JK akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Dr. Harisson Mwakyembe katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani humo jana.
JK akiwa katika vazi la uchifu mara baada ya kusimikwa na chifu mkuu wa Mbeya akishirikiana na machifu wa wilaya zote za mkoani humo.
JK akisimikwa uchifu
umati mkubwa ulifurika kuja kumsikiliza JK wakati alipohutubia Mbeya mjini jana.

kwa picha zaidi
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Michuzi plz rekebisha maelezo ya picha mfano JK akimnadi mgombea Mwakwembe = Mwakyembe (2) JK akisimikwa Uchimu =Uchifu. mjomba vipi au swaumu imekushika vilivyo?
    mdau Paka la Jikoni UK.

    ReplyDelete
  2. Michu inaonyesha uraia wako na wewe una utata maana kiswahili kimeenda kushoto. inaonyesha wewe ni mzambia itabidi tumuone Lawrence Masha athibitishe Uraia wako.

    ReplyDelete
  3. Hongera mdau hapo juu kwa uchunguzi na maoni yako!! Pia mjomba rekebisha hilo neno "Anguma" sijui kama ulikuwa ukimaanisha "Aunguruma" kama ni neno jipya tunaomba maana yake. Mdau wa Kiloleli-Mwanza

    ReplyDelete
  4. Amesharekebisha jamani huyu ni raia wa Tanzania,msimshtaki kwa Makamba na Masha

    ReplyDelete
  5. DAH!!!!
    KWA MTAJI HUU SISI WAPINZANI KAMA HATUNA CHETU VILE.MAANA VIONGOZI WETU HAWAZUNGUKI SANA VIJIJINI UPINZANI UNABAKI MJINI TU. MASIKINI LI-PUMBA NA SILAHA.

    ReplyDelete
  6. Kwa kwa kwa kwa kwa kwa, wadau mmepinda!

    ReplyDelete
  7. Asalaam aleika!
    Ankal, ili jambo la baadhi ya wagombea waliopita na hawatohitaji sanduku la kura naona halijakaa vema,kumthibitisha mgombea apite bila kupingwa haileti demokrasia ya kweli, mbona JK alikuwa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro cha urais ccm lkn alipigiwa kura??linaleta harufu ya rushwa,coz kuna tetesi wagombea wengi wa upinzani uko mikoani ni njaa kwenda mbele,kwahiyo ni rahisi kununuliwa. Ningependa tume ya uchaguzi ipitie upya sheria hii, wananchi wapewe nafasi ya kupiga kura ili tujue wangapi wanaunga mkono au la.

    ReplyDelete
  8. Picha ya mwisho depicts a creative photographer....hongera kaka michuzi

    ReplyDelete
  9. kale kasebe kake! katamu kweli ! che! che!
    heti Akima mama wote tumchague!
    kiitikio: Jakaya kikwete
    Akibaba wote tumchague!
    Jakaya Kikwete
    Vijana na wazee tumchague
    Jakaya Kikwete
    Tanzania! Kikwete! Tumchague! KIkwete
    Wimbo mtamu kweli

    ReplyDelete
  10. Hongera CCM , hongera JK, hongera wabunge wa Mkoa wa Mbeya.Bila ya umoja wa hawa wabunge wa CCM Mbeya ingepata matatizo katika uchaguzi huu.
    Umoja wa wananchi na wabunge wa CCM wanaibeba kwa sana CCM mkoani Mbeya, wananchi tupo nyuma yenu kuwashinda wapinzani ambao hawaoni ndani.

    ReplyDelete
  11. hiyo picha ya mwisho ,mbona watoto watupu au ni UPARENI ..hapo nasikia kuna hadithi ..baba wa taifa alikosa kura UPARENI ..alifanya mkutano wa kampeni kwakuwa wapare wana maumbo madogo alifikiri ni watoto watupu wamekuja mkutanoni..akawaambia.."NYIE WATOTO HAMRUHUSIWI HAPA NENDENI MKAWAITE WAZAZI WENU...watani zangu wapare wakaja juu ,..Atheee huyu mtheeee anatutukana ..

    ReplyDelete
  12. Siasa iko complicated manake samtaim inabidi ushikane mikono na maadui wakubwa wa maswahiba zako.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  13. SIO WOTE LAKINI WANAKUJA KWA NIA YA KUKIPENDA CHAMA CHA CCM WENGINE WANAKUJA KUMUONA JK SIUNAJUA MIKOANI KUMUONA RAIS NI BOMBA LA UJIKO NA HATUA KUBWA KWA HIYO UMATI USIKUOGOPESHE EHEHEHH

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...