Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia John Mc Intyre(watatu kulia),Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa(kushoto) na Waziri wa TAMISEMI Mhe.Selina Kombani(kulia) wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi ujenzi wa Miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi zilkizofanyika Ferry kivukoni jijini Dar es Salaam leo mchana.
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka jjijini Dar es Salaam(Dar Rapid Transit Agency ) Bwana Cosmas Takule akieleza jinsi mradi huo utakavyofanya kazi pindi utakapo kamilika hivi karibuni jijini Dar es Salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaamm williuma Lukuvi wakisikiliza kwa makini.
Mtendaji Mkuu wa Mradi wa mabasi yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam Bwana Cosmas Takule akionyesha mchoro wa ramani ya utekelezaji wa mradi huo jiji Dar es salaam huku Rais Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Miundombinu Dr.Shukuru Kawambwa, Waziri wa TAMISEMI Bi.Selina Kombani na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya dunia Bwana John Mc Intyre wakisikilza kwa makini wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu ya mradi huo zilizofanyika Ferry Kivukoni, jijini Dar es Salaam leo mchana.

(Picha na Freddy Maro)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. niko nje ya mada kaka!je ni kweli kuwa jaji mkuu amenusurika ajali tabora?nimesikia tu sina hakika na najua bloguni humu ndo manakuwa na habari mapema!Mungu azidi kukulinda!

    ReplyDelete
  2. CHANGA LINGINE HILI.
    HIVI HAWA WANASIASA WANAJIONA WAO NI KAMA MIUNGU KWAMBA WENGINE HAWAWEZI KUTOA MAWAZO YENYE MAANA.

    KUTATUA TATIZO LA FOLENI JIJI LA DAR HALIITAJI ROCKET SCIENCE NI SWALA DOGO SANA TENA LISINGEWEZA KUIONGEZEA SERIKALI MZIGO MKUBWA WA KULIPA PESA NYINGI KWENYE FIDIA.

    ZILE BARABARA NDOGONDOGO ZA MITAANI ZIWEKENI RAMI NA ZILE ZILIZOJENGWA KWA MPANGO MAALUM WA KUZIPUNGUZIA MSONGAMANO BARABARA KUBWA ZIWEKWE RAMI KAMA MTAONA MSONGAMANO WA MAGARI BARABARANI.

    KILA MTU ANATAKA GARI LAKE LISIPITE KWENYE MAKORONGO LIPITE KWENYE RAMI BARABARA ZENYEWE ZENYE RAMI ZIKO NGAPI.

    WEKA RAMI ILE BARABARA YA BUGURUNI INAYOTOKEA VINGUNGUTI, YA TABATA INAYOTOKEA SEGEREA KAMA UTONA FOLENI NYERERE ROAD.

    WEKA RAMI BARABARA YA M'NYAMALA SINZA MPK MWENGE, MSASANI MPK KWA NYERERE. KAMA WATAONA FOLENI ALY H MWINYI.

    CHUO KIKUU KUTOKEA KIMARA AU MBEZI. MBEZI TO SEGEREA, MBEZI LUISI TO TANK BOVU KAMA WATATONA FOLENI UBUNGO.

    WAMENG'ANG'ANIA MABASI YA KASI HUU NI MRADI WA MTU TU ANATAKA KUUPITISHA ILI ANAFAISHE FAMILIA YAKE. NYIE SUBIRINI MUONE NANI ATACHUKUA HIYO TENDA KAMA SI KINJE AU RIDHWANI.

    WATANZANIA TUAMKE SASA TUWE NA SAUTI YA KUIAMBIA SERIKALI YETU NINI TUNATAKA.

    TOENI MAWAZO YENU SIYO KILA KITU TUMSUBIRI KIKWETE TU.KUNA VITU VINGI TU VYA KUFANYA NA SI LAZIMA MABASI YA KASI.

    ReplyDelete
  3. hayo bus yaendayo kwa kasi ndo yapi hayo ebu tupeni ufafanuzi wataalamu !!

    ReplyDelete
  4. Tarehe Tue Aug 10, 06:15:00 PM,


    wewe mtowa waoni wa kwanza utakuwa kalumanzila !! huoni habari nyingine kabisa ya kukushitua?!

    ReplyDelete
  5. Mimi kila mara nilishamwambia MICHUZI kama kweli unataka kuwa journalist wa kweli you have vto do the following-
    Kwanza sikatai blog unajitahidio sana ku-update news or kinachotokea kila saa. LAKINI TATIZO LA BLOG HII YOUR MISSING FOLLOW-UP NEWS. HII NINA MAANA KWAMBA UNAPOST VERY SENSITIVE ISSUE ZINAZOWAKERA WANANCHI KWA UJUMLA LAKINI UNASHINDWA KUWAKILISHA IDEAS ZILIZOTOLEWA KWENYE BLOG YA JAMII KWA WAHUSIKA. HII NINAITA UPUNGUFU WA UTUOAJI WA HABARI KWA UPANDE WAKO, KAZI WATU NI KUTOA TU IDEAS NA SOLUTION LAKINI ZOTE ZINAISHIA KWENYE KUONGEA TU NO ACTION OR FOLLOW-UP QUIESTION WAT I STATED ABOVE. NILISHAWAHI KUTOA SUGGESTATION HABARI KAMA HIZI MUHIMU ZINAZOGUSA WATANZANIA NOW AND FUTURE TANZANIA INGEKUWA BORA KWA NAMNA YOYOTE UTAFUTE WAHUSIKA WA MIRADI HIYO AU ALLEGATION YOYOTE UWAINTERVIEW KWA NJIA YA VIDEO AU KWA SIMU TUWEZE KUONA NA KUWASIKILIZA WAT THEY SAY NA HII KAMA HUNA MASWALI LETE FOPRUM NI MASWALI GANI UNATAKIWEA KUWAULIZA WANAJAMII WAKUPE KAMA HUNA TOUGH QUESTION TUKUPE. LAKINI MAMBO YA KUONGEA NAKUTOA IDEAS HALAFU HAZIFANYIWI KAZI NA BLOG YAKO AU FOLLOW-UP QUESTION KWA WAHUSIKA I'M VERY SORRY TO SAY I'M TIRED TO SEE THIS DAILY. MICHUZI BADILIKA NA NAOMBA UFANYIE KAZI HAYO MAMBO KAMA UTAHITAJI HIDDEN CAMERA KWA INTERVIEW NAWEZA KUSAIDIA ILI TUWAANIKE WATU UFISADI WAO
    Mdau USA

    ReplyDelete
  6. TATIZO NI KWAMBA NCHI INAONGOZWA NA WANASIASA.MWANASIASA ANASEMA WEKA TUTA HAPO NA PALE NA PALE,TANROADS BADALA YA KUTOA USHAURI WA KITAALAM WANATII AMRI YA MKUBWA .

    BAADA YA MUDA FOLENI NDEFU,KUNA FOLENI KUBWA KUTOKA MBEZI/TEMBONI MPAKA KIMARA MWISHO KWA KUWA TUTA LILIWEKWA KWA AMRI YA MWANASIASA PALE KIMARA STOPOVER.

    Anony wa Tue Aug 10, 06:44:00 PM UMEONGEA POINTI SANA KUHUSU KUBORESHA BARABARA ZA NDANI,VIONGOZI WALIOPO WANATAKA SIFA TU NA HUO NI MTAJI WA KURA KATIKA UCHAGUZI WA RAISI.HAYA YETU MACHO ISIJE IKAIBUKA RICHMOND NYINGINE..

    ReplyDelete
  7. hayo mabasi yatapaa juu kwa juu au ndio yataanza yale mambo ya ukiona hilo basi liko nyuma yako unasimamisha gari lako pembeni basi lipite kwanza...Bongoooooooo

    ReplyDelete
  8. kuhusu barabara nyingine, someni hapa: http://habarileo.co.tz/kitaifa/?n=9253

    ReplyDelete
  9. Hebu nitulie miyeeee.....mabasi yaendayo haraka yatapitia wapi? Magari ya Faya yenyewe hayana pa kupita kukiwa na dharura itakuwa mabasi?

    ReplyDelete
  10. NAONA HAPA WATU WANAPIGA KELELE TU HATA HAWAJUWI HUO MRADI UTAKUWAJE, NA KUNA WENGINE HAPO WANASEMA WAKO NJE LAKII BADO WANAPIGA KELELE KAMA VILE HAJAONA KINACHOFANYIKA HUKO NJE. SASA KWA UFUPI NI HIVI KATIKA NJIA ZILE BASI HIZO ZITAPITA KUTAJENGWA LANE AMBAYO ITAKUWA KWA MABASI TU NA SI GARI INGINE NA GARI INGINE IKIPITA KATIKA LANE HIYO ITAKAMATWA NA KUTOZWA FAINI, PIA UKATAJI WA TIKETI ZA KUSAFIRIA YAANI BUS ZITAKUWA ZINAKATIWA KATIKA OFISI KWA WINGI KULIKO KWENYE BUS, WATA-DISCOURAGE KUKTA TIKETI NDANI YA BUS, PIA KUTAKUWA NA UWEZEKANO WA KUKATA TIKETI YA SIKU MZIMA, YA WEEK NZIMA, YA MWEZI MZIMA N HATA YA MWAKA MZIMA NA TIKETI HIYO UNAWEZAKUPATA BASI LOLOTE KATI YA HAYO MABUS. HII INAFANYIKA KATIKA NCHI ZOTE ZA WEST NENDA LONDON UTAKUTA KUNA LANE ZA MABUS TU MJI MZIMA GARI ZINGINE HAZIRUHUSIWE KUKANYAGA KATIKA LANE HIZO UKIKANYAGA UNADAKWA NA UNALIMWA FINE NA SI LAZIMA UKAMATWE NA POLISI KUNA CAMERA ZIZONYAKA NAMBA YAKO YA GARI NA KUPELKA CENTRAL TRAFFIC OFFICE NA UTALETEWA FINE YAKO KATIKA POSTA USIPOLIPA UTASAKWA UKIBISHA GARI INACHUKULIWA NA KUSAGWA UKIKOMAA KUKATAA KULIPA. SO EBU TUSUBIRI WANAFANYA NINI THEN TUPIGE KELELE.

    ReplyDelete
  11. mdau wa aug 11,4:56 am watu ndio wanuliza hizo barabara za kupitisha mabasi haya peke yake ziko wapi?

    sasa unavyotaka kufanananisha na ulaya kwani barabara zao ziko kama zetu? wamejenga kwa mpangilio kila kitu.

    ReplyDelete
  12. Kaka Michuzi naomba umuulize huyo jmaa aliyetowa hoja 04.56, kwamba hizo basi ndogo HICE ambazo ni za kila polisi na viongozi wote hapo Dar zitafanya kazi wapi? kama kwa sasa hazifuati sheria. kama ni Hice ya kiongozi au ya polisi haikamatwi, je kama trafic polisi yupo juu ya sheria je ni nani atakatishwa hizo tiketi, kwani hata polisi kwenye gari yake anakwenda kazini atapita kwenye hizo lane na baathi ya viongozi je ninani atawapa hizo tiketi. Watu wengi tu nimewaona wanawakatia pesa polisi ili waondoke na hakuna kesi, Watu wengi walevi na wanasababisha ajali na kila siku bado wanendesha mgari yao. Tushukuru mungu kwamba huu mradi utawasaidia sana sisi waendao na mabasi, kwa sisi ambao hatujafika huko majuu tukaona hizo lane kaka michuzi ungetupatia picha tukaona. Pia kuleta technologia mpya bila kuelimisha jamii jinsi gani ya kuitumia ni kazi haswa.Nakuhakikishia watakaolipa Faini ni walal hoi wengi hawatalipa kitu. Na kama unataka kujuwa ni angalia jinsi gani biashara zilivyo nyingi na asilimia 50 hakuna anaelipa kodi na kama hiyo asilimi 50 analipa kodi ni kidogo sana. Kama hiyo campuni ni ya mtu binafsi labda zitadumu, kama ni za serikali ni sawa tu na Tanesco kulipisha watu kulipa milioni na kama huna unaongea na mhasibu mhasibu nashukuwa nusu na wewe unalipa nusu.

    ReplyDelete
  13. KUIACHA BARABARA YA MBAGALA KWENYE AWAMU YA KWANZA YA MRADI NA KUIWEKA BARABARA YA UHURU INAONESHA JINSI WATAALAMU WETU WANAVYOFANYA KAZI BILA UTAFITI KWANZA. BARABARA YA KILWA INA WAKAZI WENGI SANA KULIKO BARABARA ZOTE ZA JIJI HIVYO INGESTAHILI KUWEMO KWENYE AWAMU YA KWANZA.

    ReplyDelete
  14. Anonymous Wed Aug 11, 04:56:00 AM, umeelezea vizuri sana mfumo wa uendeshaji wa mabasi ya haraka naamini hayo umeyapata nchi za wenzetu huko ambako kuna mipango endelevu na mawazo ya wataalamu uheshimiwa. tatizo la bongo upangaji wa miji ulikosewa toka enzi hizo wkt ambao idadi ya watu ilikuwa ndogo mfano leo hii kuweka muundombinu mdogo tu unahitaji uwekezaji mkubwa unaoishia kulipa pesa za kufidia watu na kutatua migogoro itakayochomoza. ukitazama ramani mfano ya mradi inaonyesha hayo magari yatapita ktk nafasi baina ya barabara za sasa(naweza kuelimishwa km siko sawa hapa) kwa mtazamo wangu nafasi hiyo ni finyu mno kuweza kutumika na gari mbili kila upande pasipo kuhatarisha maisha ya watu.

    ReplyDelete
  15. Nawahakikishia mambo mawili 1) Waendesha magari wa kibongo watapita katika hizo barabara za mabasi hayo, wakiwemo watu wa kawaida, maofisa serikalini, polisi yaani watapita.Si unajua Bongo ilivyo! kila mtu anajianya yeye ana haki popote! 2) Huu mradi hautadumu kwa muda mrefu UTAKUFA, ni kweli kuna mtu/watu wachache ndio watakaonufaika, lakini kwa wabongo wengi hasa wakazi wa Dar, watasaga meno kwa sana, kwasababu foleni itakuwa kama kawa. Wabongo hawana sifa ya kuanzisha na kuendeleza miradi endelevu, kwasababu mawazo sio yao, huletwa na wageni kutoka nje kwa maslahi yao. Aliyesema serikali inapaswa iboreshe barabara ndogo ndogo za mji amepatia sana, lakini wazo hilo halina maslahi kwa wakubwa, hawawezi 'kula', na kwa kuwa hawawezi hatasikiliza chochote,

    ReplyDelete
  16. Tatizo nafikiri ni jina lililotumika. Kwani unaposema magari yaendayo kasi inabidi ufafanue, ya sasa hivi yanaenda kwa kasi gani? na hayo yatakayoletwa yataendeshwa kwa kasi ipi?? (140 kph??).

    Neno sahihi ni kuwa na barabara (I mean special lane) au kuboresha public transport system, itakayokuwa na sehemu maalum kwa kupita mabasi ya usafiri wa umma tu (hapa sio viteksi).

    Kwa hiyo inategemewa kwenye hizo lane hakutokuwa na foleni. Nyie mlioko huko majuu nafikiri munaona huu utaratibu.


    Mambo ya kasi hayapo, kamji kenyewe kembamba, yatakuwa yanakimbilia wapi??!!

    ReplyDelete
  17. Huu mradi unafunguliwa kwa maana ya kufungwa? Manake toka tuanze kuusikia!

    Nimeguswa tu na concept ya kuanzisha safari za ndani ya DSM kutumia treni, nafikiri huu ndio mradi unaoonesha matarajio zaidi kuliko huo wa kasi.

    Amenena mdau aliyesema kasi yanakimbilia wapi?

    ReplyDelete
  18. .....Ankal mdau umekupa changamoto muhimu sana kuhusu suala la mrejesho, au feedback. kuna mambo mengi humu yanajadiliwa lakini hayana majibu au hatuna uhakika kama ujumbe unawafikia walengwa. kwa mfano tuliwahi kuomba utuletee sheikh azungumzie mahakama ya kadhi na jinsi inavyo fanya kazi, kuhusu islamic banking,tuhuma za Ruge na Zinduka na mambo kadhaa. Hii blog ingesaidia kuelimisha watu, kuongoza pamoja na kutoa majibu kwenye maswali magumu, kuliko kuzusha ubishani na watu kutoa maelezo au uzoefu usioendana na hoja zao. Story inayozingatia upande wapili ni tamu sana! nawasilisha kwako, ni mtazamo tu!
    Fundi Mchundo Alhaj Said Kubeni.

    ReplyDelete
  19. Wadau hii ni hali halisi ya vijiji vya Tanzania(huduma za afya mbovu watu wanalala chini tu hospitalini).je barabara za magari ya kasi ya nini.wahamishe wizara zote hapa mjini wazipeleke nje ya mji foleni zitapungua
    N.b tuache kupotezaana mda na pesa za kukopa za nini?wizara kibao muhimu zinaitaji pesa .Toa Amri JK viongozi wote Dodoma na wizara zao. STJ Plus STK ziondoke dar halafu barabara za mitaani lami. kazi simple tu(Halafu barabara za mabasi ya kasi ni Dar tu ndio mmeona inamaana mikoa yote 25 inawakilishwa na Dar-TZ ndio maendeleo mkoa huu tu wengine wanaridhika eti )mikoa mingine bado Tanganyika

    ReplyDelete
  20. tafsiri ingine ya kasi ni kwamba yatakuwa hayasubiri mpaka lijae.ndo litoke kituoni.kituoni dakika 15 asubuhi rush hour yote mzigoni saa nne yanafanya kazi machache tisa mpaka mbili usiku yanafanya yote. usiku kila route inakuwa na moja linalopita kila baada ya saa. hapo tutaweza sema bongo hailali. madereva ni full time na wengine part time.

    ReplyDelete
  21. KWELI WAHENGA WAKIARABU WALINENA...TAMAA HUATHIRI AKILI...

    Ugonjwa unajulikana kuwa barabara ni ni ndogo na population ya magari inakuwa kila siku bada ya siku...au hatuna vitengo vya takwimu???

    mimi naamini sana yakuwa akili za viongozi wetu wengi zime kuwa disfunctioning any more.

    lakini hatushangai..HIYO NI MRIADI YA MTU BINAFSI HAKUNA CHA SEREKALI.

    ReplyDelete
  22. anon wa hapo juu [aug 11 08:12:00] umesema! changa la macho plus tamaa. hivi hii miji yetu si ilikuwa na MASTERPLAN toka enzi za mwaka 47? kama sikosei kulikuwa na reli even, toka Wazo hadi bandarini. Ndio ilikuwa aimed at kubeba cement in bulk lakini the line and idea were there.Watu wakauza viwanja. Tatizo la Dar ni hamna mpangilio wa PUBLIC transport.Ingefaa tungekuwa na reli.Oooops nimesahau hata ile ya kati inayotupeleka majumbani kule vijijini tuliwauzia "wawekezaji" bei cheeeeeeeeee! hadi mataruma wakang'oa! JK you need to have a vision and the guts to see it through haya mambo ya kuwachekea washikaji ambao kutwa wanaharibu si mazuri na yatatufikisha WOTE pabaya.What legacy are we leaving to our children and grandchildren? Mara Flyover, mara rapid bus! vyote ndoto za Abu Nuwasi....flyover daladala zitageuka ndege zi fly kweli kweli tena vile hata leseni ukiitaka unaletewa home! kweli Maisha Bora kwa .....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...