Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Jonathan Njau baada ya kusimama katika Kijiji cha Dung’unyi na kusalimia wananchi wakati akiwa njiani kuelekea katika uwanja wa mkutano wa kampeni Makiungu Mjini Mkoani Singida leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauya, akipiga gitaa la besi katika Jukwaa la bendi ya Vijana Jazz, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa urais wa CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, uliofanyika kwenye Uwanja wa Makiungu mjini leo.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Bi Mariam Lazaro (90) mkazi wa Kijiji cha Dung’unyi, kumuombea Kura mgombea Udiwani wa Kata mpya ya Dung’unyi, Bwana Bruno, (kushoto) wakati msafara huo ukipita katika kijiji hicho kuelekea Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida leo katika mkutano wa kampeni.Picha na Muhidin Sufiani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Brother mbona hatuoni na kampeni ya vyama vingine?

    ReplyDelete
  2. habari kaka michuzi.Tumeshatuma maoni watu kibao ili wasome mawazo yetu cha ajabu umetubania kabisa sijui kwanini na sisi ndio wadau wa tuvuti hii au mwezetu umeelemea upande mmoja kuwa fear.ni mimi mdau wa michuzi Blog

    ReplyDelete
  3. Tehe teh tee!

    Naona upele sasa umepata MKUNAJI.
    M-bangubangu/tindiga kazana mwanangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...