
JK akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha, Edward Lowasa kwa wapiga kura wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa kampeni.

JK akihutubia wananchi wa jimbo la Monduli mkoani Arusha jana jioni.

Mkazi wa jimbo la Monduli mkoani Arusha, akiwa ameketi jirani na bango lenye ujumbe wa wagombea wa CCM nafasi za Urais, Ubunge na udiwani kupata asilimia 99, wakati wa mkutano wa kampeni uliohutubiwa na JK jana jioni.

JK akiwahutubia wakazi wa mji wa Namanga(mpakani mwa Tanzanani na Kenya) jioni ya leo wakati wa mkutano wa kampeni.

JK akimpatia zawadi mmoja wa watoto waliokuwepo katika mapokezi yake alipokuwa akiwasili katika mji wa Namanga,Arusha jioni ya leo.

JK akiwasalimia watoto

Wananchi wa jimbo la Monduli mkoani Arusha, wakinyanyua mikono juu kuonyesha kumuunga mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, wakati akihutubia mkutano wa kampeni jimboni humo.

kina mama wa kabila la Wamasai wakiimba nyimbo za kukisifu chama cha CCM na kumsimfu JK wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jioni hii katika mji wa Namanga jijini Arusha.

watu kibao wakiwa wamefurika kumsikiliza JK leo.
raisi wetu kikwete unaona jinsi watu wa umasaini wanakavyo kupenda. tafadhali make sure ile barabara ya kutoka arusha mpaka musoma inajengwa ili wamasai wa hizo sehemu nao wapate maendeleo. hao wakenya wanajenga barabara kila sehemu nchini mwao na hakuna mtu anawapinga. wana lobby kwa wazungu ili wawatetee. wanachotakia tanzania ni kuzidi kuwa maskini ili waje kuwanyonya.
ReplyDeletechagua kati ya maendeleo na utamaduni
ReplyDeleteFikra hizo ndio maana hazitupeleki mbali. Nani kakuambia huwezi kuendelee ukimaintain utamaduni wako.
ReplyDeleteKasumba kama hizo ndio zinatofunya tukimbilie kila kitu anachofanya mzungu kama ni "maendeleo". Hivi na exposure yote unayopata hujaona society ambazo zimeendelea wakati zikidumisha utamaduni?
Yaani karibu robo tatu ya watu hawa walikuja kwenye kampeni hii ya JK ilikuwa kwa kushinikizwa na kupatiwa usafiri wa bure... huko kwa Slaa, watu hushiriki kwa ridhaa yao.. Hii ndiyo tofauti ya wahiriki wa Kiwete na Slaa.
ReplyDeleteAlly Hamis
Rais wetu mpendwa JK, Sisi wananchi wa mkoa mzima wa Manyara (minus Karatu)na mkoa mzima wa Arusha tuko bega kwa bega na wewe na chama chetu CCM. Ndiyo maana tumekataa kurubuniwa na chadema ambao wamejaribu kutugawanya kwa misingi ya dini. Pamoja CCM tutashinda nguvu ya giza chadema inayotaka kutugawanya Watanzania.
ReplyDeleteMorani Halisi, Madukani, Monduli.
Laiti baadhi ya masetla wa kichaga wasingekuwa wanafanya mikutano yao kwenye vikao vya mbege ambako wanatumia lugha yao kuikampenia chadema, chadema wasingelipata matatizo ya kuchukiwa Monduli. Lakini kwa kuwa wameamua kuonyesha ukabila waziwazi hatutakipigia chama chao kura ng'o. Ole Saibul junior.
ReplyDeleteINAKUWAJE TANA FISADI ANAENDELEA KUNADIWA?LOWASA NI FISADI NA MUDA WAKE WAKUENDELEZA UFISADI UMEISHA NINI SASA ANATAKA?PUNZIKA BABA UFAIDI MAPESA YAKO YA RICHMOND.
ReplyDeleteUchaguzi huu ni kati ya maskini na matajiri. Go figure who is who?
ReplyDeleteNinamheshimu Mhe.J.Kikwete binafsi kwa kuwa ni mtu straight up...hana ukabila wala udini...wapinzani particularly Slaa wanajaribu kushinda uchaguzi kwa kutugawa kwa ukabila etc,....yet Kikwete anafumbia macho hii kitu na kuendelea kutuomba kura kwa kutuunganisha,...Mungu ambariki. Besides, He is the only president who has openly discussed the union issues...it was so clever of him to make the VP the chair of the union affairs. Kikwete is the only candidate I see who can walk us thru the millenium goal challenges/goals.Tumpigie kura huyu jamani and kwa wale mnaotaka kuwapa nafasi wapinzani pls do so as well.
ReplyDeletehaukatazwi kusema binadamu..ila ukweli wa mambo ni ccm itashinda katika uchaguzi wa mwaka huu,tena kwa kishindo.
ReplyDeleteNa ulie muita Lowassa fisadi...hayo ni maneno tuu hata kwenye khanga yapo.
Lowassa nae atapita tena mwaka huu..
habari ndo iyo.
CCM oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee...