Hafla ya Kukabidhi Hati Idhini (charter) za Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inapenda kuuarifu umma wa Tanzania kuwa, imekamilisha zoezi la kukabidhi hati idhini (Charter) za vyuo vilivyowasilisha rasimu zao katika hafla itakayofanyika kwenye viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano, tarehe 18 Agosti 2010.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakabidhi rasmi hati idhini kwa wakuu wa vyuo vikuu kumi kama ifuatavyo:
1. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam atakayekabidhiwa hati idhini za:
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu, Dar es Salaam (DUCE)
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Iringa (MUCE)
2. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo atakayekabidhiwa hati idhini ya:
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara, Moshi (MUCCoBS)
3. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini atakayekabidhiwa hati idhini za:
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo)
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Sebastian Kolowa, Lushoto (SEKUCo)
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba cha Kikristo cha Kilimanjaro (KCMCo)
4. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania atakayekabidhiwa hati idhini za:
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mwenge, Moshi (MWUCE)
* Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba na Sayansi za Afya cha Weill Bugando, Mwanza (WBUCHS)
5. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dar es Salaam (HKMU)
6. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, Mbeya (TEKU)
7. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia, Dar es Salaam (IMTU)
8. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania, Dodoma (SJUT)
9. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM)
10. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Tunguu Zanzibar (ZU)
Zoezi la kukabidhi hati idhini lilifanyika kwa mara ya kwanza tarehe 5 Machi 2008 ambapo vyuo saba vya serikali vilikabidhiwa hati idhini kama ifuatavyo:
1. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2. Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
3. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
4. Chuo Kikuu cha Mzumbe
5. Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya Muhimbili
6. Chuo Kikuu cha Ardhi
7. Chuo Kikuu cha Dodoma
Institute of Finance Management (IFM) Mpo wapi????? Bado mmelala tu. Hicho chuo huku nje kwa kweli hakitambuliki. Ni vigumu sana kumuelewesha mtu akaamini kuwa hiyo pia ni elimu ya juu. Vyuo vingi vilivyoorodheshwa hapa juu vimeanza miaka ya karibuni. IFM tangu 1972. Amkeni Jamani!!!
ReplyDeleteMdau Ughaibuni.
Mdau wa ughaibuni,J
ReplyDeleteni politics tu kuhusu IFM, serikali haitaki kiwe chuo kikuu kwa sababu zisizojulikana,huku ikijulikana mfumo wa ufundishaji wa ifm ni bora kuliko vyuo vyote vilivyopo TZ,
angalia hivo vyuo tajwa hapo juu,mtu upo hapahapa TZ na hujawahi kuvisikia, havina tija yoyote, vipo vipo tu for the sake of it.
Ni vigezo gani vinatumika kuset standard za chuo kuwa chuo. Je ni kigezo gani kinaikwamisha IFM isiwe katika hiyo list ya vyuo vikuu, ukizingatia ni moja ya chuo kinachotoa elimu yenye ubora wa hali ya juu ambayo ukiilinganisha na vyuo vilivyotajwa hapo juu haina tofauti hata kidogo.
ReplyDeletehiyo elimu ya ubora wa hali ya juu unalinganisha na wapi???wabongo bwana kwa sababu umesoma hapo basi ina ubora wa hali ya juu!!!!!!
ReplyDeleteYaaani wanawabania tu IFM... Kuna vyuo wala havina kabisa viwango... Ni ishu tupu hiko chuo... Si ndio hawahawa tunasoma na tunaona kwa media..jinsi vilivyo sio vyuo vya viwango.. Tena vingine hapo ni ukabila mtupu... Mpaka wanafunzi wanakandamizwa... lakini kama wewe ni wa kabila fulani tena una godfaza umepeta...Tusiangalie side moja tu... Vyuo vingi ni mitaji na elimu watoayo ni mbovu na yabidi mtu usote haswa.. inabidi waseme vigezo vitumikavyo kwa kweli... wamejaza mitoto yao tuuu ambayo ni mimbumbu... sijui product itakuwa nini kama si uozo... ndo yale badala ya operesheni ya kichwa itakuwa ya mguu... Bad enuf hao TCU wanavijua na wanajua uozo uliopo bt still eti wako kwa list..Ndio maana watu na wazazi watafight watoto wetu wakasome nje...
ReplyDeleteacha kele zako wewe kisa umesoma hapo IFM ndo unachonga eti vyuo vingine vipo vipo tu tatizo huvijui na uwezo wakusoma huko huna/hukuwa nao, kwanza ada za hivyo vyuo zipo juu na uwezo hukuwa nao; kama unataka kujua vigezo vilivotumika unajua mahala husika tembelea tovuti utapata kwa undani na barua pepe utatuma acha kulemaa na kiadvance diploma chako ulichopataga hapo!
ReplyDelete