Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare akizungumza katika hafla ya kufturisha iliyoandaliwa na kampuni yake hivi karibuni katika viwanja vya karemjee jijini Dar.
Sheikh Mkuu wa Tanzania,Muft Shaaban Simba akipokea vitabu vya Quraan kutoka kwa Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare.kulia ni Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Mwamvita Makamba na katikati ni Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Mussa Salum
Watoto waliofika katika hafla ya kuftarisha iliyoandaliwa na kampuni ya Vodacom kupitia mfuko wake wa Vodacom Foundation.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watoto pamoja na walezi wao mara baada ya kufturu.


Na Mwandishi Wetu


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation umetenga zaidi ya milioni 40/- katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ili kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo vya yatima na wale wanaoishi katika shule za bweni.

Msaada huo unaotolewa kupitia kampeni ya ‘Share and Care’ utawalenga watoto kutoka mikoa minne ambayo ni Dar es Salaam, Tanga, Pemba na Unguja na vifaa kama mchele, unga, mafuta ya kula, madaftari na maharage vitatolewa kama futari kwa watoto hao wanaohitaji upendo hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kufutari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare alisema kwa kutambua umuhimu wa jamii inayofanya nayo biashara kampuni yake imeona irudishe kiasi cha faida wanayoipata kwa wananchi ili kiwasaidie.

Akifafanua alisema kwamba tangu mfuko huo uanzishwe miaka minne iliyopita umeweza kusaidia jamii mbalimbali ya Watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani kwa mara ya tatu sasa hususani katika nyanja za elimu, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wale wanaosoma katika shule za bweni na kukosa huduma za chakula.

“Kwa mwaka huu kupitia kampeni yetu ya ‘Share and Care’ tutarudisha tulichokipata na tutaweza kuwafikia watoto zaidi ya 3,000 wa mikoa ya Tanga, Pemba, Unguja na kwa kuanzia tayari tumetoa msaada wa takribani milioni 18/- kwa baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye vituo vya watoto yatima na kutoka shule za bweni mkoani Dar es Salaam,” alisema Mare.

Naye Sheikh mkuu wa Tanzania Mufti Shaban Bin Simba ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo kutoa futari isiyozoeleka majumbani pia imetoa fursa kwa waislamu kutoka maeneo mbalimbali kukutana katika kumi la kwanza na kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Aidha Mufti Simba licha ya kuishukuru kampuni ya Vodacom Tanzania kwa misaada iliyotoa kwa jamii ya waislamu alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe mkono na kuigwa na kampuni zingine nchini.

“Kupitia kampeni hii ya ‘Share and Care’ mliyoianzisha ili kuisaidia jamii ya waislamu katika kipindi hiki cha mfungo natumaini kampuni zingine zitapata fursa ya kujifunza kutoka kwenu,” alisema.

Tofauti na hayo Sheikh mkuu alitoa rai kwa Vodacom Tanzania kuwa kitendo hicho kizidi kuitia moyo kampuni hiyo na kutumia changamoto waliyoipata kurekebisha kwenye mapungufu na kuboresha zaidi katika mafanikio waliyofikia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Yule pale mwene kibagalashia siyo Maharage Chande yule?!!...duh jamaa kwa ubwabwa! Just Kidding Bro...LOL

    ReplyDelete
  2. Well done Vodacom. Other organizations should emulate this deed.

    ReplyDelete
  3. swali:vodacom mnatoa izi milions kwa dini zingine pia ktk sherehe zao?
    au ni kampeni ya kusaidia waislamu tu?

    tafadhali

    ReplyDelete
  4. BIASHARA UJANJA, MZUNGU HADI ANAVAA KANZU, MARKETING!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. KITABU KITUKUFU CHA MWENYEEZI MUNGU
    LA YAMMASSUHU ILLA LMUTWATWAHIRIIN

    HAPA HII INAKAAJE MBELE YAKO MUFTI?

    SHEIKH MKUU SIMBA NA SHEIKH HADI MUSSA TUELEZENI NINI FATWA YAKE?

    MURIDI

    ReplyDelete
  6. Allah anasema kuran haitakiwi kushikwa na asiyekua tohara, jee huyu mkurugenzi yuko tohara? wenye kuijua kuran tusaidieni hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...