Kwa video hii (ya TBC1) na nyingine kibao BOFYA HAPA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Makame kimkabidhi Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe fomu za mgombea Urais wa Chama hicho leo mchana katika ofisi za tume jijini Dar. Nyuma ya Mh. Mbowe ni katibu mkuu wa CHADEMA ambaye atagombea Urais

Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa akitoka Tume ya Uchaguzi leo baada ya kuchukua fomu tayari kwa kuanza kinyang'anyiro hicho

DK.Wilbrod Slaa ambaye ni mgombea wa urais kupitia chama cha Chadema akipongezana na mgombea mwenza Hamis Mzee Hamisi baada ya kukabiziwa fomu na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame .katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Fremon Mbowe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. kufanya mikutano ya hadhara sio kuvunja sheria. Ila kuomba kura kama alivyokuwa anafanya Dr. Slaa ni kuvunja sheria ya uchaguzi.Mfano aliomba wafanyakazi wampe kura hata kabla ya kampeni.

    Kama mtu anaeomba kuingia ikulu, haheshimu sheria hata kabla ya kuingia ikulu je akingia itakuwaje? Tuweni makini na upigaji kura wetu Octoba 31.

    ReplyDelete
  2. Dear Tanzanian the TIME FOR CHANGE IS NOW, PLEASE LET THIS HAPPEN

    ReplyDelete
  3. MSEKWA,CRY BABY,WHAT A SHAME CCM ARE CRYING FAUL.THEY HAVE DONE SAME THING CHADEMA'S DOING RIGHT NOW.lol

    ReplyDelete
  4. Yaani huyu mbowe naye anagombania kupitia chama cha chadema au nimeelewa vibaya? mimi siamini macho yangu...Nilizania amehamia juzi juzi tu kuongeza joto ya chama kumbe alikua anataka kupitita huku....Nilizania ni Slaa tu...HUyu atawaharibia chadema angebakia huko huko sijui kwenye chama gani alikuwapo vile...

    ReplyDelete
  5. Duh huyu mgombea mwenza, yaani dalili ya kushindwa tu..

    ReplyDelete
  6. Mwenye kusikia na asikie na mwenye macho haambiwi tazama, ule muda mwafaka naona umefikia tamat, ni muda mwingi nimekua nikijiuliza tanzania kweli ina rushwa?, sikutaka kusema ndio kwani nilikuwa bado sijamaliza kutafuta jibu langu nililolipata siku chache zilizopita.. tumeweza kujionea rushwa imetawala sehem gan na nani wamekuwa chachu wa utoaji na upokeaji rushwa., swali kuu nililojiuliza na kufunga mjadala ulionisumbua ni kwamba "TULIWAHI KUYASIKIA HAYA TUNAYOYASIKIA TOKA VYAMA VYA UPINZANI"

    ReplyDelete
  7. Anon.10,06:46:AM kweli hujui ungesoma maelezo upya kwa makini na hayo masikitiko yako yataisha.Pole

    ReplyDelete
  8. Sasa na huyu mwenyekiti wa tume mbona kavaa jezi ya chadema au ndo tuseme anaipa shavu.gangamala kaka walete na wenzako

    ReplyDelete
  9. we mtoa maoni wa4 huo sasa ni uchechi kupindukia ina maana hujuagi mbowe yu upande upi..hahahaha

    ReplyDelete
  10. Tatizo hapa ni definition sahihi ya kampeni. Kama kusema kuomba kura ni kampeni je kukataa kura ni kampeni pia?

    Kama ni hivyo basi CCM wasilie faulo sasa hivi wakati ndio walionza kutaja issue za kura haswa pale waliposema hawaitaji kura za wafanyakazi wa Tanzania.

    ReplyDelete
  11. muda wote wanasiasa nia yao ni kushika hatamu za uongozi, hivyo basi harakati zao zote za kufanya mikutano ni kwa nia ya kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura ambao ndio wana uwezo wa kuweka chama cha siasa madarakani kwa kutumia kura zao.

    Hii ya kuunza kampeni kabla ya uchaguzi hakuna kwani baada ya uchaguzi tu kwisha wanasiasa wanaanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi mwingine.

    Msekwa anasema CHADEMA wameomba kura na kukashifu vyama vingine, je anasahau Kikwete na Makamba walisema nini pale Lumumba siku ile JK alipochukua form za kugombea urais?


    Toa kwanza boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kitanzi kwenye jicho la mwenzako.

    ReplyDelete
  12. DUU!! CCM SAFARI HII WANALIA FAULU?
    MATUMBO MOTO.

    ReplyDelete
  13. MKUKI KWA NGURUWE

    ReplyDelete
  14. MSEKWA PAMOJA NA UZOEFU WOTE HUO UNADHANI CCM WAO HAWAJAFANYA MIKUTANO YA KAMPENI MPAKA SASA HIVI. KJ MWENYEWE ALISEMA BAADA YA KUCHUKUA FORM KWAMBA KUANZIA SASA NI KUFANYA KAMPENI ZA NGUVU, NA AKASEMA VIONGOZI WA TAIFA WAMEJIPANGA VYEMA NA KUHIMIZA WATU KUFANYA KAMPENI NYUMBA KWA NYUMBA HADI KITANDA KWA KITANDA, JE HAYO HAYAKUWA MANENO YA KAMPENI?

    ReplyDelete
  15. Mzee msekwa haupo tena kwenye enzi za chama kimoja cha siasa, hivyo ni lazima ukubali changomoto unazokabiliana nazo toka kwa wapinzani,kumbuka enzi za ukiritimba ilishayeyuka,ninaweza kusema CCM ndio waliokuwa wa kwanza kuanza kampeni pale Dodoma walipowakusanya TOT, vanafunzi wa chuo kikuu, waigizaji, wanamuziki wa kizazi kipya na wenyeviti wa CCM waliofungua matawi CCM nje ya nchi, pia walikuwemo wawakilishi vyama mbalimbali toka vyama mbali mbali kote duniani. Mambo yalitokea yalirushwa live na TBC kwenye mtandao wa internet ambapo mimi nilibahatika kuyaona live kwenye laptop yangu hapa ughaibuni.

    Ninakuu maneno au ujumbe ambao wanafunzi wa chuo kikuu waliimba kwenye wimbo wao, walikuwa wakesama Kikwete atawagalagaza upinzani, je huu haukuwa mwanzo wa kampeni kwa wanaCCM? si haya tu kulikuwa na mambo mengi kadha wa kadha ambayo yalikuwa na kila dalili za kuanza kampeni pale Dodoma.Je mbona vyama vya upinzani havikulalamika?

    ReplyDelete
  16. CHADEMA kabla ya kuingia IKULU kimeanza kuvunja taratibu zake yenyewe.Taratibu zao zinasema mgombea lazima athibitishwe na vikao ndiye aende kuchukua fomu mbona Slaa ajathibitishwa.Tena Mbowe anasema atadhibitishwa baadaye.Swali Je hicho kikao hakina uwezo wa kumkataa?Kama kina uwezo wa kumkataa na kikamkataa itakuwaje na yeye ameshachukua fomu?Hichi ni chama cha demokrasia kweli au cha kidikteta ?Jamani angalieni hawa watu msije kuja juta.

    ReplyDelete
  17. kitu kimoja tu mimi nadhani naweza kuwapongeza chadema ni kutokuwa na mgombea specialist wa urais kama cuf. yaani wao kwa muda wa miaka 15 sasa unasikia lipumba anagombea urais wa muungano na maalim seif anagombea zanzibar. hivi mtu ukishindwa mara mora, tena vibaya kama vile alivyoshindwa lipumba safari zote si basi tena uwaachie wenzio? nimefurahi kwamba wao chadema, mbowe aligombea safari iliyopita na sasa kamuachia dk. slaa. huo ndio ukomavu wa demokrasia, ingawa najua safari yao ya kushinda uchaguzi bado ndefu.

    ReplyDelete
  18. sikutegemea kama CCM mtakuwa dhaifu kiasi hicho, kumbe mnamuogopa Dk. Slaa eeh! nyie mlivyoanza mbwembwe za uchaguzi mapema hamkujua kuwa kuna simba mwingine anasubiri kuunguruma baadae? yaani mliyofanya nyie mliona sawa tu kwamba Kikwete hana mpinzani, sasa kaibuka mnaanza kutapatapa. mnadhani wananchi hatukusikia mliyokuwa mnayasema hadharani kuponda upinzani? mnaogopa nini sasa wenzenu wakifungua vinywa kusema? CCM WAOGA LOH! NA MWAKA HUU MTAULA WA CHUYA KWA UVIVU WA KUPEMBUA MANAKE KUCHAGUA MMESHINDWA!

    ReplyDelete
  19. Hivi ni mimi tu ndio masikio yangu yana taabu ama huyu mtangazaji wa TBC1 anatamka jina la Dr Slaa kama Dakta Klaa. Katika taarifa nzima nasikia jina la mgombea wa uraisi wa Chadema likitamkwa kama dakta Klaa. Hizi mbinu za kupotosha watu za TBC zitatupeleka pabaya. Halafu michuzi usibanie hoja yangu. Nawakilisha!

    ReplyDelete
  20. Slaa?? HAPANA. No mvuto. Lugha ni ubabe ukali hasira fitna na uzushi. MMMno nono

    ReplyDelete
  21. KILA CHAMA KINA UHURU WA KUFANYA MAMBO YAKE KWA JINSI KINAVYOONA INAFAA. KAMA KULIKUWA NA KOSA BASI TUME YA UCHAGUZI ISINGETOA HIZO FORMS.

    WALE WANAOSEMA HII NI DEMOKRASI GANI YA DR SLAA KUCHUKUWA FORM WAKATI HAJADHIBITISHWA NA MKUTANO MKUU, HAJULIUZE MBONA CCM ILITUMIA VITISHO NA KUKATAZA MTU YEYOTE HASICHUKUWE FORM KUTOA CHANGAMOTO KWA JK.

    WAHENGA WALISEMA MTI WENYE MATUNDA NDIYO UTUPEWA MAWE, MKUKI KWA NGURUWE PIA NYANI AONI KUNDULE

    ReplyDelete
  22. WEWE ULIULIZA KWA JE KIKAO CHA MKUTANO MKUU AKINA UWEZO WA MKATAA INAELEKEA HUJUI SIASA. WATAMKATAA VIPI MGOMBEA PEKEE ALIYEPENDEKEZWA NA KAMATI KUU YA CHAMA?

    WATAMKATAA KWA SABABU ZIPI? AU KWA SABABU AMEONYESHA KUIPA CHANGAMOTO CCM? NA WATAMKATAA HALAFU WAMCHAGUE NANI?

    JE CCM MBONA HAWAKUMKATAA KIKWETE DODOMA?

    ReplyDelete
  23. this time slaa na chadema kwa ujumla wamechemka!wangeongeza nguvu ya upinzani bungeni kwa kukomalia ubunge kwanza yaani ingewezekana hata mbowe angegombania ubunge.sasa wakishindwa uchaguzi october which is what is going to happen anyway ndiyo imetoka!

    ReplyDelete
  24. Ombama, siyo wewew tu hata mimi nimeshangaa sana huyo mtangazaji kusikia akitamka Klaa mwanzoni nilifikiri ni kakosea kumbe ndivyo ajuavyo Loh! matatizo ya kazi za kupeana kwa kujuana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...