Sekretarieti ya uchaguzi ikiwa makini kurekodi majina ya wagombea katika nafasi mbalimbali.Kutoka kulia ni Mzee Mayanga,Mdau Alistide Kwizela na Agnes Kimwaga wa BASATA.Mshindi wa Nafasi ya urais wa shirikisho la filamu,Bw.Simon Mwakifwamba akiwashawishi wajumbe kumchagua.Mwakifamba alichaguliwa kwa kura zote za ndiyo 24 kutokana na kuwa mgombea pekee aliyependekezwa na vyama vyote wanachama.Dawati Kuu la usimamizi wa uchaguzi wa Shirikihso la Filamu likiteta jambo muda mfupi kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza.Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego,Msimamizi wa Uchaguzi Kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo,Michael Kagondera na Mlezi wa mashirikisho,Mzee Rashidi Masimbi.

Wajumbe wote wa Mkutano ulioshiriki kwenye uchaguzi wa shirikisho hilo na wadau kwa ujumla wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi.


===== ==== ==== ===

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hatimaye leo limekamilisha rasmi mkakati wa kuyapa nguvu mashirikisho manne ya sanaa nchini kwa shirikisho la sanaa jongefu (filamu) kupata viongozi wake wa muda.

Awali, siku tatu zilizopita mashirikisho ya sanaa za ufundi,muziki na maonyesho yalipata viongozi wake wa muda na leo ilikuwa ni zamu ya shirikisho la sanaa jongefu (filamu) ambalo linaundwa na vyama kama cha Maigizo,Umoja wa Watengenezaji Filamu,Umoja wa Wahariri wa Filamu,Chama cha Watunzi wa Filamu,Chama Cha Wasambazaji Filamu,Umoja wa Waongozaji Filamu (Directors),Umoja wa Wachaguzi wa Mandhari (Location) nk.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA na kusimamiwa na Bw.Michael Kagondera Kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo,Bw.Simon Mwakifwamba Kutoka chama cha waongozaji filamu alichaguliwa kwa kura zote 24 kuwa rais wa kwanza wa shirikihso hilo baada ya awali kupendekezwa na vyama vyote kuwa mgombea pekee.

Hali ilikuwa hivyo pia kwenye nafasi ya makamu wa rais ambapo, Richard Ndunguru Kutoka Chama Cha Watunzi wa Filamu alipendekezwa kuwa mgombea pekee kwenye nafasi hiyo na kuthibitishwa kwa kura zote.

Nafasi ya Katibu Mtendaji ilikwenda kwa Wilson Makubi Kutoka Chama Cha Wahariri wa Filamu ambaye alipata kura zote 24 na kumbwaga vibaya mpinzani wake Hussein Darweshi Kutoka Chama cha Wasambazaji wa Filamu.Nafasi za ujumbe zilikwenda kwa Rahim Mtangi,Makame Bajomba,Denis Swea na Khadija Nyambasi.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi,Rais wa shirikisho hilo,Bw.Mwakifwamba alisema kwamba,masuala makubwa atakayoyafanyia kazi ni pamoja na uboreshaji wa mapato ya wasanii wa filamu kupitia kazi zao, uboreshaji wa kazi zao na uimarishaji wa umoja na mshikamano wa wasanii.

Mlezi wa mashirikihso ya wasanii,Mzee Rashidi Masimbi alisema kwamba, viongozi wa shirikihso wana kazi ya kuandaa kanuni kulingana na katiba,kusaka ofisi, kuongeza wanachama, kutanua mtandao wa shirikisho, kutafuta fedha, kupanga mkakati kazi wa muda mfupi na mrefu kwa ajili ya kulinawilisha shirikisho.

Kwa upande wake,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisisitiza kwamba, mashirikisho ya wasanii yanaundwa mahsusi kwa ajili ya kujenga umoja wa wasanii, kutanua ushirika wa wasanii nchini na kuwafanya kuwa na kauli pia msimamo thabiti pale linapokuja suala la wao kutetea maslahi na kusimamia haki zao.

Moja ya matatizo makubwa ya wasanii ni wao kutokuwa na umoja hivyo kushindwa kutetea maslahi yao ikiwa ni pamoja na kupanga viwango vya malipo na vipato.BASATA linaamini kwamba, chini ya mashirikisho inategemewa kwamba, viongozi watakuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wasanii lakini hasa ni mwanzo wa wasanii kujisimamia na kuwa na nguvu katika masuala yote yanayowahusu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...