Kwa orodha ya wataogombea ubunge na
uwakilishi kwa tiketi ya chama hiki katika uchaguzi mkuu ujao:
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hiki chama kina tatizo la wazi kabisa. Kimelalia Zenji na ishu fulani fulani huku Bongo. Tanzania haiwezi kujengwa na chama chenye sura hii. Hiyo siyo Tanzania tuliyoijenga na Nyerere.
ReplyDeleteNi lini wapinzania huaanza kufikiria kusimamisha mgombea kwenye jimbo? Ukipitia orodha hiyo unaona chama Cha CUF hakijafikisha hata robo ya wagombea katika majimbo ya Tanzania bara, sasa miaka yote karibu 20 ya uwepo wake kilikuwa kinafanya nini? Nadhani vyama vya upinzani vinahitaji mtazamo mpya wa namna vinavyohusiana na wapiga kura na watu vinavyotaka kuwaongoza.
ReplyDeleteTatizo la hiki chama ni moja kuna lugha fulan ambazo mimi huwa sizikubali wanazipenda sana utakuta matawi yanaitwa mara COSSOVO,mara BAGHDAD mara HAMAS sasa yana maana gani kwetu?!!!! Hebu angalia hata hiyo kofia ya mkubwa ilichoandikwa reflection yake hasa ni nini. Kule kwetu Kondoa kuna waafuasi wengi sana wa chama hiki lakini leo nikienda nikamkuta babu yangu amevaa kofia imeandikwa wanaumeee!!! nitashangaa sana
ReplyDeleteNI CHA KILICHOSHINIKIZA UWEPO WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR KIKIDHANI WAKATI WOTE KITAKUWA CHAMBA NAMBA MBILI ZANZIBAR NA KUSHIRIKI KATIKA SERIKALI YA ZANZIBAR KWA MANTIKI HIYO NI CHAMA CHA WATU WAPENDA MADARAKA NA SIYO KUONGOZA WATU. TATIZO LA VURUGU LITARUDI TENA PALE KITAKAPOKUWA SI NAMBA MBILI NA CHAMA KINGINE KUWA NAMBA MBILI NA KUSHIRIKI KATIKA SERIKALI NACHO KUWA NJE YA SERIKALI KWANI KATIKA MABADILIKO HAYO YA KATIBA YAO YA KUUNDA SERIKALI YA MPITO BAADA YA UCHAGUZI HAIONYESHI KWAMBA VYAMA VINGINE VITASHIRIKI KATIKA SERIKALI YA UMOJA WA KIITAIFA NA HASA UKICHUKULIA NI CCM NA CUF NDO WALIKUWA WAKISHIRIKI KATIKA VIKAO VYA KILE WALICHOKIITA MGOGORO WA KI-SIASA ZANZIBAR. HILI JAMBO MBELENI LITALETA VURUGU ZAIDI KWA VILE ALIKUFIKIWA KISAYANSI ZAIDI NI JAZIBA TU IMETUMIKA. CHAMA KUTOKUWA NA WAGOMBEA WENGI WA UBUNGE TANZANIA BARA HIYO NI FIKA KABISA INAONDOWA UHALALI WAKE KUWANIA URAIS WA MUUNGANO KWA LIPUMBA SIONI ATASHINDAJE KAMA HAWA-FILE WABUNGE BARA MAJIMBO YOTE. NA TUTAENDELEA KULALAMIKA JUU YA CCM KUSHIKA HATAMU HADI TUFE KWA VILE SISI WENYEWE HATUNA AKILI ZA KUKITOWA MADARAKANI
ReplyDeleteNATOKA KIDOGO NJE YA MDA HII MNIWIE RADHI.
ReplyDeleteKUNA LUGHA ISIYO RASMI YA BLOG YETU YA JAMII TUNAIELEWA.
LAKINI PALE TUNAPOTUMIA KISWAHILI BASI UNCLE FANYA MAARIFA KIWE KISWAHILI FASAHA. MIFANO KATIKA PAGE YA LEO INAYONITIA KICHEFUCHEFU KATIKA LUGHA YETU YA KISWAHILI NI KAMA IFUATAVYO:
MAZIWA FEKI - NAANDIKA WALAKA BADALA YA WARAKA.
MISS TANZANIA - KUTEMBELEA KILIMANJARO NA ARUSHA KWA AJIRI YA... BADALA YA KWA AJILI.
TUNATEGEMEA KWENDA MBELE ZAIDI BADALA YA TUNATARAJIA. TEGEMEA NI DEPEND ON NA TARAJIA NI EXPECT.
VODACOM - KUFTARISHA BADALA YA KUFUTURISHA. FTARI NI JINA/NOUN NA FUTURU NI TENDO/VERB HIVYO NAUNI HAIWEZI KUNYAMBULIWA NA TENDO/VERB LINAPONYAMBULIWA NDIO TUNAPATA FUTURISHA.
ASANTE-MNYARUGUSU
Ijue historia ya zanzibar kabla ya kutoa maoni,cuf ni chama kilichoundwa baada ya wapemba kunyanyaswa miaka yoye tangu mapinduzi, na hii inatokana na sababu ya waarabu kuwa vinara wa biashara ya utumwa, hapakuwa na mtu mweusi aliyefanya biashara hiyo bali weusi waliletwa kutika tabora, kigoma na kwingine kwenye gulio walio baki ndiyo hao wanaojiita waunguja, hii imejenga chupi katika jamii hizi mbili, ndiyo maana hapajawahi kuwa na rahisi mpemba, lakini kupitia uelewa wa Abeid Amani Karume, kamaliza tatizo hili mwaka huu tutakuwa na rais na makamu wote wapemba hii itaifanya zanzibar kuwa na maendeleo makubwa sana kwani hawa jamaa sio mafisad hata siku moja ndiyo maana hawapo kwenye epa na richmond.
ReplyDeleteMdau Uk
mdau Uk naona hadi kiswahili umesahau, unasema chupi badala ya chuki anyway, typing error!
ReplyDeleteanyway,aliechangia kuhusu lugha isiyo ramsi amenifurahisha kwani hata mimi huwa najiuliza pia, watu wana tatizo gani kuchapia hata kiswahili, ajira mtu anasema ajila hatukusoma kiswahili shule ya msingi?
anyway, swala la CUF, mhh!! sidhani kama wanatufaa sababu mi ninavyoona wana udini zaidi, na mwisho wa udini ni kupigana.CCM ingeweza kufanya vizuri sana tatizo viongozi karibu wooote ni ma selfish, wanajali maslahi yao kuliko ya wapigakura.
nahisi upinzani kuchukua urais Tz bado ni ndoto, kwani hebu jiulize mf CUF wachukue urais, sijui wataanzia wapi ku take -over na kukaa sawa ili nchi iende, na huo udini wao,anyway!! yani kwa kifupi Tz mambo magumu, labda tusubiri atakaekuja baada ya JK.maana looooh!! tabu tupu!!
mariam - USA
Mariam USA Umenena.
ReplyDeleteHao wanaoponda CUF wasilalamike maisha magumu! mbona kila siku wanalia hatuna umeme,hatuna maji hatuna kazi na kufuatilia mafisadi wanaoiba mamilioni-ACHENI UPUMBAVU hawa CUF hata kama wana uchu wa madaraka YOU CAN NOT JUDGE THE BOOK BY COVER kumbukeni,wapeni nafasi kisha muwa hukumu na hiyo ndio demokrasia-waingereza wamewakandia CONSERVATIVE miaka mingapi sasa wamechagua hao hao kwa kuwa wanataka mabadiliko-KUMBUKENI WATANZANIA WA ZANZIBAR WAMECHOKA-KUNA SEHEMU MAJI HAYAJAWAHI KUTOKA TOKEA DUNIA IUMBWE HATA MTU UKIJENGA NYUMBA HUFANYI FITING YA MAJI-HII NI AIBU MAJI YALIYOJAA KISIWANI PALE.ANGALIENI MABADILIKO YA WAPINZANI NCHI ZINOJUA DEMOKRASIA-ANGALIA KIWANGO CHA ELIMU NA MAISHA CHA ZANZIBAR SEIF ALIPOKUA MADARAKANI KISHA JUDGE NA SASA HIVI.
ReplyDeleteWanawake hawana nafasi ktk Cuf.Habari ndo hiyo.
ReplyDelete