waimaji wa bendi ya Mjomba inayoongozwa na Mrisho Mpoto (kati) wakiimba moja ya nyimbo wakati wa hafla hiyo.

Mwezi Januari 2010, Femina HIP na D.light kwa pamoja walizindua kampeni ya kitaifa ya ‘Haki ya Mwanga Salama’. Lengo la kampeni ni kuchochea mabadiliko ili hatimaye shule zote, wanafunzi, wazazi na serikali watafakari na kuunga mkono matumizi ya taa za sola.

Mkurugenzi Mtendaji wa Femina HIP, Dk Minou Fuglesang, anasema: “Tungependa kuona wanafunzi wote wanapewa vitabu, kalamu, sare za shule lakini pia wanapatiwa taa salama ili waweze kujisomea na waboreshe maisha yao”.

Shughuli mbalimbali za uelimishaji zimefanyika ikiwa ni sehemu ya kampeni hii. Mrisho Mpoto, msanii maarufu wa mashairi, ni balozi wa kampeni ya “Haki ya Mwanga Salama”. Amekuwa akitoa burudani kwa jamii nchini kote, huku akizungumzia faida za taa za sola.

Hivi sasa ametunga wimbo “Mama Siwema” ambao unaelezea hadithi ya Siwema, mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa na bidii ya hali ya juu masomoni, ambaye alipoteza maisha yake katika ajali ya moto wakati akijisomea kwa kutumia taa ya mafuta (chemli).

Ukosefu wa vyanzo salama vya nishati ni changamoto kubwa inayoikabili Tanzania, kwani 10% tu ya wananchi ndio wenaofikiwa na huduma ya umeme. Maeneo ya vijijini, ni 2% tu. Lakini leo hii kumekuwa na ongezeko la upatikanaji wa vifaa vinavyotumia nishati ya jua na taa zinazotumia nishati hiyo, ambazo hata wananchi wa vijijini wanamudu gharama yake.

Teknolojia hiyo hivi sasa ipo na kuna haja ya kuhamasisha matumizi yake katika jamii. Femina HIP na D.light kwa pamoja tunatoa mchango wetu muhimu katika kuhakikisha kwamba jamii ya Tanzania inaelimika na kutumia taa za sola ili kuboresha kiwango cha elimu kwa kuwawezesha wanafunzi kujisomea katika mazingira salama, kuishi mtindo bora wa maisha na kuboresha maisha ya jamii nzima.

Katika hafla hii, D.light imezindua ofa maalumu ya taa ya kusomea ‘Solata’ kwa shule za sekondari nchini Tanzania. Wanafunzi 50 kwa kila shule ya sekondari wataweza kupata taa ya sola ya kusomea, yenye thamani ya Tsh 22,500 kwa bei pungufu ya Tsh 10,000 TU! Vocha maalumu zitasambazwa sambamba na toleo lijalo la Jarida la Fema ambalo litasambazwa mwezi Oktoba.

Kwa habari zaidi wasiliana na

frederick@feminahip.or.tz
ama
laura.smeets@dlightdesign.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...