MAREHEMU JULIUS MSEKWA.

FAMILIA YA PIUS MSEKWA INA HUZUNI KUTANGAZA KIFO CHA MPENDWA WAO JULIUS MSEKWA, KILICHOTOKEA PARALIMNI, CYPRUS, JUMAMOSI YA TAREHE 11/09/2010.

JULIUS ALIKUWA AKIISHI NA KUFANYA KAZI NCHINI UINGEREZA TANGU MWAKA 1996, ALIKUWA AMEKWENDA CYPRUS KWA MUDA MFUPI , AMBAPO NDIKO MAUTI YALIPOMFIKA.

TARATIBU ZA KUREJESHA MWILI DAR ES SALAAM KWA AJILI YA MAZISHI ZIMEKAMILIKA NA MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIWA KUWASILI JUMAPILI 19/09/2010, ALFAJIRI KWA NDEGE YA EGYPT AIR.

MAZISHI YATAFANYIKA JUMATATU 20/09/2010 KATIKA MAKABURI YA KINONDONI, DAR ES SALAAM.

MSIBA UPO NYUMBANI KWA NDUGU PIUS MSEKWA, NO. 13 BONGOYO RD. OYSTERBAY. KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU, SALA ZETU WOTE NI KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU

MAHALI PEMA PEPONI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. duh,at least kwa mara ya kwanza sijaona maombi ya mchango ili kusafirisha mwili wa marehemu
    R.I.P J.MSEKWA

    ReplyDelete
  2. Yani Im shocked!

    Jirani Obay

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wafiwa maan huyo aliyeondoka anaonekana kuwa bado kijana mdogo ambaye Taifa na ulimwengu ulikuwa bado ukimhitaj.

    Kwa watu wa ughaibuni naomba niulize, mbona kumekuwa na misiba ya kufululiza na wanaokufa ni vijana wa umri wa kati hasa kutokea maeneo ya Ulaya na Scandnavia!!? Nafikiri hili linahitaji mjadala.


    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  4. angalia ratio ya watu wanaokufa nyumbani na walio ughaibuni ipoje ndio huandike,cha muhimu ni kumuombea marehemu sio lawama kufa nipopote,fikiria kabla ya kuandika,poleni sana familia ya marehemu.

    ReplyDelete
  5. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema,huyo kaka anayehoji vifo ni wangapi wamekufa leo huko nyumbani?umewahi kufanyia mjadala?naomba ufikirie kabla ya kuandika.wote ni wasafiri sijui mwenzetu.............

    ReplyDelete
  6. poleni sana kwa msiba may his soul rest in peace. anony wa sept 16, mauti haya chagui age,sex wa region. mjadala una weza kuwepo na vipi mauti yakikuta wewe utajuaje kilicho zungumziwa? just grow up

    ReplyDelete
  7. R.I.P Msekwa

    Annon wa Thu Sep 16, 04:32:00 PM

    Unataka mjadala wa nini juu ya kifo?. Tanzania wanakufa watu kila siku, watoto, vijana, wazee n.k kwa sababu ndiyo demographic iliyopo Tanzania, same kuona watu wa Ulaya na Scandinavia wanatangazwa wamefariki ujue ndiyo demographic ya watanzania waliopo huko, Unataka wazee wafe wakati hawapo?.

    Kufa ni ahadi na wakati ukifika hakuna dawa wala location, kifo kinaweza kukuta anywhere.

    ReplyDelete
  8. anon hapo juu, Hii ni mipango ya mungu kwani sio wote wanaofariki wanawekwa kwenye blog hii jamii.
    Mungu amalaze mahali pema peponi.
    Mbona hata tz wanafariki wengi

    ReplyDelete
  9. Poleni sana familia ya Msekwa! Nimesikitika sana kusikia kuwa Julius ametutoka. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  10. R.I.P JULIUS MSEKWA

    Poleni saana familia wahusika na marafiki kwa kifo cha ghafla kilichomtokea ndugu yetu Julius.
    Huu ni msiba uliyotupiga moyoni wote tunaomfahamu ndugu Julius, bado ni kijana mdogo kwa umri na kututoka mapema hivi ni majonzi makubw saana kwa sisi sote.
    Mungu amlaze mahari pema.

    Mickey Jones
    mdau wa Denmark

    ReplyDelete
  11. mdau una maana scandnavia sio ulaya.Halafu mbona sijaona tangazo la msiba wa mtu scandnavia mwaka huu!umejiconfuse.mdau

    ReplyDelete
  12. Poleni sana Familia ya Msekwa. Mwenyezi Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu Julius.. Amina. Sasa jamani kwa nini msiba usingefanyika pale Mlalakuwa ambako ndipo siku zote tumekuwa tunajua ni kwa kina Julius Msekwa. Tena hata mama yake mzazi kazikwa pale pale!! Anyways haya ni mambo ya familia japo wazee wa Mlalakuwa tuliyemlea mtoto hatujafurahia.

    ReplyDelete
  13. Good point Anony wa Bongo
    Hata mimi nimejiuliza sana hili swali, wabongo hatuko salama huku watu wanakufa tu vifo visivyoeleweka na ni vijana
    nafikiri hili swala linatakiwa kufanyiwa uchunguzi

    ReplyDelete
  14. Wewe Nkyabo unataka mjadala na nani? Tafadhali muandike mungu barua mapema,ili ku book hiyo appointment ya mjadala. Si unajua tena mungu yupo busy sana, kwahiyo hakikisha umetuma barua yako wiki tatu kabla ya tarehe ambayo unataka mjadala ufanyike.RIP MSEKWA

    ReplyDelete
  15. Acha primitive statistics.. we uoni vijana wanavyokufa bongo kwa pikipiki na ngono.. jadili hilo..

    Julius aka konyagiusa
    Los Angeles , California

    ReplyDelete
  16. Duh what happened.

    Too young to go lakini yote ni mipando ya Mungu.
    RIP

    ReplyDelete
  17. R.I.P Julius! Poleni sana Familia ya Msekwa.

    From Jirani mitaa ya State House.

    ReplyDelete
  18. Kwanza tuwape pole ndugu, marafiki wa marehemu na familia yake Mzee Msekwa. Kuhusu hoja ya Mtoa Maoni Nkyabo juu, kauliza swali nyeti sana. Kwanini vijana wengi wanafariki mapema Ulaya karibuni? Hatuwezi kusema kwa hakika sababu gani kila mmoja anakufa ghafla maana sisi sio tuliofanya "autopsy" au kuwagangua; lakini ninachoweza kuchangia mada hii muhimu ni hili. Maisha ya Uzunguni ni ya haraka na yana "stress" sana hivyo si ajabu kupatwa na mstuko wa moyo,nk. Pili, ingawa maisha ya Majuu yamerahisishwa kwa teknolojia na mawasiliano mepesi bado yanaweza kuhatarisha moyo. Hakuna mawasiliano ya kibinadamu (kama humjui mtu huwezi tu kubwata naye mazingira haya) ; tatu, Waafrika tunakuwa na majukumu mengi tukiwa Majuu. Tuna majukumu ya kumaliza kilichotuleta (kusoma, kazi, nk), tuna majukumu ya kusaidia ndugu na jamaa(hususan nyumbani), tuna wengi wa kufikiria, halafu kuna kupambana na hali ngumu ya hewa na baadhi ya wenyeji wasiopenda wageni. Spidi kali; mwendo wa roketi..
    ( Tusisahau pia kuwa karibuni nyumbani na Majuu kumeenea ugonjwa wa kisukari kwa vijana hasa kutokana na unene...)
    Mwisho hakuna rahisi kwa mtu mweusi popote alipo; iwe Afrika au Majuu. Hata vigogo hubidi kukuna vichwa, kinamna. La muhimu ni kujaribu "kuleta uwiano" (balance) katika kila kona ya maisha. Kuangalia unajitunza, kupumzika pale unapotakiwa (lala saa zinazotakiwa) kujaribu kula kwa mpangilio (huku unafanya mazoezi ya viungo) na juu kabisa, kumheshimu Muumba. Mungu aiweke roho ya marehemu pema peponi, Amen!

    ReplyDelete
  19. Inna lillah wainna ilah raajioun..Baba yangu Mzee Pius Msekwa pole sana kwa kuondokewa na kijana wako. Tumshukuru Mola kwa kila linalotufika

    ReplyDelete
  20. RIP Julius. Poleni wafiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...