JK akiwapungia wanachama na wapenzi wa CCM waliojitokeza katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa muendelezo wa mkutano wa kampeni mkoa kwa mkoa.
Mwenyekiti wa Chadema wa kitongoji Miseyeki Selei (maarufu kama Masaai) akimkabidhi JK kadi za Chadema na kusema kuwa yeye na wenzake 42 wameamua kuagana na upinzani kwa sababu ya kukosa maendeleo kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Kikwete akipokelewa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Hai kabla ya kuhutumia maelfu ya watu waliofika kumsikiliza kwenye mkutano wake mkubwa wa kampeni Bomang'ombe.





October 31, 2010 ndiyo mwisho wa dakika tisini naona wachezaji hawa danadana nyingi mno.
ReplyDeletekaka michuzi turushie picha za jk monduli pliz
ReplyDeleteAnko Michuzi, Dawson hapa. Unanishangaza sana jinsi unavyoandika mfano ikiwa ni ccm unasema maelfu ya wananchi lakini ukija upande mwingine unasema mamia ya wananchi wakati kimtazamo idadi inaweza virtually kua sawa. Bila kupotezeana muda naomba ufafanuzi na pia usinitupe kwenye trash bag maana sijaongea rabish. Ni hayo tu
ReplyDeleteNdimi mtiifu Dawson from Washington D.C baby
Issa, siku hizi wewe ni mpiga picha wa chama cha mapinduzi? Umehama Serikalini?
ReplyDeleteAnkal, nakadiria kuwa tulikuwa zaidi ya watu 70,000!!!! hapa A Taun tuna mwamko: Hatuwezi kukubali kurubuniwa na kugawanywa. Japokuwa mimi ni Mkibosho halisi, lakini nimekwishawaambia wakibosho wenzangu tuepuke siasa za ukikuyu isije kutupeleka pabaya. Mwenzako akinyolewa (Kenya) si lazima utie kichwa chako maji. Tunaweza kuukataa utengano unaohubiriwa kwa vitendo na chadema. O. M. Machinjioni ya magari. A-town.
ReplyDeleteBig up Michu. Hii ni blog yako, wasioipenda wahame (they can go to hell for all I care). Wasikuyumbishe hata wakikutukana. CCM DAIMA. Mwana CCM. Niko Kiborloni Moshi.
ReplyDeletehaki ya nani we dawson umenichekesha sana, yani humu ndani watu wako makini kweli, ankal unalo safari hii hadi kampeni ziishe manake dah, mara jana umeambiwa unaficha kofia ya kijani na kweli na mie kuchunguza nikaiona ulikuwa umeiminya maeneo flani ha ha haaaaaa!
ReplyDelete