Haya ndiyo baadhi ya Magari kati ya 100 yanayoshindaniwa katika promosheni ya “Shinda Mkoko”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. Hadi sasa Magari 8 tayari wateja wa Vodacom wamejishindia tangia promosheni hii ianze na bado 92 yanawasubiria wengine.


Baadhi ya washindi wa magari ya Hyundai i10 yanayotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake ya ‘Shinda Mkoko’ wamesema zawadi hiyo itawasaidia kukuza uchumi wao kwani itarahisisha usafiri katika shughuli zao.

Akizungumza kwa njia ya mahojiano kutokea Dodoma baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa promosheni hiyo, Tolino Pechaga ambaye ni fundi umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema anatumaini gari hilo litakamilisha ndoto yake ya kimaisha katika kujiletea maendeleo.

Akifafanua alisema, ingawa alikuwa akitumia magari ya wafanyakazi kutoka Maili mbili anakoishi hadi Udom, ujio wa Hyundai i10 utamaliza muda wa kukimbizana na basi hilo na kumpa nafasi ya kufanya kazi zake binafsi baada ya muda wa kazi kwa mwajiri wake.

“Unajua mimi ni mwajiriwa wa chuo, lakini nafanya pia kazi zangu binafsi. Usafiri ulikuwa kikwazo namba moja kufikia malengo yangu, lakini sasa kila kitu kitaenda sawa kwani tayari nitakuwa na usafiri wangu binafsi utakaorahisisha maendeleo yangu,” alisema Pechaga.

Kwa upande wake Benard Asenga wa Keko Magurumbasi jijini ambaye ni mfanyabiashara wa duka la bidhaa ndogondogo na vyakula alisema alikuwa akitumia muda mwingi na baiskeli kufuata bidhaa sokoni Kariakoo, lakini gari hilo litamuwezesha kuboresha utoaji huduma kwa wateja wake.

Aidha Asenga alifafanua kwamba mara baada ya kukabidhiwa Hundai i10 aliyojishindia atabadilisha mtindo wa biashara anaoufanya na anafikiria kuwa mjasiriamali wa kati (SME’s) na kumiliki duka la bidhaa za jumla na rejareja.

“Sasa sitatumia tena baiskeli kufuata bidhaa mjini, nafikiria kukuza biashara yangu kutoka hatua moja kwenda nyingine jambo litakaloniwezesha kukuza hali yangu kiuchumi,” alisema mfanyabiashara huyo.

Naye Simon Kihuru ambaye ni dereva wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songea alisema zawadi hiyo iliyotolewa na Vodacom Tanzania itampunguzia gharama za usafiri kwa ajili kuwapeleka na kuwarudisha watoto wake shule kwani wataweza kutumia gari hiyo kwa matumizi ya binafsi.

“Kama nilivyosoma kwenye magazeti mbalimbali kwamba gari hiyo haitumii gharama kubwa kuihudumia, kwa kuwa mimi ni dereva itaniwezesha kutunza fedha zangu baada ya kukwepa huduma za daladala ambazo sio salama sana hususani kwa watoto,” alisema Kihuru.

Akizungumza hivi karibuni kwenye hafla ya uzinduzi wa promosheni ya ‘Shinda Mkoko’ iliyopanga kuwazawadia wateja wake gari moja aina ya Hyundai i10 kila siku Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru alisema shindano hilo litawahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini na kwamba ndani ya siku 100 kila siku mtu atakuwa anajipatia gari moja.

Alisema promosheni hiyo ni moja kati ya shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya miaka kumi ya utoaji huduma wa Vodacom Tanzania nchini. Mpaka promosheni hiyo itakapokamilika tayari magari 100 ambayo kila moja litakuwa na thamani ya milioni 12/- yatakuwa yameshatolewa.

“Katika kusherehekea maadhimisho haya ya utoaji huduma zenye mafanikio kwa wateja wetu na jamii kwa ujumla, tumeona tutumie fursa hii ya kumbukumbu ya miaka kumi ya utendaji wa Vodacom Tanzania kwa kurudisha faida iliyopatikana kwa wateja wetu,” alisema Mafuru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Za Leo kaka,mimi nina maswali na hawa voda, bado sielewi elewi, hilo shindano lao linachezeshwa saa ngapi, manake pale kwenye TBC huwa siyo live, kwa kweli wanajua kutega, kama ni hela wanakula si mchezo, ukituma tu unaliwa na wala namba ya simu yako hata kwenye shindano hujuwi kama imeingizwa au la.

    hafu internet ya voda kuna siku inakuwa na kwikwi, kama jana usiku na juzi ilikuwa haipatikani, kabisa, ikitokea haipatikani wa kumuuliza ni nani au kifanyike kitu gani?
    Nipelekee ujumbe kaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...