. Emmanuel Chipondwa mkazi wa manzese(kushoto)akimsikiliza kwa umakini mfanyaka zi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Adam Khamis alipokuwa akimpa maelekezo ya kutumia vocha mpya ya shilingi 300“JITI TATU”ya kampuni hiyo iliyozinduliwa leo na kugawiwa bure maeneo mbalimbali jijini Dares salaam.
Mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia)akimkwangulia Omary Abdallah wa pili kutoka kulia vocha mpya ya shilingi 300“JITI TATU iliyozinduliwa leo tayari kwa matumizi ya mawasiliano,kushoto ni mfanyakazi wa Vodacom Adam Khamis.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Omary Abdallah(kushoto)akimpa maelekezo Aisha shabani namna ya kutumia vocha mpya ya shilingi 300“JITI TATU”ya kampuni hiyo iliyozinduliwa leo na kugawiwa bure maeneo mbalimbali jijini Dares salaam.
Vodacom yazindua vocha ya shilingi 300.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imezindua vocha ya bei nafuu zaidi hapa nchini Jiti Tatu itakayouzwa kwa shilingi 300.

Wateja wa Vodacom wanaotumia huduma za simu za mtandao huo watanufaika na huduma hii ambayo itawawezesha kuongea kwa kiwango hicho cha fedha.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya, alisema kwamba huduma ni muhimu kwa Watanzania wengi kwani itawawezesha kuwasiliana kwa bei nafuu zaidi.

“Tutaendelea kuwaletea kuwaletea wateja wetu bora na kwa bei nafuu ili kuwawezesha kuwasiliana kwa urahisi” alisema na kuongeza kwamba Vocha hizo zitapatikana kila kona ya chini yetu.

Alibainisha kwamba uzinduzi wa vocha hizo utakwenda sanjari na zoezi litakaloendeshwa na wafanyakazi wa Vodacom la kupita maeneo mbalimbali na kuwagawia wateja wa Vodacom Vocha hizo

Aliyataja baadhi ya Tanzania watapita ni Tandika Sokoni, Kariakoo, Mbagala na vituo mbalimbali vya vya mabasi.

“Kutokana na uwekezaji wetu katika huduma hii unaokwenda sanjari na ubora wa mtandao wetu, wateja wetu wataendelea kuunganishwa na kuboreshewa huduma zatu za mawasiliano” alisema na kuongeza kwamba Vodacom itaendelea kutoa huduma zake kwa bei nafuu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2010

    huu ndio ushahidi halisi wa maisha bora kwa kila Mtanzania.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2010

    michuzi naomba jiti.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2010

    Asante Vodacom kwa kutufikiria...sasa line yangu naiamsha!

    mdau wa
    millioni 10

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...