Balozi Mpya wa Tanzania nchini Uingereza Mh Peter Kallaghe aliwaalika Watanzania na kuftari pamoja nyumbani kwake jumamosi tarehe 04.09.10. Baada ya kuftari Mh Kallaghe alijitambulisha na kuwashukuru Watanzania wote waliofika nyumbani kwake. Pia aliahidi kuwa karibu na Watanzania.
-Na Urban Pulse Creative

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. London inawaka waka. Wivu sina ila roho inauma! Hongera Balozi na mama Balozi. Hongera wananchi wa London. Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  2. Huo mwaliko ulitangaziwa wapi? Mbona asilimia kubwa ya Watanzania hatuna habari? Fanya kaji Idd party tukujue mkuu wetu mpya ndani ya Ukerwe.

    ReplyDelete
  3. Ndg Anonymous, kabla sijaeleza mtizamo wangu kuhusu swali lako mwaliko ulitangazwa wapi? Nampa Hongera Balozi Kallaghe, ukichukulia kwamba toka afike nchi hii mpaka afuturishe alikuwa hajamaliza hata siku kumi, mimi sikusikia mualiko wala sikuwepo lakini nampa Hongera kaanza vizuri, na baada ya kuona video iliyorushwa na Urbun Pulse, kwenye mitandao mbali mbali ni kwamba aliona juu ya ugeni wake afanye kitu katika mwezi huu mtukufu ambao kwa ndugu zetu waislam una maana sana. lakini nina imani ataitisha kikao rasmi ili kuonana na wanaTZ wooote, usikate tamaa, HONGERA BALOZI, nina IMANI mbegu aliyoipanda balozi MAAJAR, haitakufa, kama alivyosema ustadhi mmoja, London tumepata bahati, imeondoka nyota ingarayo imekuja nyota ingarayo, NYOTA NJEMA HUONEKANA ASUBUHI, Balozi Kallaghe endelea kuwa karibu na wanaTZ. kaondoka Mama kaja Baba uzi uleule, HONGERA, GLORIA

    ReplyDelete
  4. hamna lolote, sifa tuu mama hawezi kumpata. Yote haya kumfurahisha rais,hana stori basi tu. balozi mwenyewe mbona hashua tupu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...