Waziri wa Sayansi na Tek nolojia Prof. Peter Msolla akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni ishirini Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.

Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufuatia Taasisi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kushika nafasi ya kwanza leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti mwaka 2010.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akiangalia mbegu za mahindi na kupata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kilimo Kutoka kituo cha utafiti Ilonga kilichoko kilosa mkoani Morogoro Dkt. Chaboba Mkangwa. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Hassan Mshindi.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Bw. Godfrey Kimarya mgunduzi wa tanuru la mkaa lenye uwezo wa kutoa mkaa mwingi na wenye ubora kwa gharama nafuu leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini.Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine -Morogoro (SUA) Prof. Rhodes Makundi (kulia) na Christophe Cox (kushoto) wakitoa maelezo ya panya buku wenye uwezo kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) leo jijini Dar es salaam wakati sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini .Profesa Rhodes Makundi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - Morogoro (SUA) akitoa ufafanuzi wa panya buku wenye uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla leo jijini Dar es salaam wakati wa sherehe ya kutoa tuzo za taifa za ugunduzi na ubunifu na kutoa Mwega kwa ajili ya utafiti

(Picha na Aron Msigwa )

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. kweli swaumu imebamba, huyo mzungu ndo prof makundi??!

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kwa wataalamu wetu.

    WADAU VIPI MICHUZI AKIWEKA MAMBO YA ELIMU NA TECHNOLOGIA HUWA UNASHIKWA KIGUGUMIZI

    J BURA

    ReplyDelete
  3. Mdau anon wa Mon Aug 16, 05:53:00 PM

    Sasa sisi panya buku wa kufukua mabomu wanatusaidia nini?

    Ndio maana unaona kimya. Wangefanya utafiti wa kuongeza nguvu za kiume uone micomment itakavyojaa.

    ReplyDelete
  4. KATIKA FANI YA UANDISHI WA HABARI/PICHA, MARA NYINGI PICHA HUTAMBULIWA KUTOKANA NA "PESPECTIVE" YA MSOMAJI/MTAZAMAJI!

    HAPO JUU, YAANI, KULIA NA KUSHOTO YAKO (WEWE MSOMAJI/MTAZAMAJI)!

    ReplyDelete
  5. Hilo Tanuru naona sisi tumechelewa. Mimi naishi Italy na ukitembelea sehemu za ndani ndani kwa wenyeji wao wanaokea mikate kama hilo long time tu...

    ReplyDelete
  6. anon wa 'PERSPECTIVE' pole kwa swaumu!

    ReplyDelete
  7. mimi naomba kuuliza swali nchi yetu nasikia kuna wana sayansi na ma engineering !! hila sijawahi kuona au sikia lolote walilo gundua ambacho kikasaidia jamii yetu ya kitanzania sasa panya buru wa kuchimbua ma bomu wa nini ? tutakula hayo ma bomu sisi ama?

    ReplyDelete
  8. Wagunduzi na wabunifu si lazima watoke kwenye taasisi , hapo ndipio tunasema ni kupeana? hao chuo kikuu kwenye computer wamevumbua nini ..kama si kuongezeabna umaarufu na kula... Kuna vijana wadogo na ambao hawana elimu ila wana uvumvuzi lakini serikali kupitia taafisis yake ya uvumbuzi na ugunduzi inawapuuza ..badala ya kuwaendeleza.. igeni na angalieni mifano ya nchi kama marekani zinaangali vipawa hivyo tangu wakiwa wadodo...na kuhamasisha wazazi kuvigundua na mashuleni.. ndiyo maana tunaishia kuiga na kufuata mkia.. hakuna mpya.. paanya, Computa.. matanuru vyote hivyo si vipya na kwa nchi za wenzetu wamevumbua upepo wanatengeneza umeme uwasaidie wananchi kupunguza gharama za umeme .....Tatizo letu ni wavivu wa kufikiri na hiyo wizara ya sayansi na tecknologia ..hawajua maana ya wizara hiyo ..wanahisi tu katika utendaji kazi wao..Tunataka uvumbuzi na ugunduzi kwa manufaa ya Jamii kwa ujumla...

    ReplyDelete
  9. nchi yetu haiko katika vita, ingependeza zaidi hao panya wapelekwe hukoo iraq na afghanistani, yale mabomu ya mbagaraaaaa llikuwa bahati mabaya tuu!

    ReplyDelete
  10. tatizo letu watanzania lilelile hatupendi kuelewa mambo kwa undani wake..tunacomment tu bilka kufikiria! kiama jambo hulielewi kaa kimya! umeambiwa hao panya mbali na kwamba wanaweza kutegua mabomu pia wanaweza kugundua vimelea vya TB, hiyo inamaana mahali kwenye magonjwa ya milipuko kama tauni au TB unaweza kuwatumia kugundua mahali vinapoanzia au kuzaliana na hivyo kuzuia mfumuko wa ugonjwa, nimefuatilia kuhusu huyo profesa makundi nikagundua ndio alihusika kuuzima kwa sehemu kubwa ugonjwa wa tauni kule Lushoto Tanga mid 90's. Nadhaniswala nikupata watu kama yeye kwenye field mbalimbali nyingine lakini sio kublame ugunduzi wake, jiulize wewe umefanya nini so far!

    ReplyDelete
  11. Mtoa Maoni: Anonymous - Tarehe Mon Aug 16, 09:01:00 PM, nimekusoma, asante sana!

    Swaumu kwangu mwiko! (CHEKA)!

    ReplyDelete
  12. Hao panya buku wamenona kweli. Wasije wakageuka kitoweo cha watu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...