
Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea wa ubunge katika jimbo la Karatu kupitia chama hicho, ambaye ni mridhi wake, Mchungaji Israel Natse, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana.

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni zake kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Bariadi juzi.

Baadhi ya wanachma na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakishangilia hotuba ya mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wakati akihutubia mkutano wa kampeni zake, kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana.Picha na Joseph Senga
Yaani chadema wamekosa mgombea karatu nzima mpaka wamteue rev. natse. Shame on them!!!
ReplyDeleteWhat???? Tunakwenda wapi jamani? Tusichanganye maji na mafuta. Tusichanganye siasa na dini. To be forewarned is to be forearmed.
ReplyDeleteViongozi wa ndini wabaki kwenye dini,watatupeleka kubaya tukichanganya dini na siasa...historia inasema hivyo!!
ReplyDeleteJamani.Slaa na CHADEMA mbona mnatudharau watu waKaratu hivi. Mnatuletea mchungaji. Si mngemteua hata PP au Lazarus Tito. Hapana kura yangu ninampa Dr Lori wa CCM. Mwaka huu CCM inachukua jimbo.
ReplyDeleteMheshimiwa Mchungaji Lackson Mwanjali ni mbunge wa Mbeya vijijini kwa tikiti ya CCM anayemaliza muda wake. Mh,Mchg,Dr Getrude Rwakatare ni mbunge wa viti maalum kwa tikiti ya CCM anayemaliza muda wake.
ReplyDeletechadema mimi nawakubali ila kwa hili mnachemka sana.mkubwa wewe si mchungji sasa inakuaje unaacha kazi za kanisa unaingia ktk siasa tena,kondoo wako watachungwa na nani wakati unajua kabisa kazi za kanisa ni wito sasa inakuwaje uachane ka kanisa uende katika siasa mchungaji au ndio yale yale ya lwakatale.ACHENI TAMAA BWANA TUMIKIA KANISA MSIJE MKATULETEA MAMBO YA UDINI HAPA HATUTAKI BANA
ReplyDelete