Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego (kushoto) akisisitiza jambo kuhusu sanaa ya unenguaji nchini.Katikati ni mwasilishaji wa mada,Mama Nsao Shalua na Katibu wa CAJAtz,Hassan Bumbuli.
Mkurugenzi wa Extra Bongo,Ally Choki ‘Mzee wa Farasi’ naye alikuwepo.Hapa akichangia ambapo alisema kwamba, tatizo la wanamuziki wa dansi wana wivu uliokithiri hivyo kushindwa kuwa na unenguaji wenye kubeba utambulisho wetu.
Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakiangalia kupitia Projector moja ya picha chafu ya mnenguaji wa bendi.
Sehemu ya umati wa wadau wa Sanaa ukifuatilia kwa makini kauli kuhusu unenguaji zilizokuwa zikitolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA,BW.Materego (hayuko pichani).

Na Alistide Kwizela,BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka viongozi wa Bendi kuacha mara moja tabia ya kuwadhalilisha wacheza shoo (wanenguaji) kwa kuwavalisha mavazi ya kutia aibu na yanayodhalilisha utu wao.

Aidha,BASATA imewataka wanenguaji hao kuthamini utu wao na kufikiria upya dhana kwamba bila kuvaa nusu uchi basi sanaa ya muziki wa dansi haiwezi kupata soko na kuvutia watazamaji wengi kwenye maonyesho.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linaloandaliwa kwa pamoja na BASATA na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) na kufanyika kila Jumatatu,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, lazima wadau wa muziki wa dansi wafikirie upya na kubadili mara moja tabia ya kuendekeza maonyesho yanayochafua maadili ya mtanzania.

“Wanenguaji lazima wafikie hatua waseme kwamba, udhalili wa nusu uchi basi tena.Wavae mavazi yenye heshima kama wanavyovaa wale wa kiume” alisema.

Aliongeza kuwa dhana kwamba bila wanenguaji kuvaa nusu uchi maonyesho ya muziki wa dansi hayapati watazamaji na biashara haifanyiki ni uongo na inaonesha jinsi wasanii wa dansi walivyokosa ubunifu wa kuvutia watu kwenye maonyesho yao na badala yake kubaki wakiendeshwa na hisia zisizo za kisanaa.

“Ushindani wa kibiashara ambao unaomfanya msanii kuwa dhalili ili kuvuta watu kwenye maonyesho haukubaliki bali unawafanya wasanii kuwa makapuku na wanaopoteza thamani yao” aliongeza.

Alisisitiza kwamba, BASATA limekuwa likikemea na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya unenguaji wa nusu uchi lakini mabadiliko yamekuwa ni ya muda na baadaye kurudi kwenye udhalilishaji uleule.

Aliongeza kwamba,Baraza kwa sasa linafanya utafiti kwenye sanaa ya unenguaji na mara utakapokamilika mwongozo kwenye sanaa hii utatolewa na kutakiwa kufuatwa na wadau wote.

Kwa upande wake, mwasilishaji wa mada Mama Nsao Shalua ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji sanaa, BASATA alisema kwamba, mavazi katika kazi ya sanaa yapo kwa ajili ya kuwakilisha tamaduni za jamii husika hivyo vichupi vinavyoonekana kwenye majukwaa yetu havina utambulisho wala maana yoyote.

‘Maleba (mapambo/mavazi) katika sanaa yoyote yanakuwa na utambulisho wa jamii na kazi husika hivyo vivazi vya nusu uchi vinavyovaliwa havina nafasi” alisema.

Katika Jukwaa hilo la sanaa lililopambwa na maonyesho ya wanenguaji kutoka bendi mbalimbali nchini waliokuwa katika mavazi tofautitofauti wadau wengi walilamika juu ya mavazi ya kutia aibu wanayovaa wanenguaji na kutoa wito wa hali hiyo kukoma mara moja.

Jukwaa la Sanaa litaendelea kama kawaida Jumatatu ya wiki ijayo kwenye Ukumbi wa BASATA ambapo mada itakuwa ni Soko la Ubunifu wa Mavazi Tanzania na Changamoto zinazowakabili itakayowasilishwa na Mbunifu maarufu nchini Mustapha Hassanali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Muziki..ulevi na uzinivu ni vitu pacha.Hapa hakuna cha mavazi wala nini ishu ni watu watafute kazi nyengine zakufanya na co kuendekeza upuuzi tu.Najua mtakuja na hoja kwamba watu wanatajirika kwa muziki na muziki ni ajira lkn napenda kuwakumbusha kwamba hata ujambazi na uuzaji wa madawa ya kulevya pia huatajirisha watu,so navyo vinafaa?Na hapa naomba nieleweke vizuri miziki ya aina yote haifai na hupelekea ktk uzinifu iwe ni dansi,muziki wa kizazi kipya,tarabu,kwaya na hata maulidi vyote ni miziki tu na wote mlio na mtazamo huru mtagundua nini hufanyika ndani ya hii miziki niliyoitaja.Namaanisha yote bila ku-exclude hata mojawapo.So tuache miziki ya aina yote na tufanye mambo mengine ya maana na biila hivyo kelele zenu za kukataza vichupi zitakua zabure.

    ReplyDelete
  2. HUU ni Udikteta sasa,
    Hauwezi kumpangia Mtu jinsi ya kuvaa,
    Wengine hivyo vichupi mnavyovichukia ndivyo vinavyotupeleka kwenye shoo.
    SWALA LA UTAMADUNI ,WATANZANIA UTAMADUNI WETU NI WA KUVAA MAJANI NA NGOZI; TENA KWA KUFUNIKA NYETI TU:
    MAVAZI MENGINE YOTE YALITOKA KWA WAGENI; waarabu sana sana,
    ELIMU YA KUJITAMBUA NDO YA KUIKAZANIA;MBONA ULAYA WATU WANA VAA NUSU UCHI TENA BARA BARANI LAKINI BADO WANAHESHIMIANA;
    LABDA KAMA MNATAKA KUMPA DILI HUYO KABA...LI ANAYE BUNI MIBATIKI; NAJOTO LOTE HILI ;HIYO MINGUO MNAYO BUNI AVAEE NANI??
    Kwanza gharma pili emekaa kiajab ajabu tu.

    ReplyDelete
  3. we mdau wa kwanza una akili kweli?ebu tuondolee uzee wako hapa kwani hupo dunia gani?

    ReplyDelete
  4. Ok can you look to miss Tanzania's side Mr Basata? Vipi na wizi wa mabilioni ni utamaduni wetu pia?

    ReplyDelete
  5. what about ngoma za utamaduni? watu wanavaa almost uchi na wanacheza kama wanafanya matusi.

    Huyu jamaa anachemsha! Sex sells!

    ReplyDelete
  6. KATIBU WA BASATA WEWE BADO MGENI KWENYE HII SANAA YA MUZIKI. TUNAKUHESHIMU SANA ACHANA NA HIYO ISSUE YA AINA YA MAVAZI KWANI ITAKUUMBUA BURE. MZEE KAWAWA ALIJARIBU SWALA LA MAVAZI LAKINI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALIKUJA KUMUUMBUA KIAINA KWA KUTANGAZA WANANCHI WAACHIWE KUVAA WAPENDAVYO KWANI MAVAZI NI FASHION TUU. INAKUJA NA KUPITA.

    ReplyDelete
  7. Kweli mdau hapo juu ni fashion tuu hizo kwa wanenguaji pia. Unajua miaka ya kuanzia 1994 mpaka 2007 mabinti zetu wengi wa kibongo walikuwa wanapenda kuvaa Vitop na kuacha matumbo wazi mchana kweupe. Hivi sasa Vitop hivyo unaweza kusema ni kama havipo tena. Huwaoni mabinti zetu wakivivaa tena labda wale wakuja kuja bado.

    ReplyDelete
  8. Vipi Katibu wa BASATA kwenye mashindano ya urembo VICHUPI unaruhusu na unaenda kushuhudia. Kwanini kwenye mziki wa dance ndiyo unaona vichupi vina kasoro?. Usituharibie starehe tafadhali

    ReplyDelete
  9. Vipi Katibu wa BASATA kwenye mashindano ya urembo VICHUPI unaruhusu na unaenda kushuhudia. Kwanini kwenye mziki wa dance ndiyo unaona vichupi vina kasoro?. Usituharibie starehe tafadhali

    ReplyDelete
  10. BASATA ITABIDI PIA MUENDE COCO BEACH MKAZUIE VICHUPI ILI WATU WAOGELEE NA SUTI NA MABAIBUI,PIA MSHAURI MASHINDANO YA UREMBO WATUMIE MABAIBUI.TIMU YA SOKA TAIFA WAVAE KANZU NETIBOLI MAJINZI.UTAMADUNI WETU NI KUVAA MAJANI KIUNONI BILA CHUPI WALA BLAZIA MAANA HIZO NGUO NILIZOZITAJA HAPO JUU ZIKIWEMO CHUPI NA BLAZIA ZIMELETWA NA WAARABU NA WAZUNGU.SASA HUYO MWENYEKITI NA WENZAKE KWA NINI WAMEVAA CHUPI HAPO MKUTANONI.SIAMINI KAMA MTOA MAONI WA KWAZA KABISA ALIKUWA HAJAVAA CHUPI NDANI WAKATI ANATYPE MAONI YAKE.HUO SIYO UTAMADUNI WETU,KAVUENI NGUO ZENU MVAE MAJANI BILA CHUPI.

    ReplyDelete
  11. Watanzania wanapenda hanasa sana ndo maana wanashupalia mambo kama haya utasikia wanatolea mfano Marekani nyie TZ mnaweza jilinganisha na marekani, ni hanasa tu hakuna lolote musiki hata ukivaa vizuri kwenye shoo hat kwenye video cha muhiumu hapa ni ujumbe sasa hawa jamaa wanapenda uchi makahaba tu.

    ReplyDelete
  12. eti "nusu uchi"

    eti "kulinda maadili"

    Wanenguaji lazima wafikie hatua waseme kwamba, udhalili wa nusu uchi basi tena.Wavae mavazi yenye heshima kama wanavyovaa wale wa kiume” alisema.

    ni vipi mtoto wa kike avae kama mtoto wa kiume..wadada wakivaa kama rafiki yangy Sister P..utasuíkia sio maadili eti "msag*ji..

    Hii ndio tz porojo nyiingi tu..mpaka leo vazi la taifa kitendawili...BASATA MPOOO?wasanii wanaibiwa na mnawaibia MPOOO?

    Sema shukuruni Mungu nyie basata wasanii walio wengi(sio wote) wapo tayari kuburuzwa ndio maana mnatake advantage..

    Tutafika tu

    ReplyDelete
  13. Wanenguaji waache ushamba,, kuvaa nusu uchi sio dili wengine tunakwenda kusikiliza nyimbo sio kuangalia mapele ya watu mwilini miili yenyewe kwanza imechoka. Mbona kina Marijani walikuwa mabingwa na kina Mbaraka Mwinshehe, Maneti nk mbona hawavai nusu uchi, mnaouunga mkono vichupi wote walevi wa ngono

    ReplyDelete
  14. Nashangaa BASATA wanasubiri nini kuwapiga faini kubwa kama vile Traffic na Majembe wanavyopiga faini daladala korofi. Bendi zinazoharibu maadili zifutwe. Na hayo mashindano ya vichupi yalaaniwe hadi na sisimizi kuharibu mabinti zetu,Kikwete piga marufuku

    ReplyDelete
  15. Huku tunakoelekea jamani hakueleweki wakati hawa wanapigiwa kelele wamevaa nusu uchi kuna huyu Lady Gaga kawaacha watu midomo wazi kwa kuvaa nyama i mean nyama ya kutoka buchani!

    ReplyDelete
  16. Nyie vipi? hawa si ndio wale waliokuwa wakinengua kwenye kampeni ya ccm huko kwa malecela! wanafaa tu, mpaka ccm imewapeleka mtera, basi wanafaa.

    ReplyDelete
  17. Asanteni sana Basata kwa kuliona hilo maana hii ni aibu tosha! Naomba sana isiishie kwa wanenguaji tu wahusika wawaangalie pia hawa wenzetu wa filam, maana naona nao wanakuja kasi na vivazi vya nusu utupu.

    Mdau Zanzibar

    ReplyDelete
  18. nshimimana aka dumisaneSeptember 14, 2010

    Anoni wa Sept. 14, 04:19:00 sijui unataka nini hapo unaposema watu waogelee na suti!?

    unakuja kasi...

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  19. juzi tumechagua Miss Tz leo wanenguaji hawafati maadili.
    Tafuteni kazi zingine

    ReplyDelete
  20. BASATA TOENI USHAMBA, NUSU UCHI MWENYE BIKINI..MZEE ZIMEKUJAA NINI NDO MANA UNAONA SHIDA..TAFUTA MKE!!!!!1

    usA

    ReplyDelete
  21. BASATA acheni ujinga. Fanyeni kazi ya kusimamia maslahi ya wasanii, sio kupoteza muda kufukuza vichupi.

    Msanii anavaa kutegemea na hadhira. Kama hadhira inapenda vichupi itamshangilia. Kama hawapendi vichupi watamzomea.

    So far, ni wazi kuwa vichupi ndio dili.

    ReplyDelete
  22. wanenguaji wamnezidi its tuu muchi jamani bora wangenengua kama kidance dance kama wamarekani lakini wao kama wako unyagoni wakati unyagoni ni siri kubwa haitakiwi hiwe adharani hiyo ndo mira ya kitanzania.lakini sikuizi unyago waziwazi na zile video za sasambu sasambu nazo iwe kwa siri ni kwajiri ya kina mama tu sio nchi nzima inashuhudia mambo ya kitcheni pati the whole meaning is ruined mauno wazizi mpaka wanalamba miche kama wanaramba mbolilo astagafirulai Basata waingelieni kina mama/dada na kujiadhiri na mipicture yao ya lana ya kitchen party.wana adhirika tu uchafu mtupu utamaduni wetu inatakiwa iwe top secrete

    ReplyDelete
  23. Hata kwa waliko akina Gaga, wanaume vijana wanaovaa mitepesho na kuonyesha chupi zao, wanapigwa vita: Broklyn (NYC), Connecticut na sehemu nyingne za Texas!

    Sisi tulipowaona tu, tukaanza kuiga bila hata ya kujua hiyo mitepesho na miondoko ya majipu kordani na matakoni ilianzaje!

    Achilia mbali...marepa!

    Eti ndio vya usasa! Kwani tuliandikiwa au tnashikiliwa bunduki vichwani kuwa kila chao cha usasa ni lazima tuige?

    ReplyDelete
  24. JAMANI LAKINI SI NDIYO ASLI YETU WANAWAKE LAZIMA WAONYESHE MAUMBILE YAO,NGUO TULILETEWA NA WAZUNGU SISI TULIKUWA TUNATEMBEA UCHI WA MNYAMA SASA CHA AJABU KITU GANI
    WAACHENI WAVAE YOTE RUHUSA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...