Habari na picha na John Bukuku
Mchezaji wa Mpira wa kikapu nchini Marekani NBA anayechezea timu ya Memphis Grizzlies akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuanza kwa programu ya Basketball Clinic itakayoanza tarehe 12 Agosti kwenye viwanja vya Don Bosco jijini.

zaidi ya 400 wanatarajiwa kukutana kwenye clinic hiyo ambapo TBF kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Phares Magesa amesema wanatakiwa kujiandikisha katika shule zote zenye vilabu vya Basketball nchini kote.

Lakini pia Hasheem Thabeet ameeleza kwamba katika nchi za Afrika ameshafanya Basketball Clinic kama hizo katika nchi za Nigeria, Senegal, Ivory Coast pamoja na Tanzania kwa sasa, kwa nchi za Asia amefanya programu kama hiyo na mchezaji mwenzake Yao Ming kwa nchi za HongKong, Quatar na Taipei, kulia katika picha ni Makamu Mwenyekiti wa TBF Phares Magesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. We want to see you prosper in NBA, Hashim. You are young and can do all the politics later, at least after you have made your seat indispensable in NBA!

    ReplyDelete
  2. PIG UP HASHIM.......SAIDIA UMMA NAKUHAKIKISHIA UTAKUMBUKWA DAIMA NA NI AKIBA YAKO KWA MOLA. PIG UP SANA KWA HIYO PROJECT..KP IT UP..

    ReplyDelete
  3. Yaani tangu ligi iishe huyu alikuwa bado hajafanya kiliniki? sasa hivi alitakiwa awe anafanya mazoezi ya kuanza ligi, mtu mwenyewe alikuwa anastrago.

    Mjomba unatakiwa uwe na personal trainer ili ujiweke fiti ili uwe ucompete kwenye starting center!

    ReplyDelete
  4. Yaani huyu champion anapata his chache kuliko mimi US Blogger na John Mashaka.

    Kweli wabongo tunapenda domo.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. Yaleyalee... Kilimo kwanza wakati machungwa yanaoza Lushoto!! Watu watalima wakati soko la uhakika hakuna.. Kila siku Hasheem analalamika kuwa nchi haina viwanja vya Basketball. Sasa hizo kliniki atafanyia wapi? Yeye angesaidia kwanza tuwe na viwanja vya maana ndio aendeshe kliniki yake.
    Itakumbukwa kwenye mahojiano yake na Clouds alilalamika wachezaji wenzake hawezi kuwaomba kuja kwa kuwa TZ hakuna viwanja, sasa anachofanya yeye ni nini kuhusu viwanja? Bora hata angewachangisha kwanza hao wenzake tujenge viwanja.

    Mzozaji

    ReplyDelete
  6. Dogo anakula BATA kwa kwenda mbele!! hahahaha LOL

    mdau PAris
    AKA msoma nyota

    ReplyDelete
  7. Angalia, kusahaulika ni jambo dogo tu, angalia maraisi wastaafu kama mkapa, mwinyi na wangine walioshika nyadhifa tofauti, waling'ara siku zao baada ya kiti kuyoyoma kama wangekuwa wanajichanganya na kadamnasi wangepigwa kikumbo tu, sasa wewe inabidi ufanye ufanyavyo u-shine maana nguvu na bidii yako ndio silaha yako, politics huiwezi na kisomo chako hicho ndugu!!!

    ReplyDelete
  8. wapinzani hawakosekani na pengine ndo uliotufikisha hapa tulipo. tatizo wabongo tunajifanya mno tunajua mambo sasa kajitokeza huyu mwenzetu kutoa anachoweza, kelele nyiiiingi hatuwezi kwenda kokote namna hii tumwache jamaa afanye anayoweza kuyafanya kwani kuna watz wenzetu wangapi wenye mafungu ya kutosha na hakuna lolote wanalofanya???

    ReplyDelete
  9. twiluumba!!

    ReplyDelete
  10. Wachezaji wenzake nao huwa wanafanya kliniki za nmana hiyo mahali pengine duniani.

    Labda ni mojawapo ya majukumu ya kuendeleza mchezo huo popote duniani...kwa minajili ya kuwapata potential wachezaji wa kwenda kuchezea timu za Amerika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...