JK na mgombea ubunge jimbo la Rombo Mh. Basil Mramba wakikupa dole tupu wakati wa mkutano wa kampeni huko Tarakea leo
JK akisalimiana na wanafamilia wa Mh. Mramba alipowasili Tarakea leo
JK akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango alipofanya mkutano wa kampeni tarafa ya Ndungu kwenye jimbo hilo. Umati wa wanaCCM ukiongozwa na Mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki,Anne Kilango wakimsubiri JK awasili kwenye uwanja wa mkutano akitokea Mombo mkoani Tanga.
Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakimshangilia JK wakati akimwaga sera katika jimbo la Same Mashariki leo.
JK akipokea ilani ya uchaguzi ya Rombo kutoka kwa mgombea ubunge wa Jimbo hilo Mh. Basil Mramba wakati wa mkutano wa kampeni leo
wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Rombo,wakimsikiliza JK alipokuwa akiwahutubia katika jimbo hilo leo.
wanachama wa CCM jimbo la Rombo wakimshangilia JK uwanja wa Tarakea leo

Kinamama wa Rombo wakimlaki JK uwanja wa Tarakea leo

Mgombea ubunge wa CCM wa Jimbo la Rombo anayetetea kiti chake jimboni hapa Mheshimiwa Basil Mramba amemmwagia sifa nyingi Mheshimiwa Kikwete kwa kasi yake ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na kuleta mafanikio mengi wilani Rombo.


Mheshimiwa Mramba aliyasema hayo kwenye mkutano mkubw awa kampeni Tarakea ambapo aliainisha kwa ufupi sana mafanikio hayo kwenye maeneo mbalimbali.

1. Ujenzi wa barabara ya lami; imeunganisha Rombo na wilaya ya Moshi Vijijini na maeneo mengine ya mipakani mwa wilaya. Barabara zote ni za kiwango kizuri na zinapitika wakati wote mwaka mzima.

2. Upanuzi wa Elimu ya Sekondari; Mwaka 2005 wakati ilani ya CCM iliagiza shule moja ya sekondari kwa kila kata Tanzania, Rombo ilikuwa tayari ina shule hizo. Lakini kwa nguvu ya utekelezaji wa ilani hiyo, Mheshimiwa mramba alisema kwa sasa Rombo ina Shule 41 za sekondari za kata. Shule kumi bora za mkoa wa Kilimanjaro, tano ziko Rombo. Aliongeza kuwa, mafanikio hayo yametokana na jitihada binafsi za wana Rombo kusambaza vitabu, walimu wa ziada waliomaliza kidato cha sita n.k. Kila mwaka wilaya ya Rombo inatoa zaidi ya wanafunzi 500 kwenda sekondari na 500 kuendelea na elimu ya juu. Mheshimiwa Mramba alisema mafanikio haya ni makubwa mno kwa ngazi ya wilaya na yasingetekelezwa kama si jitihada za Mheshimiwa Kikwete.

3. Upatikanaji wa Maji: Wilaya ya Rombo ni mojawapo ya wilaya chache Tanzania ambapo maji yanatiririka mwaka mzima kwa ujazo wakutosha.
4. Upatikanaji wa Umeme:

Mheshimiwa Mramba alieleza umati mkubwa wa watu kwamba hivi karibuni wilaya ya Rombo itakuwa na umeme wa kutosha kutoka na mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA). Kuanzia mwisho wa mwaka huu, umeme utasambaa kwenye kila kitongoji wilaya ya Rombo.

5. Kilimo: Mafanikio makubwa yamepatikana kwenye kilimo cha kahawa na ndizi ambayo ndio mazao makuu ya chakula na biashara. Kuna mpango wa kuanzisha kilimo cha matunda kwenye ngazi ya kaya. Alisema jitihada hizi zitasaidia wakazi wa Rombo kujiongezea kipato na matunda yawe kama zao la biashara wilayani hapo.

6. Mwisho Mheshimiwa Mramba alimshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kusimamia ujenzi wa barabara kubwa ya lami inayopita wilayani Rombo. Na alitoa ombi kwa mheshimiwa Kikwete kusaidia katika jitihada za wana Rombo kupambana na umasikini kwenye ngazi ya kaya, ili kila Mtanzania wa Rombo aondokane na umasikini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. hafungwi mtu hapo

    ReplyDelete
  2. Huyo mgombea wa Rombo ni mwisi sana!!Acheni kufuga mafisadi!!

    ReplyDelete
  3. Huyo wa Rombo ni Mwisi, Fisadi!!

    ReplyDelete
  4. Wa Rombo ni mwisi, fisadi!!

    ReplyDelete
  5. Siasa ya nchi hii very interesting!!!
    Huyu Mramba hakupaswa kuwepo kwenye kampeni in first place. Kinachomsaidia ni kuwa "he knows too much" .
    Ni lie hadithi ya asiye na dhambi na awe wa kwanza kutupa jiwe .....

    ReplyDelete
  6. hivi bwana michuzi vyama vingine vimeacha kufanya kampeni au vipi mbona hutuwekei au unataka sisi tulio mbali tuamini CCM ndio bora lol

    ReplyDelete
  7. HAO WAWILI TU YANI RAIS NA MRAMBA WAMEFICHA BILION 400 PEKE YAKO. 400 BILLIONS COMBINATION. NA MTAKOMA WATANZANIA

    ReplyDelete
  8. Hivi ni mtanzania gani aliemjinga kutojua kama Basil Mramba anakesi ya ufisadi mahakamani..Rais nae eti anamshika mkono kumnadi mbele ya wananchi. Huu ni ujinga kwa wananchi na viongozi wa chama husika.

    ReplyDelete
  9. Hivi ninyi watu wa Rombo mtadanganyika hadi lini? Mtu anatuhumiwa na Taifa zima alafu nyie mnaendelea kumshangilia. Mnatia aibu Wachagga

    ReplyDelete
  10. Phatlorenzo, MNSeptember 16, 2010

    Mramba kama Kikwete wote ni wana siasa na wana siasa watapongezana hadharani kwa kazi nzuri hata kama hawapendani. Mlitegemea Mramba aseme Kikwete anatetea baadhi ya mafisadi?
    -Phatlorenzo-

    ReplyDelete
  11. MNASHANGAA YA MUSA??? YA FIRAUNI JE???.....WATANZANIA MTAKOMA NA MTAJUTA MILELE.........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...