Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka (TFF) Frederick Mwakalebela anayegombea ubunge wa Iringa mjini kupitia CCM bado anadunda na wala hakuwahi kukamatwa na kuswekwa lupango kama inavyodaiwa.

Wakili wa Bw. Mwakalebela, Mh. Alex Mgongolwa, kaiambia Globu ya Jamii kwa njia ya simu sasa hivi kwamba mteja wake hakuswekwa rumande kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti leo kwamba jamaa kadakwa kwa kosa la kutumia rushwa ili ashinde katika kura za maoni.
Kwa habari kamili pamoja na
taarifa ya TAKUKURU Iringa
nenda libeneke jipya la michuzipost.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mdau, BloomsburyAugust 12, 2010

    Michuzi,
    Amani iwe nawe. Mwezi mtukufu umeanza naomba uache kubania comments zangu.

    Swali kuhusiana na wakili wa Mwakalebela. Kwanini umemuita Mheshimiwa? Naona huu mtindo sasa umezidi. Kwanza hao waheshimiwa wanaheshimiwa na nani, si ni sisi wananchi ndio tunaowachagua? Hivyo, kihalali, mwananchi wa kawaida ndiye 'mheshimiwa'.

    ReplyDelete
  2. Kwa utaratibu wa CCM na mizengwe yake Bw. Mwakalebela hatapitishwa hata kama hana hatia mahakamani. Toka mwanzo nilijua kwamba utaratibu wa TAKUKURU ni njia ya kupunguza malalamiko ya wanachama kama mgombea akienguliwa maana wakuu wa TAKUKURU wa mikoa wanapata ruhusu toka kwa mkurugenzi mkuu bila shaka baada ya kupitishiwa vikaratasi!

    ReplyDelete
  3. Marangu OneAugust 12, 2010

    Kampeni za mwaka huu ni za kisayansi zaidi. Ndiyo maana wazee wanapigwa chini kila kona.

    Mwakalebela kajipanga hasa. Angalia hilo gari. Angalia Wakili wake. Siyo mchezo.

    ReplyDelete
  4. Huu sio uchimbi bali ni haki ya kutaka kujua hali ya kiongozi wangu wa baadae,anae nivutia kwa maneno na vtakrima vya chini kwa chini ili nimpe dhamana ya kwenda kuniwakilisha mjengoni. Huyu muheshimiwa mtarajiwa alikuwa na chanzo kingine cha mapato tofauti na ajira ya TFF au?coz hii shutuma ya rushwa inanifanya niwe na kwikwi nikikifiria dhamana ya 5yrs anyoomba ya kuniwakilisha...kwani kama wadanganyika wanakukubali kuna haja gani ya kumwaga mlungula, tze tunaelekea wapi jamani?

    ReplyDelete
  5. naomba ankal tewekane sawa kwanza, alex mgongolwa sio mheshimiwa. kiprotokali waheshimiwa ni majaji, wabunge, mabalozi na rais. sasa huyu mgongolwa yeye ni mwanaseria tu, hawezi kuwa mheshimiwa. akiutaka uheshimiwa aende akagombee ubunge kama wengine. i stand to be corrected. tatizo kila mtu bongo anataka kuitwa mheshimiwa. ndio maana daima nitakumbuka enzi za kuitana ndugu!

    ReplyDelete
  6. ankal kweli kiboko mpaka unamichuzi post kweli unajua kuangaika kama watanzania wote wangekuwa wanajua kutafuta maisha kama wewe unavyojaribu tungekuwa mbali mungu akujalie

    ReplyDelete
  7. Sasa inatakiwa iwepo sheria yakumtaka mgombea aweke source ya mapato yake ya kampeni. Huyu alikua TFF hizi hela zote za kampeni kapata wapi? Si mbaya wananchi tunaompigia kura tujue kwa kila mgombea ili tuende na uwazi na ukweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...