Familia Ya Bwana Khalfani Abdullah Elmaamir wa Netherfield, Milton Keynes, Uk, inapenda kuchukua fursa kutoa shukrani za dhati Kwa wote ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki kwa hali na mali kuifariji familia katika kipindi kigumu cha msiba wa mtoto wake "Hilaly Abdullah Elmaamir" (umri miaka 8) aliyefariki Dunia alfajiri ya 09.08.10 akiwa likizoni Dar es salaam, Tanzania.
Mjomba wa marehemu Bwana Diego mbegu Kwa niaba ya Familia ya mama mzazi (Bi Rehema wa Milton) pia anawashukuru ndugu na marafiki wote waishio Uingereza kwa kukamilisha michango kwa ajili ya nauli za kuwasafirisha Baba wa marehemu Khalfani Elmaamir na untie Bi Khanifa waliondoka jana 10.08.10 kuelekea msibani Tanzania. "Hatuna cha kuwalipa zaidi ya ahsante na tuzidi kushikamana,
Assalam aleykum wa Ramadhani Kareem".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...