Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama akikata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Tawi jipya la huduma kwa wateja la kampuni ya simu za mkononi la Tigo lililofunguliwa leo mtaa wa msimbazi na Pemba. Kushoto kwake anaeshuhudia ni Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez . wakati wa ufunguzi wa tawi hilo jipya mtaa wa kariakoo pia Tigo ilitangaza kufungwa rasmi kwa promosheni yao iliyoendeshwa kwa miezi mitatu ya JIKOKI na Tigo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw Leonidas .T. Gama akipokea zawadi kifurushi cha huduma zinazotolewa na Tigotoka kwa mmoja wa Afisa wa Tigo huduma kwa wateja Beatrice Kinabo ikiwa ni maalum kwa kumpongeza mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi Rasmi wa Tawi jipya la huduma kwa wateja la kampuni ya simu za mkononi Tigo lililofunguliwa leo mtaa wa msimabazi na Pemba. Kushoto mwa Beatrice ni Afisa Muendeshaji Mkuu Biashara na Masoko bwana Diego Gutiérrez.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Duh!... Mkuu wa wilaya huyo... miye yangu macho tuu

    ReplyDelete
  2. assalaam alaikum, napenda nifahamu kwamba iwapo mnatangazo la Vodacom haitokuwa tatizo kwa stori ya tigo

    ReplyDelete
  3. si tatizo kwa kutangaza kampuni mbili za simu, kwa sababu huwa wanajifanya namna gani kwa kuwamiliki wanaowapoa matangazo

    ReplyDelete
  4. hivi ni macho yangu au,mbona huyo beatrice kinabo simuoni...

    ReplyDelete
  5. hata mie nashanga! kumbe kuna beatrice wa kiume nowadays!

    ReplyDelete
  6. Nyinyi ma-anonys mnayemuuliza Beatrice vipi nyinyi? Hamuoni kama Beatrice kazibwa na TUMBO la mkuu wa wilaya, mzee L Gama. Damn, jamaa ana tumbo kitu. Dah, naona anahitaji Diet ya nguvu saaaana.

    ReplyDelete
  7. Sasa unafungaje promotion bila kutangaza mshindi, au ndio wameliwa maana walisema watamtangaza mshindi mwisho wa promotion, afu kama vipi hawa watu wa vituo vya habari wanote mwisho wa hizi promotion, maana nimesikia clouds leo kupitia Leo tena watangazaji wote wanasisitiza watu waendelee kushiriki
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...