Assalaamu Alaykum
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nanihii,
Kwanza tunamshukuru Allah kwa kutuwezesha kuukamilisha mfungo na kisha kusherehekea Eid.
Pili twatuma shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano wako binafsi chini ya blogu ya jamii kwa kukubali kuchapisha matangazo yetu ya Darsa za Ramadhan ambazo zilifana sana.
Mara hii naomba utupeperushie salamu za shukrani kwa wadau hapa jijini Leicester:
SHUKRANI KWA KUFANIKISHA EID LEICESTER UK
Assalaamu Alaykum
Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumwombea rehma na amani Mtume wake SAW, ujumbe huu lengo lake ni kutoa shukrani na pongezi kwa kila aliyeshiriki kufanikisha shughuli za Darsa za mwezi wa Ramadhani hapa Leicester na hatimaye sherehe za Eid zilizofanyika hapo Msikiti wa Madani na Madrasatun Nuur, Malabar Road.
Kwa hakika orodha ni ndefu sana, hivyo si rahisi kuorodhesha majina yote, ila twaomba ujumbe huu wa shukrani umfikie kila aliyeshiriki kwa namna yoyote, iwe ni kihali, kimali au hata kimawazo.
Ushirikiano wenu si tu kwamba unatupa moyo na ari ya kuendeleza juhudi hizi, lakini pia unaacha deni ndani ya nyoyo zetu ambalo kulilipa kwake ni kuendelea kukutumikieni bila kuchoka.
Tunamwomba Allah azitakase amali zetu, atukubalie funga zetu na aboreshe umoja, mshikamano na mapenzi ya dhati baina yetu,
Amin.
Uongozi,
Madrasatun Nuur
Leicester

Hebo rudini nyumbani nyie waosha vyombo na wabeba maboksi!nasikia kule mnadoea fitra na zakaa za wakoloni na alfu mnajifanya ndo wenyeji...aaa aibu tupu!
ReplyDelete