MAMBO UNCLE MISUPU?
NATARAJI UPO MZIMA NA UNAENDELEA VYEMA NA KAMPENI ZA 2010,MIMI MDAU MKUBWA WA BLOG YETU YA JAMII,UNCLE NINAMSHUKURU MUNGU KWA KUPATA SAFARI YA KWENDA KUBADILISHA MAZINGIRA KIDOGO UJERUMANI KWA MUDA WA WIKI NA NUSU AMBAPO NAANZA WIKI IJAYO.
LENGO LANGU LA KUKUAMBIA HIVI NI KWAMBA NAOMBA UTARATIBU WA KUPATA BENDERA ZA VYAMA VYA SIASA VINAVYOSHIRIKI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI WA RAIS HAPA NCHINI NIENDE NAZO HUKO ILI “PWEZA PAULO”AKATABIRI NI CHAMA GANI KITASHINDA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA MWAKA HUU!
NITASHUKURU KWA MSAADA WAKO NA NINAKUHAKIKISHIA NITAPIGA PICHA NA NITAKUTUMIA ENDAPO PWEZA PAULO ATAKAPOTABIRI,WADAU NAOMBA MAONI YENU PIA.
MDAU Ngulla Senior.
Kaka sema tu unataka tujue kuwa unakwenda Ujerumani. Wewe huna uwezo wa kumuona Pweza huyo. Vilevile kama bendera sio lazima Misupu akutafutie, wewe mwenyewe msongo utatafuta. Kweli tembea uone mengi. Salamu zao Ujerumani. Mimi ni Mzee wa Kunyorosha
ReplyDeleteNdugu Ngula nakupongeza kwa kubadili mazingira. Mimi nipo hapa Ujerumani sasa sijui wewe unaenda jimbo gani. Kama unaenda Berlin hutakutana na paulo ze pweza kwani yeye yuko Badenwotemberg state kwenye mji mdogo tu unaitwa oberhausen kwa sababu uko juu ya milima. Mji huu uko jirani na stuttgart ambako ni makao ya jimbo nami niko hapa unaweza kunitafuta kwa namba +4917637304142 ni mobile phone.
ReplyDeletewewe wacha usanii wako. mimi nina kuambia huna aja ya pweza wala mganga wa kienyeji ushindi utakwenda ccm. ccm tu na hakuna chama kingine period.
ReplyDeleteUShirikina mtupu
ReplyDeleteWewe acha kupoteza muda wako. CCM itashinda hata iwaje kama mimi CHADEMA au CUF wala sipigi kura. Hata CCM ikishindwa kura zitageuzwa na watapewa ushindi. Wananchi wakianza kupiga kelele Obama atasema waweke kikao cha upatanishi. Wapinzani watapewa chao na CCM itaendelea kutawala. Wewe nenda huko beba box urudi na nepi za watoto.
ReplyDeleteHHE KUMBE VYAMA VINGINE VINAAMINIKA KWAKUIBA HATA KURA BASI DEMOKRASIA IKO LIKIZO BONGO NA WANGALIZI WAKIMATAIFA HUWAWANAKUJAKUMBE KUTALII AU NA WAO WANATA PER DIEM HUHU KWELI MALARIA HAIKUBALIKI
ReplyDelete