Pichani kulia ni mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na redio ya Clouds FM 88.4,Gerald Hando akipeana mkono na mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Joseph Serukamba mara baada ya kumaliza mahojiano yao leo asubuhi.shoto kwake ni Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga, Mdau January Makamba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. CHADEMA welcome again kigoma urban!!!

    ReplyDelete
  2. nimewasikiliza wadau.Januari hongera nimeona kumbe wewe tofauti na mzee wako wa maneno tu umeongea pointi na umeonyesha busara,sasa tekeleza maneno mazuri uliyoyatoa.

    ReplyDelete
  3. Ankal lazima niseme ukweli mimi nilikuwa msomaji wa ile Jambo Forum na nilikuwa simkubali huyu Bwana Makamba kwa jinsi wadau walivyokuwa wanaandika. Lakini nimekuwa namfuatilia tangu aingie kwenye ulingo wa siasa nchini na nimeanza kusoma maandiko yake na kumfuatilia lazima niseme ukweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, bwana mdogo yuko vizuri na amejipanga vizuri na Muungwana JK kumteua msaidizi wake wa karibu kuanzia foreign hadi sasa aliona kitu kwake ambacho sisi wengine imetuchukua muda kukiona na huyu dogo inaelekea kila anachofanya ni sehemu ya mkakati na sasa amekuwa gumzo hapa town. Mimi nasema tumtazame sana. Ila na yeye asije kutuangusha.

    ReplyDelete
  4. Biashara nzuri (msimu);
    Wagombea wanapata airtime<> Clouds FM wanapata wasikilizaji.
    Next time weka waungwana walioshindwa kura za maoni!

    ReplyDelete
  5. Muda wa compaign hao ccm si wanasema bado, hao sasa wameongea hapo kwa capacity gani?halafu clouds wametumia criteria gani kuwaita hao?au radio ina maslahi nao?pia wamezungumzia masuala ya rushwa kwani wao imethibitika ni wasafi?hao mkono wa dola tu haujawapitia na kuwaweka hadharani?pia waandishi wa kitanzania jifunzeni namna ya kuuliza maswali kwa watu kama hao.Gerald alikuwa anuliza swali kabla halijajibiwa anajibu mwenyewe kwanza, mfano aliuliza changamoto walizokutana nazo, kabla hajajibiwa akaanza kusema maana tumesikia masuala ya rushwa etc.Michuzi kama usipo post hii comment basi i print uwapelekee tafadhali

    ReplyDelete
  6. Hayo mahojiano yalifanyikia Bumbuli au wapi? Maana kumekaa ki-village village hivi.

    ReplyDelete
  7. wameanza campeign kabla ya muda wake, CCM wajanja

    ReplyDelete
  8. gerlad nywele hujachana. jaman kaka yangu mwe au ndo afajiri hiyo

    ReplyDelete
  9. Nawapa shavu mmewakilisha vizuri ila makamba ameonekana kama ndio mbunge mzoefu wakati ndio anzaana kabsa!

    ReplyDelete
  10. Ok,Gelald tumewasikia, twaomba kusikiliza na upande wapi, waite nyika na Zito napo mjengoni

    ReplyDelete
  11. Huyo anony wa tatu ni Januari mwenyewe au watu wake.

    ReplyDelete
  12. anonymous 03.57 pm nywele hizo ni waves wanaita wenzenu wa majuu kabda ujatoa hoja hakikisha unajua unachoongelea

    ReplyDelete
  13. kazi kweli kweli! haya mazungumzo yanapatikana wapi mtandaoni tumsikie JM anayekuja kwa kasi kwenye siasa za bongo. John Mashaka vipi uko wapi?

    ReplyDelete
  14. wote wamejitahidi sana.Gerald naye kaonyesha ukomavu kawavaa safi. Wapewe nafasi tuwaone. Ankal Januari makamba ana shea na globu yetu siku hizi au ndio mambo ya mhogo wa futari. Natania endelea kumrusha maana sasa yeye ndio news bongo.

    ReplyDelete
  15. Ndugu zangu wa Clouds, tunawaomba msome alama za nyakati na mjaribu kuonesha kwamba nyie sio mawakala wa CCM. Muwaite na viongozi wa chama mbadala - Chadema (CDM) ili nao muwahoji na watu wawasikie. Muiteni John Mnyika na Zito Kabwe ili muwe fair.

    ReplyDelete
  16. Safi kaka, kwa kutuletea wagombea hao, Next time tuitie wa chama kingine ili kuepusha bias ya chombo chako, nasi wasomaji na wapiga kura tupime maji na mchele.

    ReplyDelete
  17. Mi naona, huyo Wa KIGOMA angeulizwa amefanya nini tangu aingie madarakani miaka mi 5 iliyopita, manake barabara za mitaani zote kigoma mjini (mwanga, mlole, ujenzi mnarani na kwingineko)hazitamaniki, achilia barabara stendi tu ya mabasi haipo yaani inatia huruma, mikoa mingine yote TZA hasa mjini ina stendi za mabasi ya kueleweka.

    Mkoa hauna hata barabara ya rami kuunganisha wilaya na wilaya, kwa taarifa yako KIGOMA haiendelei kwa kuwa haina miundo mbinu madhubuti. pigania hilo kaka Nyie ndo tunawategemea kwa maendeleo ya mkoa. Si unaona wakazi wake walivyo na juhudi binafsi za kutafuta maisha.

    Afadhali ZITO tutamkumbuka daima, kajitahidi ni jimbo lake tu lenye barabara ya rami kilometa 96.

    Tatizo jingine na hao watangazaji wanaowahoji hawatoki huko wagombea wanakotoka wakajionea hali halisi ili wawaulize vizuri.

    Any way Hongereni kwa kupita mchujo wa kwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...