Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa,Ridhiwani Kikwete akivishwa kitenge alipowasili katika Kata ya Nandagala, Ruangwa ikiwa ni ishara ya Mgombea urais kupitia chama hicho, Jakaya Kikwete kuwa atashinda kwa kishindo katika uchaguzi Mkuu.
Ridhiwani akiwasalimia wananchi wa Kata ya Nandagala, Ruangwa, mkoani Lindi jana.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa,Ridhiwani Kikwete akilakiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Ruangwa kupitia CCM,Khamis Majariwa baada ya kuwasili jana katika Kata ya Nandagala, tayari kuanza ziara ya kuhamasisha vijana na wafuasi wa chama hicho kuweka mikakati ya ushindi mkubwa kwa cham

Picha na Habari
Na Richard Mwaikenda, Lindi.

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Lindi mjini kupitIa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mohammed Abdulaziz amewaomba radhi wana CCM aliowakosea wakati wa kinyang'anyiro cha kura za maoni baada ya kutakiwa hivyo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Ridhiwani Kikwete ili kuvunja makundi katika jimbo hilo.

Abdulaziz,alifanya hivyo juzi katika kikao cha ndani cha viongozi wa Umoja huo wilayani Lindi juzi, ambapo baadhi ya viongozi walieleza wazi mbele ya Ridhiwani kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko mkubwa ambao walidai ulisababishwa na wagombea wawili, Abdulazizi na Maguo pamoja na wapambe wao wakati wa mchakato wa kura za maoni.

Baada ya wanachama kueleza hivyo na Ridhiwani kugundua ufa huo uliopo Lindi mjini na kuhatarisha umoja ndani ya CCM, ndipo akaamua kutumia fursa hiyo kuweka mambo sawa kwa kumtaka Abdulaziz aliyeshinda kura za maoni na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM, afanye uungwana kwa kupita kwenye matawi kuwaomba radhi wana CCM ili kuvunja makundi na kurudisha umoja ndani ya chama.

"Mwenye nafasi ya kuvunja makundi ni yule aliyeshinda.Hawa jamaa wametukanwa na kunyanyasika hivyo inatakiwa aliyeshinda ajishushe aende kwenye matawi kuwaomba radhi ili wote wawe kitu kimoja na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, Mwaka huu,"alisema Ridhiwani huku akishangilia na wanachama.

"Wanachama wenzangu wa CCM, huwa makundi yanakufa moyoni na si machoni kwa mtu, kwani kuna mtu anaweza akakuchekea na kukuambia mambo yameisha, lakini kumbe moyoni bado anayo.Alisema katika kipindi cha harakati za kugombea uongozi makundi yanakuwepo, lakini mchakato ukishapisha na mmoja wao kuteuliwa inatakiwa kuvunja makundi na wote kumuunga mkono aliyeshinda na ndivyo tunavyotakiwa kufanya Jimbo la Lindi Mjini na kingineko". aliongeza Ridhiwani.

Alisema kuwa wakati wa kinyang'anyiro kuwania uongozi ndani ya chama ni kawaida katika kampeni huzuka makundi lakini baada ya kuwapata washindi huvunja mkundi na wote huamua kuwaunga mkono walioshinda.

Baada ya Ridhiwani kumalizia kuzungumza, alikaribishwa Abdulaziz ambaye alisimama na kuwaomba radhi wote aliowakosea na kuahidi kuwa atapita kwenye matawi ya chama jimboni humo kuwaomba radhi ikiwezekana kuwapigia magoti na hata kwa kugharaghara mbele yao.

"Kwa wale wote niliowakosea nawaomba radhi, nitapita kila tawi kuomba radhi ikiwezekana kwa kupiga magoti hata kwa kugharaghara kwani naamini vijijini na mjini wote walinipigia kura ndiyo maana nimeteuliwa kuwa mgombea katika jimbo hili,"Abdulazizi alisema na kuanza kukumbatiana na wanachama kitendo ambacho kiliashiria kumaliza tofauti zao.

Ridhiwani ambaye ameongozana baadhi ya vijana makada wa CCM,anafanya ziara ya kuhamasisha wanaCCM na wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha wanawapigia wagombea wa chama hicho ili washinde na kuunda dola kwa kipindi kingine cha mikaka mitano.Ziara hiyo ataifanya katika mikoa ya Lindi,Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Iringa na Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hii kali jamani, yani mama Salma anapiga kampeni, Ridhiwani anapiga kampeni JK mwenyewe kampeni. Familia nzima wanapiga kampeni.
    Gharama hizi kweli ni zao wenyewe?

    ReplyDelete
  2. RIDHIWANI ANA SAFARI NDEEFU KIDOGO YA KUISHI NA WATU UKIANGALIA UMRI WAKE TOFAUTI NA WAZAZI WAKE, HIVYO NATEGEMEA ANAFAHAMU FIKA UMUHIMU WA KUWAFANYA WATU WASIMCHUKIE ILIHALI BADO KIJANA, KWASABABU UKICHUKIWA NA WATU WENGI ALAFU BADO UNATEGEMEA KUISHI NAO MIAKA MINGI MBELE NI HATARI SANA.

    NI MIMI RAIA WA TANZANIA KWA KUZALIWA

    ReplyDelete
  3. Tanzania mtoto wa boss naye ni boss. mama, mtoto wote wanapiga kampeni kweli ni maendeleo ya wananchi au familia? mambo mazito wafanye viongozi wetu wa kitaifa.

    ReplyDelete
  4. Nikiangalia familia ya JK inanifanya nimkumbuke Sadam Hussein na familia yake,.nasikia kichefuchefu unapotumia gharama kubwa kuwapa elimu watoto wako then wanaishia kwenye porojo za siasa,bi mkubwa nae anatumia fedha za mama zetu kumfanyia kampeni muwewe,mkulu nae anatumia nyenzo zote za serikali kuvunja rekodi ya asilimia kurudi pale magogoni...ivi kweli Jakaya ndilo tumaini lililorejea? nani asiejua kwamba JK atashinda? familia yote imeamia kwenye siasa ili kuvunja rekodi ya asilimia au kuna jingine?iweje nguvu izi ziongeze ng'we hii ya mwisho?
    Ankal mithupu aka friend of CCM ukitaka ipost na kama unaona inawakaba sana ipotezee lkn ujumbe umefika,.

    ReplyDelete
  5. SIJUI NILIE,SIJUI NITUKANE...ILA KUMBUKENI HIZI SIO NCHI ZA KIFALME ALAAA.

    ReplyDelete
  6. huyu jamaa yupo hapo kwa sababu baba yake ni rais na si kwamba ana-deserve, we angalia siku hizi watoto wa wakubwa au elite class ndo wanatayarishwa kuongoza nchi hapo baadae, huwezi kuona mtoto wa mkulima kutoka kyela akipata hizi nafasi hata kama amesoma kupita wao.

    ReplyDelete
  7. Hata Marekani wake na waume wa wagombea urais walifanya kampeni sasa ajabu ni nini? Mbona Chadema watoto wanasubiri nafasi za viti maalum bila hata kufanya kazi yoyote na hamlalamiki? Tena kuna mtu anagombea urais mkewe ubunge, na baba na mkewe wanaongoza chama, na watoto wa wabunge nao wanapewa ubunge? Mmezidi sana unafiki watz.

    Toa boriti jichoni mwako kabla hujatoa kibanzi kwa mwenzio!

    ReplyDelete
  8. Manka-ruangwaSeptember 17, 2010

    Mtoa maoni uliyesema ati ridhiwani yupo kwa sababu baba yake ni raisi ni kuwa kauli yako si sahihi. Je unashindwa kuelewa kuwa amesoma na amekuwa akijiwajibisha na shughuli ambaz ni halali? Mbona akina John mashaka na akina Dr shayo wanatoa mawazo yao na ukiwa kule dodoma wanakuwa gumzo la vijana wetu? je wanafanya hivyo kwa sababu baba zo si marais?
    Mwache ridhiwani afanye kile anachoamini kuwa kitasaidia watanzania.

    ReplyDelete
  9. Dah....Hii kweli ndiyo Tanzania.
    Wananchi wamekabwa sana na umaskini wa kila siku kiasi kwamba hata hizi dalili za awali za viongozi walio madarakani kutaka kutengeneza Tabaka la watawala bado hawazioni hizi dalili.
    Huyu mtoto wa Raisi analazimisha siasa.
    Michuzi irushe hiyo, HABARI ndiyo hiyo.

    ReplyDelete
  10. HII NI HATARI SANA, WATU WA IRAQ WALIPOJENGA HASIRA NA SAADAM HUSSAIN, ILIWAFIKIA NA WATOTO WAKE KWAKUA NA WAO WALIJIFANYA KAMA SAADAM HUSSAIN, RAIS. MAISHA YAO YALIFANANA NA RAIS, WALIKUWA NA SAUTI KAMA RAIS, HIVYO HUYU MTOTO AMBAYE ANAJILAZIMISHA KUWA KAMA KIONGOZI NA BABA YAKE KUMSAIDIA HIVYO, HASIRA ZA WATANZANIA DHIDI YA BABA YAKE ZITAMFIKIA NA YEYE KAMA USAY Saddam Hussein NA QUDAY SADDAM HUSSEIN.

    ReplyDelete
  11. Haifurahishi hata kidogo, nchi imekuwa kama ni ya Kifalme!! Leo mama yupo huko kesho baba yupo huku na mtoto yupo kule ni maisha gani haya? hivi ni kweli hizo pesa zinazotumika si mali yetu? Hata kama mmetuibia basi tumieni kwa kificho.
    Labda nimkumbushe Rizz je Unakumbuka Kizazi cha Mabutu kilivyopotea katika ramani ya Dunia hii? Lkini leo hii ni nani anaweza kusimama mbele akajinadi kama mtoto wa Sadam Husein?
    Watanzania wanakeleka na michongo hiyo. One Day yes.
    NI MIMI MTOTO WA MASKINI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...