Mwenyekiti wa Yanga aliyemaliza muda wake, Imani Madega (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiana ofisi leo mchana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lloyd Nchunga.
Na Mwandishi wa Globu Ya Jamii

MWENYEKITI wa zamani wa klabu ya Yanga, Iman Madega leo amekabidhi rasmi ofisi kwa mwenyekiti
mpya wa klabu hiyo,Lloyd Nchunga ikiwa ni pamoja na akaunti nne za bank ya CRDB zikiwa na jumla ya shilingi milioni 200 pamoja na madeni wanayodaiwa shilingi milioni 29.8.

Katika makabidhiano hayo Madega alisema kipindi cha uongozi wake kulikuwa na mikwaruzo ya hapa na pale na mfadhili wao Yusuf Manji lakini ilikuwa ni changamoto kubwa kwao kuhakikisha wanaifikisha Yanga kwenye kilele cha mafanikio.

Pia Madega aliishukuru kampuni ya bia Tanzania (TBL) kuwa ni wadhamini wao wakuu ambao wamekuwa wakiwapa shilingi milioni 17.6 kila mwezi kwa ajili ya kulipa mishahara ya wachezaji na benchi zima la ufundi.

"Nakukabidhi akaunti nne moja inashilingi 76,000 na nyingine ina shilingi 70,095,000 na nyingne ina shilingi 197,869,700 na hii ya nne haina kitu jumla ya fedha zote tulizoacha kwenye akaunti ni milioni 200."alisema Madega wakati akitoa mchanganuo wa fedha zilizopo kwenye akaunti za klabu hiyo.

Pia alisema madeni wanayodaiwa ni hoteli ya Tamali iliyopo Sinza inawadai shilingi milioni 6.6 kampuni ya All Sports Promoters shilingi milioni 10 hoteli ya Valley View shilingi milioni 5.5 shilingi 500,000 kwa mdau wa Yanga ambae aliwauzia basi ambalo lipo Yard na Dawasco shilingi milioni 6.7.

Madega alikabidhi pia mikataba ambayo ni ya TBL ambayo wana mkataba wa miaka mitatu ambayo kila mwezi wanatoa shilingi 17.6m kampuni ya Afrika Medecal Investiment 'AMI' wana mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuwapa matibabu wachezaji, mabasi matatu ya Yanga ambayo mawili yametolewa na TBL na moja uongozi wake walilikuta ambalo ni bovu na lipo Yard huku likidaiwa shilingi 500,000.

"Tumepata pia logo kwa msajili ya makampuni ili klabu iweze kujiendesha kibiashara kwa zaidi ya shilingi milioni 10 hivyo ni jukumu lenu kuitumia kwa ajili ya kuendesha shuguli mbali mbali zitakazoiwezesah klabu kujiendesha kibiashara na kuachana na utegemezi."alisema Madega
Madega alisema mahesabu ya klabu hiyo hivi sasa yanafanyiwa kazi kwa mkaguzi wa mahesabu kampuni ya TAC Associate.

Naye mwenyekiti mpya Lloyd Nchunga alimshukuru Madega na kuaidi kuyafanyia kazi yale yote mazuri na kuyaendeleza kwa manufaa ya Yanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Sisi wanayanga tunatoa shukrani za pekee kwa muda wote ambao madega amekua kiongozi wetu. Pia tunatoa shukrani za pekee kwa kitendo chake chakukabidhi klabu ikiwa na mwelekeo na pia bila kinyongo.

    Tunakutakia kila la kheri kwa kila shughuli utakayokua unafanya. Yanga mbele Daima

    ReplyDelete
  2. Matari, MafiaAugust 11, 2010

    Hawa Yanga, hata hesabu za kujumlisha tu zinawashinda; Huo ubingwa ndio mtausikia kwenye vyombo vya habari kila siku.

    ReplyDelete
  3. Nyie Yanga kwa nini hamlipi madeni na pesa mnazo? au mnasubiri ajitokeze mfadhili wa kuwa anawalipia madeni yenu? mnajisikia raha gani kusema akaunti yenu ina mil. 200 wakati mna madeni kibao!sio vizuri kukaa na madeni lipeni.

    ReplyDelete
  4. Hongera Madega kwa kukabidhi uongozi mpya yale yanayomilkiwa na Yanga. Kizuri zaidi ni fedha shs.milioni mia mbili ambazo umezikabidhi kwa kina Nchunga. Kassim Dewji amepewa tuzo na Simba hebu tujiulizeni uadilifu wake. Simba ni waoga Kassim amepangisha majemgo ya Simba na kuchukuwa fedha zote,ameuza wachezaji nje na kutia ndani fedha. Kibaya zaidi ni ile danganya toto kwamba Uhuru Selemani ana Ramadhani Chombo walitakiwa na Hars al Huduud. Huyu bwana si mkweli kwani kuleta uzushi ule nilisema kwamba ni zuga aliyowafanyia Simba baada ya kufanya biashara ya kuuza mechi. Alijaribu na Zamalek ikavuja na wakagombana na Sianga. hONGERA mADEGA KWA KUONYESHA UADILIFU. sIMBA HAINA UTAMADUNI WA KUKABIDHISHA FEDHA KATAIKA AKAUNTI ZAKE UONGOZI MPYA UNAPOINGIA MADARAKANI. TUMUULIZE RAGE KAACHIWA KATIKA AKAUNTI YA SIMBA MILIONI NGAPI?

    ReplyDelete
  5. Hongera Madega kwa kuwa muadilifu, vilabu vyetu vya Simba na Yanga sio kawaida uongozi kukuta fedha ktk akaunti, lakini mwandishi mbona hesabu iliyoainishwa hapo ni zaidi ya TZS 200M? Kuhusu Anony wa 11.50pm nadhani malalamiko yako kwa Simba ungeyaelekeza kwa uongozi uliokuwepo madarakani wakati hayo yakitokea na sio Kassim Dewji kwa kuwa yeye hajapewa dhamana na wana simba kufanya hayo vile vile usisikilize maneno ya mtaani yaliyojaa uongo, uzushi na fitina, tafuta ukweli kabla hujamtuhumu mtu tena kwa kumtaja jina nadhani hujamtendea haki.

    ReplyDelete
  6. MliakuvanaAugust 12, 2010

    Kuwa na madeni au kutokua nayo sio hoja! Hivi lini klabu zetu hizi kubwa zimeweza kabidhi akaunti zenye hela? Hebu muulizeni Dalali na Rage walikabiziana akaunti zina hela ngapi?

    Well done Yanga! Hilo deni la milioni 50 litalipwa tuu kwenye makusanyo ya kombe la hisani, no issues hapo!

    Yanga bwana, we acha tuuu!!!!

    ReplyDelete
  7. Hongera na pongezi nyingi sana kwa Uongozi wa Madega na wenzake, hii ni mara ya kwanza ktk historia ya nchi hii kukabidhi uongozi wa mpira wa miguu na kukuta pesa ktk Akaunti wanastahili pongezi nyingi sana killa la kheri,Tunawataka na hao kina Nchunga wajitahidi ziongezeke zaidi na zaidi sio zipunguwe,maana hata mishahara inatoka kwa wadhamini,na pia Nawapongeza Simba kukabidhiana jengo chafu na deni la umeme na akaunti zina pesa kiasi cha shilling 000.052.700/=

    ReplyDelete
  8. BONGO PATAMU PESA ZILIZOPO KWENYE ACCOUNT NI 70,095,000 NA 76,000 NA 197,869,700 UKIZIJUMLISHA HIZI PESA KIBONGOBONGO UNAPATA MILLION 200, BADALA YA 268,040,700. BONGO PANALIPA.

    ReplyDelete
  9. Duh! hengereni sana wanayanga, kwa mara ya kwnza mmeonyesha uwezo mkubwa wa kutuza fedha, hapo nawapozaaaaaa saaaaaana, abayeuliza madeni waka pesa zipo, mwambie aende hata TRA nao wanamadeni, hakuna biashara isiyo na madeni, kwani hata michango ya ya wanachama yaweza kuwa madeni kwa club

    ReplyDelete
  10. Duh! hongereni sana wana-yanga, kwa mara ya kwnza mmeonyesha uwezo mkubwa wa kutuza fedha, hapo nawapozaaaaaa saaaaaana, abayeuliza madeni wakati pesa zipo, mwambie aende hata TRA nao wanamadeni, hakuna biashara isiyo na madeni, kwani hata michango ya ya wanachama yaweza kuwa madeni kwa club

    ReplyDelete
  11. TUNASHINDWA KUENDESHA KLABU ZA MICHEZO KIUCHUMI NDIYO SABABU TUNASHINDWA KUENDESHA NCHI KIUCHUMI. MIAKA ZAIDI YA HAMSINI KLABU INA SHILINGI MILIONI MIA MBILI! ZINGINE ZIMEKWENDA WAPI? TEMEKE INAKUSANYA MAPATO MAKUBWA SANA NCHINI, KUCHAFU! MAPATO YANAKWENDA WAPI?

    ReplyDelete
  12. MASKINI MADEGA WEE SASA ULIACHIA YANGA UKIDHANI UTAUPATA UBUNGE SASA UMEKOSA YOTE UTAKULA WAPI LOL???@@@!!!

    ReplyDelete
  13. Ukisoma ramani ya uso huyu bwana anayekabidhi ni muadilifu, ila mi nna mashaka na huyo anayekabidhiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...