JK akiwapungia wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa muendelezo wa mkutano wa kampeni mkoa kwa mkoa.Mwenyekiti wa Chadema wa kitongoji Miseyeki Selei (maarufu kama Masaai) akimkabidhi JK kadi za Chadema na kusema kuwa yeye na wenzake 42 wameamua kuagana na upinzani kwa sababu ya kukosa maendeleo kwa muda mrefu.Mheshimiwa Kikwete akipokelewa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Hai kabla ya kuhutumia maelfu ya watu waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wake mkubwa wa kampeni Bomang'ombe.
JK akisalimiana na vijana wa Kwasadala ambapo aliwashangaza wengi aliposhuka na kujichanganya na wananchi wa mahali hapo.
Kina mama wana CCM wa Hai wakiwa kwenye uwanja wa mkutano wa Bomang'ombe wakishangilia wakati msafara wa JK ukiwasili katika uwanja wa Bomang'ombe.
Maelfu ya wananchi waliofurika kwenye uwanja wa mkutano wa Bomang'ombe kumsikiliza Mheshimiwa Kikwete alipowasili kwenye mkutano mkubwa wa kampeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. October 31, 2010 ndiyo mwisho wa dakika tisini naona wachezaji hawa danadana nyingi mno.

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi turushie picha za jk monduli pliz

    ReplyDelete
  3. Anko Michuzi, Dawson hapa. Unanishangaza sana jinsi unavyoandika mfano ikiwa ni ccm unasema maelfu ya wananchi lakini ukija upande mwingine unasema mamia ya wananchi wakati kimtazamo idadi inaweza virtually kua sawa. Bila kupotezeana muda naomba ufafanuzi na pia usinitupe kwenye trash bag maana sijaongea rabish. Ni hayo tu
    Ndimi mtiifu Dawson from Washington D.C baby

    ReplyDelete
  4. Issa, siku hizi wewe ni mpiga picha wa chama cha mapinduzi? Umehama Serikalini?

    ReplyDelete
  5. Ankal, nakadiria kuwa tulikuwa zaidi ya watu 70,000!!!! hapa A Taun tuna mwamko: Hatuwezi kukubali kurubuniwa na kugawanywa. Japokuwa mimi ni Mkibosho halisi, lakini nimekwishawaambia wakibosho wenzangu tuepuke siasa za ukikuyu isije kutupeleka pabaya. Mwenzako akinyolewa (Kenya) si lazima utie kichwa chako maji. Tunaweza kuukataa utengano unaohubiriwa kwa vitendo na chadema. O. M. Machinjioni ya magari. A-town.

    ReplyDelete
  6. Big up Michu. Hii ni blog yako, wasioipenda wahame (they can go to hell for all I care). Wasikuyumbishe hata wakikutukana. CCM DAIMA. Mwana CCM. Niko Kiborloni Moshi.

    ReplyDelete
  7. haki ya nani we dawson umenichekesha sana, yani humu ndani watu wako makini kweli, ankal unalo safari hii hadi kampeni ziishe manake dah, mara jana umeambiwa unaficha kofia ya kijani na kweli na mie kuchunguza nikaiona ulikuwa umeiminya maeneo flani ha ha haaaaaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...