

Baada ya jina la Frederick Mwakalebela kuenguliwa katika orodha ya wagombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, baadhi ya watu wamekuwa wakihoji uhalali wa kufanya hivyo ilhali wana-CCM wengine wanaogombea viti hivyo katika majimbo mengine nchini wana kesi mahakamani lakini wameruhusiwa kuendelea na kinyang'anyiro hicho. Maswali hayo yaliifikia CCM na ufafanuzi wake unapatikana Michuzi Post...
Alipoulizwa kwa nini Mbunge wa Bariadi Mashariki Andrew Chenge na Bazil Mramba wa Rombo, wamepitishwa kutetea nafasi zao wakati wanakabiliwa na kesi za matumizi mabaya ya madaraka kama ilivyo kwa Mwakalebela aliyedaiwa kutoa rushwa, Chiligati alisema wamezingatia maoni ya wanasheria kuwa kesi zao haziwezi kuathiri uteuzi wao.
ReplyDelete“Chenge bado anatuhuma na hajafunguliwa kesi, Mramba ana kesi ya matumizi mabaya ya madaraka, nayo haiwezi kuathiri uteuzi wake. Mwakalebela ndio kwanza anaanza na rafu na kapigiwa filimbi ndani ya dakika ya kwanza, hapo tumeangalia maadili zaidi,” alisema Chiligati.
*******************Jamani ufafanuzi hapo juu ni wakujichanganya sana. Yaani unasema Mramba na Chenge hawana kesi bali wameshtakiwa tuu? Chiligati umekosea. Mwakalebela hana kesi ndio kwanza ana tuhuma tu hajafikishwa mahakani. Usitake kutufanya hatuna akili. Ukweli ni kuwa wanaangalia nafasi ya CCM kushinda na hawana watu wengine wa kuwasimamisha kwenye majimbo hayo. Ila hii ni tabia gani ya woga namna hii? Je tunapeleka ujumbe gani kwenye mapammbano dhiti ya Rushwa? Kuachia majimbo mawili tu kuna ubaya gani? (ingawa siamini CCM inaweza kukosa mtu mwingine kumsimamisha kwenye haya Majimbo kupata ushindi) Hii ni messge mbaya sana iliyotolewa na CCM. Tuache siasa za uoga na tufuate maadili na uongozi bora. Tuache kujihusisha na Viongozi wabovu kwa kuhofia tutashindwa
Ndugu zangu! Naona waandishi mtufanyie utafiti wa msemo huu: "Daima Inzi uawa kwa Rungu!". Kumbe kuna mzani wa maadili. Tunaomba waandishi mtufanyie utafiti wa Maadili ya Wajumbe wa NEC; pia tunaomba zaidi Maadili ya MWAKALABELA; BASIL MRAMBA & CHEGE: Tuone uzito wa utovu wa Maadili; Kesi ya kuua- Manslaughter, pia Kudidimiza Uchumi wa Taifa kwa kulaba dume na mshiko wa kununua Rada kwa gharama za kujenga shule za Msingi 1000 na kulipa mishahara ya walimu wake Miaka saba hvi. Chege hata Bugne la uingereza linajua wazi kuwa ananuka Rushwa... na wengi wa aina hivyo Rostam Aziz, Lwasa na wengine! Maadili kwa CCM ni Kinyago (Mask) ya kuvaa kucheza ngoma fulani....
ReplyDeleteJamani tilikwishawaambieni na hamtaki kusikia kwamba CCM ni wafugaji wakubwa wa UFISADI. Sijui hata kama wanajua maana ya ufisadi. ninawashangaa watu tena wasomi wanaojiita wapambanaji kama Mwakalebela, kwanza kabisa, hata kujiwa na wazo la kugombea kwa tiketi ya CCM. Ninafikiri hilo panga ni haki yake (liwe fundisho kwa watu wengine), na pili Mwenyezi Mungu anatusaidia kuendelea kuifanya CCM kutuonesha rangi zake halisi!!
ReplyDeleteSababu mbona zipo wazi. Kuna kitu kinaitwa kuwa "mwenzetu". Mwakalebela hana sifa hiyo.
ReplyDeletevijisenti na pesambili wapiga chenga. Tumemwagiwa changa la macho na Chiligati. du hii kaya yetu ina mambo! kweli ccm mmechemsha. Huenda watashinda lakini huu si uadilifu aliousimamia Mwalimu Nyerere. Ukiibania hii Michuzi nawe utakuwa mmoja wao kwani unazibana nyingi na sijui kwa nini unafanya hivyo.
ReplyDeleteHii kali "Mramba ana kesi ya matumizi mabaya ya madaraka"...sasa kama ana kesi ya matumizi mabaya ya madaraka kwanini umpe tena hayo madaraka?
ReplyDeleteWabongo changamkeni mtumie kura zenu kwa akili...I wish ningekua home at this time....Hawana hata aibu..
Yaani watanzania amkeni jamani huu ni ujinga..Jibu gani hilo hata mtoto wa miaka minne atajua unamdanganya....amakeni amkeni,....
ReplyDeleteNi uhuni tu. Msome Jenerali kwenye Raia Mwema ya wiki iliyopita na The East African ya wiki hii. Ni uhuni tu.
ReplyDeleteMichuzi unajua nilikuwa nakuheshimu kwa kiasi fulani kuhusu taaluma yako ya uandishi lakini baada yatokuwa mkweli na kuendeleza unafiki wako na kutoku-post maoni yangu kwasababu unajua ninaongea ukweli nimeona tu ni kwambie ukweli zaidi kwasababu hata kama hutaki kupost maoni yangu lakini utakuwa unayasoma. Naomba usiwe unatuandikia ujinga kama huu ulidai ndio ufafanuzi wa CCM. Upuuzi kama huu kaanao wewe mwenye na wajinga wenzako ndani ya chama.CCM tunajua kabisa ni chama cha watu wachache na kinazidi kuonyesha jinsi kinavyoendeshwa kidikteta. Swala la kugombea au kutokugombea kwasababu ya kesi au rushwa hio ni kazi ya mahakama lakini kwasababu kamati kuu iko juu ya sheria na wao ndio mahakama,polisi na watunga sheria basi hakuna jinsi lakini narudia tena ujinga huu siku zake zinahesabika utafikia kikoma hatuwezi kupotezea muda wa kupiga kura alafu kura zetu zote zinakukuwa hazina maana yoyote. Enough is Enough.
ReplyDeletekwa kweli mie sijajua hii nchi yetu inaenda wapi!!!mie nilijua kabisa chenge na maramba hawatoweza tena kushiriki ktk uchaguzi wa juu kwenye serekali...Mwenyenzi mungu tusaidie nchi yetu isiende pabaya na mungu ibariki tanzania...mhhhhhhhhh jamani chenge na mramba kabisa???????haya sawa bwana.
ReplyDeleteMalafyala, Ntwa, Kikolo gwa kukaja Lugano Mwakalebela achana na hayo Masisiemu nenda kwingine hapo unapoteza muda. Mbega hana lolote zaidi ya kumbeba tu pia kumbuka alichofanya alipokuwa wizara ya fwedha lakini bado wanamrudisha. Wapinzani jipangeni kunyakua hilo jimbo. Wapinzani oyeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteSuala liko straightforward. Halihitaji mtu uwe mwanasheria wala nini. Wote watatu (Chenge, Mramba na Mwakalebela) ni watuhumiwa. Tuhuma zao zote (rushwa na kutumia madaraka vibaya) zinahusu maadili. Tusidanganywe kama watoto kama vile kuna watu wanaweza kuelewa mambo yaliyo wazi zaidi yetu na kutudanganya kwa maneneo. Wameanzisha neno jipya kwenye huu uchaguzi, wanasema "rafu" kama vile ni kosa tofauti au distinct kulinganisha na mengine ya kimaadili. Hivi watanzania tutadanganywa hadi lini na watu wachache tu?!
ReplyDeleteKumbukeni kuwa Chenge na Mramba ni wa siku nyingi na wanawashikaji ndani ya NEC.
ReplyDeleteKinanichonishangaza nyie mnapiga kelele za nini? WAACHIENI WAPIGA KURA WAO HUKO MAJIMBONI MWAO NDIO WATAKAOFANYA UAMUZI WA MWISHO.
HAPO watu wametumia uamuzi wa busara zaidi, waacheni waende wakatemwe majimboni mwao lakini sisi tunazuia mpasuko ulioanza kujitokeza ndani ya Chama. Kama watu wa Iringa mjini hawamtaki Monica Mbega, wana haki ya kutoa uamuzi huo siku ya uchaguzi, kama mtu hatakiwi hata akiuzwa vipi hanunuliki. Na kama wapiga kura wa Rombo na kwingineko hawamtaki Pesambili, basi wao ndio wenye uamuzi wa mwisho. Na nyie nendeni mkatumia haki yenu ya kikatiba kupiga kura, kupiga makelele humu ndani hakusaidii kitu.
Cha ajabu mnataka upinzani ushinde at the same time mnalalamikia rafu za ccm inahuu? Si ndio mngefurahia sasa angalau badala ya viti 10 bungeni mwaka huu demokrasia itaimarika kwa wapinzani kupata viti vingi zaidi bungeni?
Jamani nachaneni na haya mambo ya siasa, hayo maziwa mabovu yaliyoingia hapo ni muhimu kuliko huyo mwakabelela, Ingekua ni CHINA hapo mtu angenyongwa hasa huyo mkurugenzi wa TBS na TRA. Kila siku nikisoma habari hapa kwenye blog ni changuzi tu kila cku, mara wa wamiss, mara michezo mara chama cha hili na lile, lakini cjaona hata umuhimu wa kuwa na hata viongozi maana hawana manufaa yoyote huko kwetu.
ReplyDeleteHuyo anayesema alikuwa anaekuheshim halafu ameamua kukutukana nadhani upeo wake wa mambo mdogo,mimi nadhani alitakiwa kueleza hoja siyo kumtukana Michuzi,kwa kawaida ukiona mtu anamshmbulia mtu badala ya hoja aliyoitoa lazima ana matatizo,achana naye wala asikusumbue nadhani ameonyesha ni kiasi gani alivyo na upeo mdogo wa mambo,chambua hoja siyo kumtukana
ReplyDeleteHAYA sasa, hicho ndicho chama kinachosema MAISHA BORA KWA KILA MATANZANIA.
ReplyDelete-Wananchi wamechagua watu wao wa kuwatetea, nyie chama mnawatoa
-Baadhi ya viongozi wenu washaonekana sio waadilifu, mnasema haingiliani na mambo ya uchaguzi( manakumbuka stori ya Mwl.Nyerere na mke wa mfalme)?
-Ni Serikali ya chama hikihiki ambayo imeminya uwezekano wa kuwepo mgombea binafsi.
-Ni serikali hii hii, iliyokataa kuongeza walimu mishahara, lakini ikaongeza marupurupu ya wabunge
-NI serikali hiihii, imekataa kuongeza mishahara ya wafanyakazi lakini ikanunua magari mapya ya raisi yanayochomoka matairi barabarani kwa gharama kubwa.
HAYA SASA AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YAKO
Na We' Mwakalebela kilichokupeleka CCM Iringa ni nini? kwani pale TFF sio ulikuwa unakula kiulaini tu jamani? Kwani pale TFF palikuwa na tatizo gani? Sasa itakuwaje, utarudi tena TFF? Achana na CCM, Ukifanya mchezo watakumaliza hao, shauri yako!!!!
ReplyDeleteWALAU LEO MICHUZI HAKUNA HABARI ZA CHADEMA MAANA ILIKUWA TOO MUCH
ReplyDeleteWe mwana wee karibu huku kwetu tukupe shavuu....
ReplyDeletehawa huweai mwanaaa.wanajua haoo..wezi watupu haoooo mwana njoo weeeee!
DK SLAAA Oyeeeeee!!
Hii inatokana na uelewa wa watu wa mjimbo wanakotoka akina Mramba na wenzake. Kama watu wao wameona wanawafaa its ok, labda kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, ilikuwa kwa faida ya watu wa jimbo lake. Na chenge vile vile, kama ile rushwa anayotuhumiwa nayo pesa zilitumika kusaidia watu wa jimbo lake sawa. Vinginevyo hata watu wao ni mbumbumbu.
ReplyDeleteWatizii wagumu sana kuelewa mambo! Hapa kuna cha kushangaa??
ReplyDeleteAngalia "integrity" ya wajumbe wa kamati ya maadili ya CC ndio hutashangaa na haya yanayoendelea.
Chama kilipokuwa cha wakulima na wafanyakazi haya yasingetokea.
mambo yamebadilika, hakuna cha kushangaa!!
Ivi ishu inayomkabili Mwakalebela na Margreth Simwanza Sitta inatofauti gani? wote si walikamawa na TAKUKURU? au ndio mambo wa mwenzetu na Mwakalebela si mwenzao?ebwana duh
ReplyDeleteUpuuzi mtupu! Watu wametoa rushwa nje nje Mtwara, lakini hakuna kilichofanywa! Uhuni mtupu. Hii nchi inaongozwa na wafanyabiashara wachache wenye fedha. Kama hamna demokrasia ndani ya chama, kweli itakuwepo nchi zima?
ReplyDeleteHii ndo Tanzania kama ulikuwa hujui.
ReplyDeleteSasa ndo tutajua akili ya watanzania iko je?
Sitokaa nimpigie mtu yeyote kura. Kura niliyompgia Mkapa mara ya kwanza inatosha.
Mdau. Singida
Guys I hate to say this but remember Jakaya ni mwanajeshi na chama kinaendeshwa kijeshi,Mwenyekiti ni Luteni kanali Jakaya mrisho kikwete,katibu ni Luteni Yusuf makamba,katibu mwenezi ni kapteni John Chiligati so in the mind if democracy failed to bring them to power they know what to do in order to stay there,therefore get ready for the bullet in the head.
ReplyDeleteMdau Chalinze.
CHILIGATI AMEDANGANYA, HAKUNA MWANASHERIA ANAYEWEZA KUTOA USHAURI KAMA HUO. CHILIGATI AMEVUNJA MAADILI,AMESEMA UONGO NA KAMA KWELI BASI AMTAJE NI MWANASHERIA GANI ALIYETOA USHAURI HUO. CHILIGATI AMOMBE RADHI JAMII YA WATANZANIA NA WANASHERIA KWA KUTUMIA WANASHERIA KUFANIKISHA MCHEZO MCHAFU WA CCM.WANASHERIA WAMEONEKANA BOGUS. SIMAMENI MUMKEMEE, AMEWADHALILISHA.
ReplyDeletemichuzi bin mitori, chonde chonde meseji zote lizobana zimwage hewani ukishafuturu, manake umeachachamaa kubana duu,
ReplyDeleteKwa maneno ya Mkuchika, ina maana kuwa CCM wameishaamua kuwa Mramba na Chenge wameshinda kesi!!!!!!!
ReplyDeleteWATU WENGI MNA CHUKI SANA. MSIWA JUDGU WATU KABLA KESI HAZIJAISHA. HASIRA NYINGI NA MAKELELE MENGI WAKATI HAMJUI HAO WATU KAMA WAKO GUILTY. ANYWAY KOSA LA KUTUMIA MADARAKA VIBAYA SIO MTU AMEIBA. I DON'T KNOW HATA NI KWANINI HAO WATU WALIPELEKWA KOTINI. BY THE WAY MSIFIKIRI CCM NI WAJINGA, WAMEKWISHA JUA NI NANI ATASHINDA UCHAGUZI NDIO SABABU WAKAWACHAGUA. PLEASE DON'T EVEN THINK WAPINZANI WATASHINDA. WAPINZANI NI WATU WACHACHE KAMA NYIE AMBAO MNAWEZA KUTUMIA COMPUTER. MAJORITY OF PEOPLE WHO WILL VOTE WANATOKA VIJINI NA HAO NDIO WILL VOTE FOR CCM. BADALA YA KUZUNGUMZA MNATAKA SERIKALI IJAYO IWAFANYIE NINI MNA JIGARAGARA CHINI MKIPIGA KELELE JUU YA UFISADI AS IF THAT WILL SOLVE TANZANIAN PROBLEMS. HIYO NI WATER UNDER THE BRIDGE.
ReplyDeletemwakalebela nae bwana, we utaagaje kabisa ofisi kwa mbwembwe. usingeacha kwanza kazi khaaaa. yaani ulijiaminisha asilimia 100 yaani hujuagi mizengwe iko kila mahali? kwani tff watu wote unafikiri walikua wanakupenda? basi ni hivyo2 upande wa 2 ebo. enewe pole baba, rudi tena tff wastaarabu watakusikiliza na uachane na siasa.
ReplyDelete......tehe tehe tehee, maneno kuntu babu! CCM inawenyewe na wenyewe nisisi, huyu ni mwenzetu na huyu si mwenzetu....upo hapo? we unagombea bila kuwa kwenye kambi ya LOWASA ua RIDHIWANI au SUMAYE unategemea nini? utapigwa Chini TUU! sasa mzee kuna biashara ya kufanya?
ReplyDelete