Home
Unlabelled
RAIS KAGAME AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI MKUU RWANDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
huyu jamaa atatawala mpaka lini?
ReplyDeleteyaani tokea 1994 then atawale kwa miaka saba ijayo, ina maana atatawala miaka 16+7=23
miaka 23 madarakani kwa democrasia ya leo ni uhuni
96% alizopata ni za wapiga kura waliopo nje ya Rwanda, kura za walio ndani hazijakamilika kuhesabiwa. Hata hivyo haishangazi kwa Kagame kushinda namna hiyo kwa kuwa wapinzani wote wenye nguvu walifanyiwa zengwe wakashindwa kugombea pia ikumbukwe kwamba hali halisi ya rwanda hakuna kiongozi mwingine anayeweza kuongoza na dola ikamwachia. Kagame ametengeneza hali fulani ambayo kiongozi lazima awe yeye tu vinginevyo jeshi litachukua nchi.
ReplyDeleteGangeni ya kwenu!!
ReplyDeletenyinyi watu,mmi ni mtanzania na ninamsupport KAGAME.kagame aliyofanya katika nchi yake ni wachache walioweza.
ReplyDeletekwa nchi ambayo bado ni changa hasa ukizingatia imetoka katika vita ya wenywe kwa wenyewe nathani bado anahitaji muda zaidi kuinyosha na kuunganisha watu.
hivyo ndiyo KAGAME anafanya,sio kuharibu bali kuwaleta watu wote.Wengine wanamkejeli kwa kauli yake kwamba sisi ni wanyaruanda,na siio hutu wala tutsi.
acheni propaganda,za mitaania.KAGAME IS RIGHT FOR NOW
na nina msupport.
kagame sio kama viongozi wetu tanzania ambao hawana uchungu na nchi.
michuzi usibanie!!!!
ahsante.
Afadhali mkuu umerekebisha hapo juu, 96% is a joke for democracy, how come?
ReplyDeletekagame hawezi kuwa shujaa kwa kisingizo eti kaleta amani nchini rwanda lazima tujiulize ni nani waliokuwa wanaleta machafuko kiasi cha nchi kuingia ktk machafuko yaliyozaa mauaji ya halaiki km sio kagame huyohuyo na maswahiba wenzake? nchi imetulia kwa sababu yeye km msababishaji mkuu kapata alichokitaka japo ni kwa damu ya maelfu ya wananchi wenzake.
ReplyDeleteKAGAME DESERVES THIS FOR THE GOOD OF RWANDA AND THE PEOPLE. YOU CANNOT CHANGE THE FACT.
ReplyDeleteKweli gangeni ya kwenu! Tanzania mnawapa watu kwa miaka kumi na wanaondoka wamejilimbikizia mali, watanzania wanabaki maskini! Angalia Kagame anayofanya Nchini Rwanda! Miundo mbinu, utawala wa sheria, usafi wa miji yao, mapambano dhidi ya Rushwa na mengine mengi. Hata pesa ya Rwanda sasa inathamani kubwa kulinganisha na Tanzania. Nenda na shilingi mia ya Tz, utapata 50 francs za Rwanda! Tz tunakalia kisiwa cha amani! wakati wachache wanajirimbikizia mali! Watanzania fumbukeni macho!! acha kuhesabu miaka ya utawala wa viongozi wa nchi nyingine wanaokubalika, angalia kwako ufanye nini uondokane na umaskini uliokithiri!!!
ReplyDeleteKagame lazima shinde kwasababu ukionekana kwamba uko pembeni na yeye hapo unaingia jela au kufa moja kwa moja,,hata wapinzani wake wakali wamesota ndani ya jela,wengine wanakoswakoswa kuuwawa,Uongozi wa nchi zetu ni kukaa zaidi ya miaka ya 20,,hata Burundi ni hivohivo Uganda hivohivo,Tanzania bado ccm inaongoza kwa kupishana ingawa nni chama kilekile ,na bado hatujavuka Zimbambwe sasa,hakuna rais anayepisha wengine bila ugomvi.Ni mdau wa Kigali
ReplyDeleteKageme hata kama angeitawala Rwanda kwa miaka 40 binafsi sina kipingamizi.
ReplyDeleteKagame ni mfano wa kuigwa na marais wengine katika bara la Afrika, hii ni pamoja na Tanzania. Ni mpenda maendeleo na ni mzalendo wa kweli.
Rwanda inayo mali asili chache kulinganisha na Tanzania, pia ni nchi ambayo ilikumbana na misukosuko ya kisiasa, lakini pamoja na hayo Rwanda chini ya uongozi bora wa rais wake Kagame wamipiga hatua kubwa kimaendeleo. Yote haya yanatokana na sera nzuri na kupiga marufuku suala la rushwa. Hakuna asiyelielewa hili.
nina uhakika baada ya miaka saba rwanda itakuwa imetupita tanzania kimaendeleo....tanzania tunahitaji viongozi mfano wa kagame,kwa aina ya viongozi tulionao,kasi ya maendeleo itakuwa ni kwa mwendo wa kinyonga hapa tanzania
ReplyDeleteMtoa habari usikurupuke kutoa habari za Uongo hapa! 96% sio matokeo ya mwisho, hayo bado! Shame on you!
ReplyDeleterwanda imetoka vitani na kwa sasa inamaendeleo kuliko tz.
ReplyDeletesehemu yoyote pale rwanda mpaka vijijini unapata connection ya internet wire less free. narudia tena wireless internet connection free nchi nzima. uk, usa, canada, japan australia nakadhalika hawajafikia hatua hiyo.
rwanda imepania na inaamuwa kuwekeza kimaendeleo kwenye sayansi na teknolojia.
rwanda hakuna rushwa kama bongo watu wanawajibika hawa jamaa wako dunia nyingine na hawategemei wachina wezi wanafanya vitu vingi wenyewe sio wabongo hata barabara hatuwezi mpaka wachina.
karakabaho mnaompiga vita kagame.
Oya Msimlaumu Kagame Hata akikaa Miaka mwenyezimungu atayomuweka wacha awe Raisi,
ReplyDeleteMambo yenu ya Demokrasia hata Huko walikoanzisha Demokrasia British hawayawezi marekani Kidogo Ndio wamerekebisha ila Bado. Wanaojuwa Demokrasia Kidogo ni North Korea tu na Iran sababu wapo na Msimamo. Kagame aliyoyafanya si madogo wenzetu wamepiga Kura kwa Amani na Sie tuige. MZ
MDAU wa pili Kaeleweka Mie Maoni yangu Kagame anafaa Kama jamaa alivyosema Kagame akiachiwa Mpinzani ashinde Jeshi linarudi Nchi inaharibika tena. Kuhusu Demokrasia hakuna sababu nchi za Nje ndio zinaweka Kiongozi kama Hawa kukitokea Vita wanawasomesha wanawaweka. James.
ReplyDeleteNdiyo maana Tanzania ipo nyuma ilitakiwa muwe na kiongozi kama Kagame hao wanaosema anakandamiza watu walikuwa wapi wakati wa Genocide? Wadanganyika hamna kitu
ReplyDeleteKweli, huyu jamaa wa ukweli. Tuna viongozi wachache sana Afrika wenye uzalendo. Kwa hali ilivyo hapa kwetu ni bora ukimpata mtu kama huyu hata atawale maisha, kwani wengi wetu tunajali sana maslahi binafsi kuliko maslahi ya nchi zetu.
ReplyDeleteHamna demokrasia huku Wahutu wananyanyaswa. Aidha wengi wao wamefungwa na kuuawa kwa kisingizio cha matukio ya genocide. Nchi hiyo inaongozwa kitutsi na Wahutu walio wengi hawana haki. Usilinganishe na Tanzania bado hakuna chuki za kikabila kwa kiasi hicho.
ReplyDeleteRwanda ni kama mkoa mmoja wa Tanzania and easy to govern.
i fully support kagame,what he has done to his country no one else could,he has completely changed rwanda economically,politically and even socially...as i am speaking now rwanda has real taken a huge step ahead compare to other african countries which got independence long time ago and politically stable such as tanzania...tanzania has been stable politically and independent for over 40 yrs but it has never taken a step ahead over rwanda which has been in civil wars just few yrs ago.
ReplyDeleteKagame safi! binanfsi namm=uuga mkono Kagame,
ReplyDeleteKaipaisha Rwanda sana kimaendeleo, Rwanda kanchi kadogo sana natumewazidi rasilimali kbao,bahari,madini,mito,mbuga, ardhi na hata idadi ya watu(watu wa DSM tu wazidi Rwanda yote) na juzi juzi tu walikuwa vtani..lkn check maendeleo yao wametuacha mbali mno.
Hii ni kwa sababu ya uongozi bora.asikwambie mtu bwana Rwanda ukikamatwa na Rushwa tu..utajuta kuzaliwa..Jamaa anaweza hata kukuua (Hii safi sana, hakuna anayejaribu kushiriki ktk rushwa)
Kagame binafsi, aliisha korofishana na watu wake wa karibu na wengine wasisi wa Rwanda sababu walihusik na rusha ( we acha bwana, huyu jamaa si mchezo).
WaTZ kwa mwendo huu wa kuoneana aibu na kubebana hatutafika popote!! ujinga wetu tunaoupamba kwa majina mazurii hoo tuna "AMANi, UPENDO eti na USTARABU" ..huku wachache wakizidi kulilmkizia mali..huu ni uppuzi kabisa.
Then, mtu akisema...ohhoo , analeta siasa za kashfa.! kashfa wapi ??mbona hela hazijarudi?? tunyamanze wakati bado mnazo na mnazidi kuiba?? kwani ukiakisema wewe ni mwizi nakweli umeiba ni kashfa?? si uende makakmani basi???
TZ tunatakiwa kupata Rais mwenye uchungu wa nchi kama Kagame, Rais atakayechukia nakuipinga Rushwa kwa nguvu zake zote! ndo tupata maendeleo ya kweli (na sio mendeleo ya kisiasa yalijaa kwenye karatasi za hotuba tamu tamu tu).
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU UBARIKI UCHAGUZI UJAO UWE WA HURU NA HAKI!!
ANKAL....LABDA TUSAIDIANE KUPATA TASFIRI SAHIHI YA NINI MAANA YA 'NCHI KUPATA MAENDELEO' INAWEZEKANA TUNAONGEA KITU KIMOJA ILA TUNASHINDWA KUELEWANA KUTOKANA NA MATUMIZI YA TASFIRI TOFAUTI...
ReplyDeleteati anachukia wahutu ni poa tuu mlichinja wenzenu kama kuku! mlitingisha dunia, nyie hamtabiriki ni bora mbanwe hivyo hivyo ruanda ya sasa ni better place
ReplyDeletewewe muandika comment ya Tue Aug 10, 03:33:00 PM usiwe mjinga samahani lakini maana kabla hujaandika ni lazima ufikilie unachoandika laa sivyo utaitwa mjinga kila siku,eti"Rwanda ni kama mkoa mmoja wa Tanzania and easy to govern." Rwanda ina Population: ya watu 10746311 milioni kumi, Zanzibar ina watu milioni moja tu ipi ni rahisi kuongoza? na ipi ina maendeleo? au nipe mkoa mmoja tu unaofanana na Rwanda kimaendeleo, Dar ina watu milioni tatu, nyang'au wee.
ReplyDeletewengi humu mnaongea msiyoyajua.
ReplyDeleteMimi baba mnyarwanda japo alikimbilia tz kwa muda mrefu na kumuoa mama ambaye mtz ila kwa sasa tumerudi rwanda.
KAGAME ameleta maendeleo makubwa sana hapa ameleta amani ametoa chuki na ukabila. Kwakuwa nyinyi mko nje na mnafanya assumptions hata siku moja hamtoweza kuelewa.
Hatuongelea wahutu na watutsi siku izi tunasema wanywarwanda tuachieni na amani yetu na hata kama ataongza miaka 70 ijayo as long as kuko na amani aendelee tu.
tunamumpenda sana KAGAME.
SOLANGE, KIGALI
wee anony hapo juu nani kakwambia kwamba rwanda kuna ukabila tena? ukabila ulikuepo miaka thelathini ilo pita hao viongozi wa zamani ndio waloruhusu kuweka kabila la mtuu ndani ya id yake ilaa huyu jaa alivokomboa nchi na kupiga stopu maauuwaji ya genocide kalipiga stopu pia hilo hamna ukabila sote ni wanyarwanda.hapa niboksi tu kukajenga ka rwanda ketu ka paradizo tumesota miaka kibao na siasa mbovu za wafaransa na hao wabelgiji leo tumesema no war nimaendeleo tu wenye wivu watakula sumu anatakae bisha aje kwa na kelele zake tumpe kibano ambacho hatokisau maishani mwake.jamaa tunampenda jamaa nimpenda maendeleo jama ana uchungu na nchii yake na wanyarwanda wote.eeh mungu endelea kumlinda huyu jama daima amen.western country wanaleta fujo kwetu kwa sababu jamaa hawapigii magoti ka viongozi wengine wa kiafrica wanaopelekeshwa na hao wazungu alaaa.africa inaitaji marais ka kagame thelathini wengine kumi ka kadafi afu uone mandeleo kwenye balaa letu la africa hao jamaa kila kitu wanachukua africa kwetu wananini zaidi yakua wajanja na kutuibia mali asili zetu.miaka saba ijao rwanda ka dubai.ni hayo tu washa nile shampeini maana mzee daah
ReplyDeletemdau kigali makazi boksi kusaka chake
mithupu naomba usiibanie hii kitu
Solange, umeongea kulingana na uwezo wako wa kuelewa, ila jiulize, baba yako alikimbia nini na kwa nini? si vema kurudi nyuma ila ujue wako watu wengi wasio na uwezo wa kusema yaliyo miyoni mwao ila ukweli utabaki palepale kuwa RPF ilivyokuwa wakati wa 1994 haijabadilika hata kidogo! siasa ni siasa tuu! Kagame anajificha katika kivuli cha maendeleo kwa Rwanda ila ukatili na chuki kwa wahutu imezidi mara dufu!
ReplyDeleteSAMAHANI KUONGELEA MTU AMBAYE HATUNA NAYE: MIM NINAONA KAGAME NI SAWA NA MAREHEMU SOKOINE. TANZANIA INGEKUWA MBALI CHINI YA WAZIRI MKUU BWANA SOKOINE. ALIKUWA MTENDA KAZI WA KWELI. JAMANI KUMBUKA ENZI ZAKE. SIYO SASA POROJO TU!!!!!!!
ReplyDeleteNasikia mendeleo yapo lakini huyu baba anamute watu kishenzi...watu walikoswa koswa kuuliwa, wengine wamekutwa wamekufa kwenye maji. Na kuna watu wamelazimishwa kumpigia kura na wanaogopa wasipopiga sehemu zao zikionekana kura ni nogo watasumbuliwa baadaye...
ReplyDeleteHata mimi sielewe miaka yote hiyo nchini ni democracy ya wapi? Hata kama aliweza kuwasaidia kuitengeneza basi wachia na wengine waendelee