Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Tanganyika Law Society uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo chuo Kikuu cha Dodoma leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tanganyika Law Society katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma leo asubuhi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Tanganyika Law society(TLS) wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa TLS uliofanyika katika ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma leo asubuhi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete(watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Mkutano mkuu wa Tanganyika Law society mjini Dodoma leo.
(Picha kwa hisani ya Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. huu mkutano unahusu nini au hio tanganyika law society inajihusisha na nini?

    ReplyDelete
  2. @ mdau wa 11:24PM. Hiyo ni jumuiya ya wanasheria wa Tanzania

    ReplyDelete
  3. Mdau, BloomsburyAugust 14, 2010

    Na huyo aliyevaa red leather suit naye mwanasheria? Au James Brown?

    ReplyDelete
  4. mwenye suti nyekundu ni mbunge wa zamani aliyepata kuwa kwenye kundi ya G55 anaitwa Kuwayawaya Stephen Kuwayawaya. huyu bwana yeye huvaa mavazi ya rangi nyekundu every single day. sijui akienda mahakamani kama huwa anavaa nyeusi, i have to find out.

    ReplyDelete
  5. Naona wahudhuriaji ni wachache maana wanasheria wengine wameona hamna maana yakufanya haya mambo wakati wa uchaguzi huu ujanja wengi wameshauelewa.

    ReplyDelete
  6. mdau wa tatu hapo juu mbavu zangu ha ha haaa, ati au james brown, ila suti nyekundu mh!

    ReplyDelete
  7. Wanasheria muende na wakati. Badilisheni "Tanganyika". sasa tuko "Tanzania". Halafu muwe critical na matatizo makubwa ya Tanzania hasa corruption, poverty na nepotism (inajumuisha ukabila, udini, na vyeo kwenda familia moja). Kuendelea kuita chama chenu "Tanganyika" inaonesha mlivyopitwa na wakati. Wacheni kusikiliza hotuba za wanasiasa na kupiga makofi tu... na kusubiri labda siku mtapewa vyeo vya kuteuliwa...

    ReplyDelete
  8. Inaitwa Tanganyika ikiwa na maana kwamba Zanzibar nao wana jumuiya yao. Ila kwa sasa kuna mabadiliko yatafanyika ili kuiita 'Tanzania Mainland....' badala ya 'Tanganyika...'


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  9. Let me very specific. Huu ni mkutano wa kila mwaka wa wanasheria wote ambao tayari ni mawakili (Advocates). Msio kwenye hii tasnia hamuwezi kujua. Mwaka huu mmejua kwa sababu umefunguliwa na rais. Society hii inafanya mambo mengi sana na ina voice kubwa mbele ya serikali. Mwaka huu wa uchaguzi, society hii ni moja wa wasimamizi wa ndani (independent election monitors).Kuhusu jina Tanganyika litabadilika kuwa Tanzania Mainland kuanzia January next year wakati sheria iliyoanzisha hii association itakapo fanyiwa marekebisho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...