Assalaam Alaykum
Vipi hali yako kaka michuzi,pole na shughuli zako za kila siku.
Nilikuwa naomba kukiwa na uwezekano uitangaze hii website mpya ya kiisalaam
ili ndugu waislam waweze kufaidika hasa
katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ambao wataweza Kusoma na Kusikiliza Quran moja kwa moja pia na lecture mbalimbali za kiingereza na kiswahili kutoka kwa mashekhe mbalimbali ndani na nje ya Tanzania,
Inşa-llah ukifanikiwa katika hili kheri itapatikana Dunia na Akhera kaka Michuzi kama unavyojua huu ndo mwezi wa kuchuma
kwa waislam wote duniani.
Asante in Advance.
Mdau kutoka Turkey-Izmir
Kassim Kingalu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Jazakamu llah kheir!
    website ni nzuri mashallah na wengi watapata faida

    ReplyDelete
  2. Jazaka Llah kheir. Website ina vitu vingi vya msingi na ni user friendly. Napendekeza pawepo na small articles nyingi kuzidi video clips kwa kuwa internet speed yetu huku bongo si kubwa sana - ili wanaotumia inetrnet caffes nao wafaidike. For me its just perfect. The articles are well researched and the scholars are of high regard: Naik, Deedat, H. Yahya, etc

    ReplyDelete
  3. Hongera sana bwana Kasimu ,İnshalah mungu akujaalie neema na baraka tele.


    Mdau Avcılar.

    ReplyDelete
  4. Hongera Kassim, May Allah be with you, helps us to realize our fortune and dedicate all we have to him through our deeds, Website ni nzuri..na idea pia ni nzuri, Allah akuzidishie Inshallah.

    ReplyDelete
  5. Ahsanteni sana woote kwa ujumla inaş-allah Allah Atupe kheri sote.
    Kuhusu swala la kuweka Articles nyingi za kusoma ni kweli kabisa kwa watumiaji wa Tanzania,nita jitahidi inşa-allah,ila kwakweli nlifikiria hilo lkn kiuhalisia waislam wengi tumekuwa wavivu wa kusoma,wengi tunapenda vitu vya kuona na kusiliza :) ndo maana nkajitahidi kuweka video nyingi na mawaidha,lkn ili tusiwanyime haki wanaopenda kusoma itabidi tufanye hvo.Ahsanteni sana kwa uşauri wenu wakubwa,nahitaji uşirikiano wenu katika kuifanya website hii kuwa bora zaidi na Hai
    kassim kingalu
    kingkessy@jabalhira.com
    masalaam

    ReplyDelete
  6. Jazakallah Khayr.Mungu akuzidishie hamasa ya kufanya kheri na kuwakumbusha ndugu zetu ktk imani.
    Mdau Eskişehir.

    ReplyDelete
  7. tunashukuru sana na Mola akupe pepo inshaAllah itatusaidia wengi.

    ReplyDelete
  8. Amin amin kwa sote inşa-llah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...