Na Asteria Muhozya;
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto imetoa hundi yenye thamani ya Tshs. 2,500,000/= kwa Chama cha Wasiiona Tanzania baada ya kupokea ombi la Chama hicho mwezi Mei, 2010.
Akikabidhi hundi hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa hicho, Bw. Robert Bundala, Katibu Mkuu, Bi. Mariam Mwaffisi amesema kuwa, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, imetoa kiasi hicho cha hundi kwa Chama hicho kwa madhumuni ya kununulia fimbo nyeupe mia moja ikiwa ni kwa ajili ya kuwawezesha wasiiona kupunguza ugumu wa matatizo mbalimbali yanayowakabili.
Aidha, Bi. Mwaffisi amepongeza jithada mbalimbali zinazochukuliwa na Chama hicho katika kushughulikia kero za wasioona nchini na kuongeza kuwa, juhudi hizo ni ishara tosha inayoonyesha dhamira ya dhati ya Chama cha Wasiiona katika kuwashirikisha wanachama kwa pamoja kujadili changamoto na utatuzi wake.
Ameongeza kuwa, jitihada hizo pia zinaongeza kupanuka kwa demokrasia na kuendeleza wajibu wa Asasi zisizo za Kiserikali katika kusaidiana na Serikali kuwajengea watu wenyewe uwezo wa kujitegemea.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Robert Bundala amesema kuwa, amefarijika sana kwa msaada huo walioupata kwasababu walihitaji nyenzo za kuwazesha kumudu mazingira yao, kwani wakati mwingi wamekuwa wakionekana kama mizigo mizito isiyobebeka.
Ameongeza kuwa, tatizo la kukosa Fimbo limekuwa likiwagharimu sana hali iliyopelekea kukodi watu wa kuwasaidia ambao nao hudai kupata chochote katika kutoa msaada huo, na kuongeza kuwa, lakini wanapokuwa na fimbo hizo zinakuwa ni nyenzo kubwa sana kwao.
Aidha, Bw. Bundala amemalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania wote kuwaona wasioona kama binadamu wengine wote kwani wao wamepungukiwa macho tu lakini wanaakili timamu na uwezo wa kufanya kazi kama walivyo wengine.
Vilevile, ameeleza kuwa, tarehe 15 Oktoba, 2010 yatafanyika Maadhimisho ya Fimbo Nyeupe Kitaifa Mkoani Shinyanga ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...