Mgombea urais kwa Chama cha NCCR Mageuzi, Mh. Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho leo jijini Dar.
Chama cha NCCR-Mageuzi kimezindua ilani yake ya Uchaguzi huku kikitaja mambo 12 ambayo chama hicho kitaelekeza nguvu iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi.

Wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa Ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.

“Ajenda yetu kuu itakuwa ni katiba, tumeanisha mambo yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo, hili ndilo nataka wagombea wetu mlizungumzie kwa kina,” alisema Mbatia.

Lakini pia Mbatia aliwataka wagombea ubunge na udiwani wa chama hicho kuendelea na kampenzi zao katika maeneo yao, lakini waepuke kuwasema watu au kutumia lugha za matusi badala yake amewataka wazungumzie hoja na matatizo yanayowakabili wananchi.

Kutokana na baadhi ya mambo hayo, Mbatia aliwataka Watanzania wakichague chama hicho kwani kitendo cha Oktoba 31 kinaweza kuwafanya wajutie kama watarudia makosa ambayo wamekuwa wanayafanya katika chaguzi zilizopita.

Lakini pia aliwataka wagombea hao kuacha tabia ya kutumia majukwaa kuzungumza watu na kueleza kuwa kufanya hivyo ni umbeya. “Epukeni kujadili watu, msitumie matusi kwani mtakwaza watoto iwapo mtatumia matusi.”

Alisema wagombea wakichambua hoja Watanzania wanajua mchele na pumba, na kwamba kuna matatizo mengi yanayowakabili Watanzania ikiwemo ukosefu wa maji, lishe “lakini kikubwa mwaka huu hoja yetu kubwa itakuwa ni katiba.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Is this guy serious?

    ReplyDelete
  2. He is serious if you are....

    ReplyDelete
  3. watu wengine bwana. maudhi tu

    ReplyDelete
  4. Kimeo hichoo...sura yenyewe hana wala mvuto...

    ReplyDelete
  5. Ni nini haswa kilichokuudhi? Badala ya kuchukia umaskini wakujitakia, ambao umetawala nchi yako. Unaudhika unapoona watu wanataka kubadilisha mambo. Kaazi kweli kweli...

    ReplyDelete
  6. Jamani mwenye ilani ya uchaguzi ya NCCR Mageuzi, CCM, CUF na CHADEMA anitumie kwa kawogo@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...