Msimamizi wa Uchaguzi wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania,Yustus Mkinga (katikati) ambaye pia Ni Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA,akitazama ubao wenye majina ya wagombea wa nafasi ya Rais wa Shirikisho la Wanamuziki Tanzania.Kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego na Rashid Masimbi,Mjumbe wa Bodi BASATA (kushoto).Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA),Kassim Mapili akijinadi mbele ya wanachama kwa ajili ya kuomba nafasi ya Makamu wa Rais wa shirikisho.Mkongwe wa Muziki wa Reggae,Ras Inno Nganywangwa ambaye aliwakilisha chama cha Tanzania Urban Music Association (TUMA) akimwaga sera zake wakati akiomba nafasi ya Katibu Mkuu wa shirikisho.
Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego akitaja majina ya viongozi waliochaguliwa kuliongoza shirikisho kwa muda wa mpito wa mwaka mmoja.
Viongozi wote waliochaguliwa wakiwa kwenye picha ya pamoja na msimamizi wa uchaguzi Bw.Yustus Mkinga (mwenye mwenye suti).

Na Alistide Kwizela.

Hatimaye Shirikisho la Wanamuziki Tanzania leo (Jumatano) limepata viongozi wake wa muda katika uchaguzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa BASATA na kusimamiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA,Bw.Yunus Mkinga.

Katika uchaguzi huo uliokuwa wa vuta ni kuvuta,Bw.Ibra Washokera aliweza kuibuka kidedea kwenye nafasi ya urais baada ya kupata kura 12 na kumbwaga Mkongwe wa muziki wa dansi,Hamza Kalala ‘Komandoo’ aliyeambulia kura 2 tu.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu wa Rais,Mwanamuziki wa muziki wa asili,Che Mundugwao aliibuka kidedea kwa kupata kura 9 na kuwaacha mbali wapinzani wake ambao ni Mkongwe Kassim Mapili na Gwalugano Ayoub walioambulia kura 3 kila mmoja.

Nafasi ya Katibu ilichukuliwa na Salum Mwinyi huku nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Mipango ikikamatiwa na Samwel Semkuto.Aidha, wajumbe waliochaguliwa ni Samatha Rajab, Said Mukandara na George Mbata.

Wakiongea kwa kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi, Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego,Bw.Yustus Mkinga na Mlezi wa Mashirikisho ya wasanii,Mzee Rashid Masimbi walisema kwamba, kazi iliyopo mbele ni kwa viongozi hao kupanga mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuwaendeleza wasanii na kupigania maslahi yao.

Aidha, walisisitiza kwamba, kwa sasa wasanii wa muziki wanatakiwa kusimama imara chini ya shirikisho lao na kuwa na msimamo thabiti katika masuala mbalimbali yanayowahusu.

Kesho itakuwa ni zamu ya uchaguzi wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi na keshokutwa ni shirikisho la Sanaa Jongevu (Filamu),Wadau wote mnakaribishwa kwenye chaguzi hizo ambazo ni maendeleo makubwa kwa wasanii na sekta ya sanaa kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HAYA MASHIRIKISHO HAYANA MAJINA? TUDOKEZEE YANAITWAJE.

    ReplyDelete
  2. MAMBOOOOOOOOOOOZZZZZZZZ ANKAL

    ReplyDelete
  3. Naona kama mavyama mengi yenye itikadi moja. Ndio yanaongeza bureaucracy au conflict of interest kwa wasanii tu haya na watu wengine kujiengezea titles

    BASATA
    Cosoto
    CHAMUDA
    TUMA
    Shirikisho la Wanamuziki Tanzania
    Shirikisho la Sanaa za Ufundi
    shirikisho la Sanaa Jongevu
    Mashirikisho ya wasanii


    Aghhhrrr I could go on and on....

    ReplyDelete
  4. Mbona Ras kanyimwa kura jamani?

    ReplyDelete
  5. Ras ana nyuki kichwani, nani ampe kura!

    ReplyDelete
  6. Mbona wakongwe wenye heshima kubwa ktk muziki wa dansi hapa nchini hakuna hata mmoja? Au uongozi huu hauna mlo kama ulivyo ubunge!!!

    ReplyDelete
  7. JAMANI WANAMUZIKI TANZANIA WANAZIDI KUNYIMWA HAKI ZAO,TOKA ENZI YA RTD MPAKA LEO...TUNGO ZAO NI KAMA NDEGE AIMBAVYO JUU YA MTI...HAKUNA MANUFAA YOYOTE ILE(Cosmas Chidumule in Bongo Beats Films).TUNAOMBA SERIKALI IFWATILIE SWALA HILI,HAKI ZAO ZINAPITIA KATIKA MIFUKO YA WENYE RADIO,BASATA NA VYAMA KAMA HIVYO...MUZIKI WA DANSI UNAZIMWA NA HAO MAFISADI WENYE KUMILIKI VYOMBO VYA HABARI.

    ReplyDelete
  8. KWELI JAMANI KILA SIKU VYAMA VINAAVYOHUSIANA NA MUZIKI AU SANAA VINAANZISHWA,NA HIVI NDIVYO JINSI URASIMU NA USUMBUFU UNAVYOZIDI NA PIA UGUMU WA WASANII KUFUATILIA HAKI ZAO UNAVYOZIDI,WATU KAMA HUYO BWANA MKINGA KILA SIKU YUPO TU KWENYE MAMBO YA SANAA NA YEYE HAJUI LOLOTE KWENYE SANAA,NA NDIYE ANAYEENDELEZA UFISADI NA RUSHWA KISHIRIKIANA NA WAHINDI KUNYONYA JASHO LA WASANII,KWA NINI MTU HUYU ASIONDOLEWE,JE?AKINA BITCHUKA,NGURUMO,KALALA,ALI JAMWAKA MKO WAPI?ONDOENI MADIKTETA
    KATIKA FANI HII YA SANAA NDIPO MTAFANIKIWA LA SIVYO MTAZIDI KUNYANYSWA NA WAHINDI NA WATU KAMA HUYO MKINGA,FISADI MKUBWA,MIMI NI MSANII NILIYEWAHI KUNYANYASWA NA COSOTA,MUNGU IBARIKI BONGO.
    MIKOCHENI,dar.

    ReplyDelete
  9. kila siku vyama vipya vihusuvyo mambo ya usanii na muziki,maendeleo kwa wasanii hakuna
    wanaohusika kwenye uongozi siyo wasanii na wala hawajui sanaa ni nini,je<jamani watu kama akina Mwidini Ngurumo,akina Saidi Mabela,Ali Choki,Shabani Dede na wengineo mko wapi siku zote hizi?hawa akina Mkinga hatuwataki maana hawa ndio mafisadi wanaosaidiana na wahindi kudhuluimu haki zenu angalieni sana ndugu zangu mtabaki masikini milele ka tabia za kutojitokeza na kudai haki zenu au kwa sababu ya kukosa elimu?hiyo Cosota kwanza ingefutwa kabisa na huyo bw.Mkinga aondolewe kwani huyo ndicho chanzo cha matatizo,wasanii tukienda kwenye ofisi yake kutaka msaada wake huwa siku zote hayupo ofisini sijui ofisi hii ilikodishwa kwa nini??tunaomba dikteta huyu Mkinga atolewe mara moja.
    msanii mwenye usongo ns Cosota
    Dar.

    ReplyDelete
  10. Cosota ifutwe maana haina faida ni unyanyasaji tu wa wasanii,vyama vimekuwa vingi na maendeleo kwenye sanaa hakuna,wasanii wanazidi kuwa maskini tu,cosota plus Mkinga Out !!to hell with Ufisadi 1!!
    mdau bongo fleva
    Dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...